Maggid Mjengwa: Nape Hakwenda Na Midundo, Ilikuwa Ni Lazima Aondoke

Maggid, utu uzima ni dawa, na ndani ya maandishi yako nimeuona ukomavu wa uandishi ambao huwezi kuuona wakati mtu unaposoma maandishi ya vijana wengi wanaojawa na mihemko.

Nilimwambia mtu mmoja kwamba kaka Nape hawezi tena kuendelea na cheo chake siku ile ile alipotoa ushirikiano wa hali ya juu kwa clouds media.

Waziri huwezi kubariki aina fulani ya uasi kwa wadau wa wizara yako halafu ukaendelea kustahili kuwa na cheo ulichonacho.

Lakini Nape bado kijana naamini anazo nguvu nyingi za kufanya mambo mengi mbeleni, iwapo atapewa nafasi na mkuu kabisa.
 
haaaaa, inaonesha ule utafiti wa 1 kati 4 hauko sahihihi, mi nadhani kati ya Watz 4, watatu ni machizi. Unamlaumu rais akitofautiana na mtu anamtumbua, ww mtu akitofautiana mawazo unamtukana (mjinga, mpumbavu, mshenzi nk) hivi wazimima ss kweli?
 
kwa hiyo mjengwa unataka kutuambia nape alipaswa kukaaa kimya kuipotezea ile issue?sio sahihi na kama upo hivyo unapitwa na wakati sasa ki mawazo
 
Mimi sioni sababu ya clouds kutengeneza hii story Maana there is a high price for them to pay hakuna mtu especially mfanyabiashara anayependa ugomvi na serikali hata kidogo Makonda amewakosea hawa watu period!!
 
Huko sahihi kabisa Mjengwa hata mh. raisi leo amesema 'haiwezekani mtu anatoa habari ili serikali iandikwe vibaya alafu anashangilia' Nape amechagua alichokipata,ndio basi tena.
 
Hivi aliyofanya makonda ni sahihi? Kuvamia kituo cha redio na hili sakata la vyeti ni Mambo ya kawaida eti? Hata kama nape ana makusud yake lakin pia tuangalie kama anachokipigania kina uhalali au vp

Du hivi kweli huwa mnasomaga au nakuwa kama mmebanwa na kitu. Moja je ni kosa mtu kutoa hoja yenye mantiki. Mbili kama huelewi ukikaa kimya utakufa. Tatu. Unasema uhuru wa kuongea sasa wewe kinakuma nini kisa hukutaka ukweli unataka kuchezewa sharubu. Kuna watu hamna akili mpka kinyaa. Katoa hoja kutokana mada yake sio yako kichwani na wala mada yake haikuwa ya makonda kama makonda. So long as you are in Tanzania. Na wewe kama kweli upo Dar. Itapaswa ufuate sheria. Kama hutaki toa kificho nenda kamtukane huyo makonda ikulu ya mkoani kwenu. Ndo ujue. Nyie ndo akina harmo rapa. Waoga ila mnajificha hapa haman hoja matusi tu. Afu uhuru. Humpendi mtu kila siku kumzungumzia ni dalili ya upendo hiyo. Negation of negation is affirmation. - - =+
 
kwa hiyo mjengwa unataka kutuambia nape alipaswa kukaaa kimya kuipotezea ile issue?sio sahihi na kama upo hivyo unapitwa na wakati sasa ki mawazo
Nape alikosea mazingira ya kubishana na Makonda, yeye km waziri anavikao rasmi mfano vikao vya baraza la mawaziri kule ndipo alitakiwa akamkaange makonda ila akachagua kuivua nguo serikali, serikali haifanyi kazi hivyo labda alikua anadhani bado ni mwenezi wa ccm
 
Eti magufuli kachukizwa na Heading za magazeti ya leo, Anadai jamaa aliyetoa bastola alifanya hivyo kwa utashi wake , serikali haihusiki na kile alichofanya.

Nadhani alitegemea sinema yake ya kichina ya jana itapewa promo. Cha ajabu ilipoteza mvuto kabla haijafika kwa walaji.
 
Duh!! Tumefikia pabaya sana watanzania,mtu akitoa mawazo yake kama mtanzania anaonekana adui.
Majid katoa mawazo yake na sio vizuri kumuona adui.
Hongera sana majid mjengwa ujumbe umefikia.
umefika kwa mamako
 
View attachment 485993

Kwa tunaofuatilia mambo hii ni habari iliyokuja kwa kuchelewa. Kwangu mimi ni siku ile Rais wa Jamhuri alipoongea Ubungo kwamba Mkuu wa Mkoa Makonda aendelee kuchapa kazi, na baadae Waziri wake wa Habari anatangaza tume kumchunguza Makonda. Nape angemsaidia Rais kwa kuvunja alichokiunda kwa maana ya Tume. Kisha kujiuzuru, basi.

Maana, kwenye Jamhuri, hakuna uwezekano wa jambo kama lile kufanywa na Waziri na akabaki kuwa Waziri. Nape ambaye alipaswa, Kama Waziri wa Habari, kuwapo pia kwenye tukio kubwa kitaifa kama lile la uzinduzi wa ujenzi wa flyovers pale Ubungo mbele ya Rais wa Benki ya Dunia. Angeshiriki, angesikia msimamo wa Rais wake kuhusu RC Makonda, na angekuwa na mawili tu ya kuchagua, kumuunga mkono Rais wake au kujiuzuru.

Nayaona manne makubwa:

1. Kutofautiana kwa Nape na Makonda katika suala la Wema kutajwa kwenye orodha hadi kufikia kupigana vijembe kumekuwa na athari kubwa. Hakuna dhambi ya kutofautiana, lakini, kulikuwa hakuna maana ya kuendelea kupigana vijembe.

2. Tume ya Nape kumjumuisha mhariri ( Balile) ambaye gazeti analoliongoza lilibeba habari dhidi ya Makonda katika siku hiyo hiyo ya kutajwa kwa Kamati na ni mhariri huyo huyo ndiye aliyesoma ripoti. Hilo lilikuwa na walakini mkubwa.

3. Umoja wa ghafla wa watu wasiopikika chungu kimoja kutaka Makonda atumbuliwe ( Rejea goli la mkono). Hili linaleta mitazamo mipya kwamba huenda suala zima lina siasa ndani yake. Kwa pamoja inajengeka dhana ambayo haipaswi kupuuzwa, kuwa zoezi zima lilichukuliwa kwa maslahi binafsi zaidi kuliko linavyoelezwa hadharani. Ni kweli, na tumesikitishwa sana na kitendo cha RC Makonda alichofanya pale Clouds TV.

RC Makonda alilikoroga na alistahili Kukemewa, lakini, hiyo usitutie upofu kushindwa kuyaona mashimo kwenye mchakato wa kushuhulika na mapungufu ya RC Makonda. Mchakato usiwe uliojaa mashaka, na mashaka haya huondolewa kwa wenye kuyashuhulikia kutanguliza weledi na kuweka kando yasiyohusika.

Hata tunapozungumzia dhana ya kugomea habari za RC Makonda si sahihi. Kimsingi tunaweza kugomea habari za Makonda lakini si RC Makonda. Habari za RC Makonda ni habari zenye kuhusu Serikali na Wananchi. Habari za Makonda kama Makonda, iwe amekwenda kucheza muziki au harusini hizo zinabaki kuwa habari za Makonda.

4. Hili la nne ndio kosa kubwa alilofanya Nape; Kuendelea na zoezi lake hata baada ya Rais 'kufunga mjadala'. Kama Waziri wa Habari, Nape ni Msemaji Mkuu wa Serikali inayoongozwa na aliye madarakani. Katika kazi hiyo, na kwenye Jamhuri, wakati mwingine Waziri wa Habari husema ' Kama kasuku' , kile kilichosemwa na Rais, hata kama ukikaa naye pembeni anaweza kukwambia kuwa hakubaliani nacho.

Hitimisho, uamuzi wa kumtoa Nape kwenye Baraza ni sahihi ili kurudisha nidhamu na mtiririko mzuri wa utendaji kiserikali.

Nape Nnauye ameshindwa kuendana na midundo au kusaidia kupanga midundo ya kwenda pamoja na aliye juu kwenye Jamhuri na Serikali kwa ujumla.

Katika wakati nchi iko kwenye utekelezaji wa miradi mingi midogo na mikubwa huku ikikopa kugharamia hayo. Ni mikopo ya Watanzania kuilipa, si ya Magufuli. Inahitajika hamasa kubwa ya kuwafanya Watanzania wafanye kazi. Waziri wa Habari ni mmoja wa watu wa kuifanya kazi hiyo.

Ni imani yangu, kuwa Nape ni kijana, mahiri na mwenye ushawishi mkubwa. Anahitaji kutulia na kutafakari namna atakavyoweza kuisaidia Chama chake na nchi kwa nyakati zijazo.
Fala ww
 
Magid naona hajielewi zaidi anajitafutia kick kwa mgongo wa Nape.
Hai hitaji kukaa darasani na kuisoma sura ya Nape. Nape hakua mfuasi wa midundo ya boss wake. Nape alichoshwa na midundo ya bosi wake, na kisha midundo hiyo ikaanza kurindima kwake kama kelele.
Haikua bahati mbaya kwa nape kuyafanya Yale yalio jiri.
Tafakari
Naunga mkono hoja kwa 100% Nape alichoka na Udikteta hakupenda kuwa sehemu ya unyanyasaji wa vyombo vya habari, sasa watu watashuhudia mwakyembe akiyafungia magazeti kibao na Udikteta juu ya habari utakuwa wa kutisha
 
Kupingana na matakwa ya Rais ni uhaini.....Nape alistahili kufukuzwa kwa kutaka kumdhalilisha mteule wa rais RC Makonda
Kama waziri... nape alifuta hatua zote za kuhakikisha habari hii inamfikia mkuu kwa utash zaidi.
Lakin mkulu alikuwa na hila zake tu.. sijaona mahali nape amekosea.. ni hila za yeye na mwanaye.
 
Leo ndo nimemjua Mjengwa vinzuri,siamini no yeye kaandika upuuzi huu.
Haki siku zote ina gharama ila tofauti huwa ni kiwango tu. Mandela akikaa gerezani miaka 27. Yesu Kristo alisulubiwa pale golgota ili kujenga daraja kati ya mwanadamu na Mungu. Huyu kijana alijua na amekubali kupoteza u waziri kwa ajili ya kutetea haki inayominywa na mungu mtu anayejiona yuko sahihi kila saa na ktk mazingira yote. Hauwezi kumtetea std 7 na form 4 failure ambaye kafoji vyeti ili apate ajira na bado ukaona uko sahihi. Ninapata hisia ya kiroho kwamba siyo bure. Yako makusudi ya Mungu ktk jambo hili
 
Kwa hiyo hata kama wananchi wanaonewa watu waende tu na midundo ya raisi du kweli wewe ni
Mwandishi au
 
Back
Top Bottom