JMP Mchungu
Member
- Jun 30, 2015
- 49
- 125
Bidhaa za magendo na Magari ya kifahari zaidi ya 20 vimekamatwa katika mpaka wa Holili uliopo wilaya ya Rombo
=====
Gabriel Mwangozi, meneja TRA mkoa wa Kilimanjaro amesema magari hayo yanatofautiana makosa, mengine yalibeba magendo ambapo mengine yatatozwa faini na mengine yakitaifishwa kutokana na urudiaji wa kosa au kuangalia ukubwa wa kosa lenyewe.
"Magari mengine, watu wengine waliingiza tu bila kujua. Anaingiza analeta, amenunua tu huko gari lake, kwa mfano ile Amarok, kuna kijana alikuwa anasoma South Africa. akaona amependa gari akainunua akajua akishanunu akija nalo hapa tu haina shida na akawa anaitembelea, likawa limekamatwa kwa sababu muda ule uliokuwa utatakiwa ukawa umeshapita na taratibu ambazo alitakiwa afanye hakuzifanya" Alisema Gabriel
Mkuu wa wilaya ya Rombo, Dr. Athuman Kihamia anasema licha ya kukamata bidhaa za magendo bado haijawa dawa kwa waingizaji wa bidhaa hizo.
Pia wapo wanaojaribu kutumia wafanyakazi hasa wa chini kuwarubuni kwa njia moja au nyingine. Dr. Kihamia kasema wote hawako salama na kusema hata wanaopitisha bangi wanawafahamu na kama wamefanikiwa kupita bahati mbaya wasiwadanganye wenzao kwamba kunapitika.