Kilimanjaro: Mapipa 50 ya kemikali na simu 1,076 za magendo vyakamatwa mpakani mwa Tanzania na Kenya

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro imeendelea na operesheni dhidi ya biashara za magendo mipakani ambapo imekamata mapipa 50 yenye jumla ya lita 12,500 za kemikali (spirit) yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 15.5 ilyokuwa ikisafirishwa kwenda nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza na wanahabari leo february 26.2020, Meneja Mamlaka ya mapato Mkoani wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi amesema mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti upitishwaji wa biashara za magendo zinazoingizwa na kutolewa nje ya mipaka kwa kutumia njia zisizo rasmi na kwamba wamejipanga usiku na mchana kuhakikisha vitendo hivyo vinadhibitiwa kikamilifu.

Amesema katika operesheni hiyo wamekamata pia simu 1,076 za viganjani aina ya Itel zenye thamani ya zaidi ya sh14.8 milioni katika mpaka wa Holili uliopo Wilaya ya Rombo zilizokuwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria.

Mwamgosi amesema bidhaa zote na magari yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa hizo yanashikiliwa na mamlaka hiyo huku taratibu za kisheria zikiendea kuchukuliwa juu ya uvunjifu huo wa sheria.

JIFUNZE;
Ushuru wa bidhaa

Ushuru wa bidhaa ni kodi inayotozwa kwa bidhaa au huduma maalum zilizozalishwa ndani ya nchi au kuingizwa nchini kwa viwango tofauti. Kodi hii inatozwa katika viwango maalum na viwango kulingana na thamani.

Vitu vinavyotozwa viwango maalum ni pamoja na:
Mvinyo, vinywaji vikali, bia, vinywaji laini, maji ya chupa, juisi ya matunda, Dividii, Visidii, Sidii na kanda zilizorekodiwa sauti, sigara, tumbaku, bidhaa za petroli na gesi asilia.

Vitu vinavyotozwa kulingana na thamani yake ni pamoja na:
Huduma za kutuma na kupokea fedha, huduma za mawasiliano ya kielektroniki, malipo ya huduma za televisheni, samani zilizoingizwa kutoka nje, vyombo vya moto, mifuko ya plastiki, ndege maalum, silaha za moto, makasha maalum, vipodozi na dawa.

Viwango kulingana na thamani ni: 0%, 5%, 10%, 17%, 15%, 20%, 25% ,30% na 50%.
 
Back
Top Bottom