Magazeti yana njama na kafulila? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti yana njama na kafulila?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnmashilatu, Jan 13, 2012.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Tangu kutolewa uamuzi wa halmashauri kuu ya NCCR mageuzi kumvua uanachama mbunge wa kigoma Kusini Bw David Kafulila, baadhi ya magazeti ynatia shaka kwa jinsi yanavyoripoti suala hilo

  Sina nia ya kuingilia uhalali wa uamuzi huo wa NCCR mageuzi, lakini kuna vyombo vya habari ambavyo vinaonekana kuwa na lengo fulani katika suala hilo

  Jumanne wiki hii katibu mkuu wa NCCR mageuzi bw Sam Ruhuza alizomewa wakati akiwahutubia wakazi wa kasulu, baada ya kuanza kuzungumia suala la kufukuzwa kwa kafulila.

  Tukio hilo lillitokea Jumanne Juioni mjini Kasulu lakini halikupata "Covarege" katika vyombo vilivyozoeleka vya habari hususan Magazeti hadi siku tatu baadaye ambapo issue hiyo imeibuka "kwa nguvu"

  Magazeti ya mwananchi na Nipashe ya leo yameandika habari hiyo na kuipa uzito, lakini kinachotia hofu ni aina ya uandishi uliofanyika katika habari hiyo

  ukichunguza habari hiyo utaona kuwa kama imeandikwa na mwandishi mmoja na baadaye kuisambaza katika magazeti hayo ikiwa imefanyiwa mabadiliko machache.

  Najiuliza iwaje habari hii itokee siku tatu nyuma haikupata "mvuto" na baadaye iibuke na kupewa uzito huo? je si sawa na yaliyokuwa yakifanyika wakati wa kampeni za mwaka 2005?

  hili naliona mimi tu au na wengine pia wanaona kw ajicho kama langu?
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  umaarufu wa kafulila hauwezi kumalizwa na vyombo vya habari.nccr ina wbunge kigoma pekee.hata isipoandikwa kwenye media ruhuza amejionea kwa macho yake jinsi alivyokuwa bogas
   
Loading...