Shigongo ni kada Wa CCM Wa muda mrefu sana, hata mwaka 2010 alikuwa ni miongoni mwa wanaCCM waliomba kugombea ubunge katika jumbo Fulani mkoani Mwanza, bahati mbaya alishindwa kwenye kura za maoni. Sijui kama mwaka huu kama hakugombea na kushindwa.
Kwa sasa Shigongo ni miongoni mwa team ya wanaCCM ya propaganda kwa kutumia vyombo vya habari wanavyovimiliki. Wengine ni Antony Diallo(Star TV, Free Africa, Kiss FM), General Ulimwengu(RAIA kwema na RAIA Tanzania), Ruge Mutahaba/Joseph Kusaga(Clauds FM,Coconut FM, Clauds TV), Msama(Dira Tanzania) nk.
Kwa sasa hali ya kisiasa ni mbaya sana kwa CCM hivyo kila chombo cha habari ambacho wanaweza kukitumia kufanya propaganda zao chafu watakitumia, ndio maana hata vyombo vya umma kama TBC, habari Leo, Daily News na Sunday News vimekuwa ndio vyombo rasmi vya kufanyia kampeni za CCM. Hawana jinsi tena, hali yao kisiasa ni mbaya sana na inazidi kuwa mbaya kila siku kuelekea siku ya uchaguzi.