Magazeti ya Leo na Tamko la UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya Leo na Tamko la UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Jan 21, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wana JF, hivi magazeti kazi yake ni kuchukua kila wanachoambiwa na kuona na kukiweka kwenye magazeti yao bila kukifanyia tathmini na kuona mantiki yake na kujua ni jinsi gani watakitoa kwa watu ili kilete maana iliyokusudiwa? Naomba anayejua uandishi anihabarishe.

  Leo magazeti karibia yote yameonyesha kama tamko la UVCCM ni la kishujaa sana na kwamba vijana wa CCM wamekikoromea chama na wamechoshwa na hali ya mambo inavyokwenda.

  Kwa maoni yangu nimeona tamko lile kama lilikuwa na lengo la kusafisha watu wengine na kuwabana wengine. Kwa nini wanataka issue ya Dowans irudi Bubgeni? Ninadhani wanataka kumsafisha EL na kutaka akina Mwakyembe na Sitta na ile kamati ya Mwakyembe wawajibishwe kwa kuliiingizia taifa hasara, wanataka watuaminishe kwamba akina Mwakyembe ndio walikosea.

  Lakini pia kwa moto wa kisiasa ulivyo nchini wasingeweza kuunga mkono Dowans kulipwa hata wangekuwa wajinga kiasi gani, kwa kuwa wanajua kila mtanzania anataka Dowans wasilipwe.

  Kuhusu mikopo, hii wamechomekea ili waungwe mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa wanajua hawa wanafunzi wana influence kwenye jamii.

  Mengine waliyoyasema ndio yanatia kichefuchefu kabisa (Kumshambulia Dr Slaa).

  Sitaki waandishi wa habari wawe na mawazo (tathmini) kama yangu lakini kwa kweli hili tamko sioni kama linastahili kuonyeshwa kwamba ni la kishujaa mbele ya jamii, kama magazeti mengi yalivyofanya (almost yote), bali limejaa unafiki, uzandiki, uzabizabina na kujipendekeza kwa hali ya juu. Ningekuwa mhariri, habari hii nisingeiweka front page.

  Hayo ni maoni yangu, asante sana wewe uliyeyasoma na karibu kwa maoni yako.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hivi Tanzania kuna Wahariri gani au Waandishi gani wa habari kama wapo labda mmoja tu ambaye anajua kutumia taaluma yake vizuri wengine ni njaa ndizo zawasumbua
   
 3. 7

  7ceven Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wametumwa ba babu na baba zao wapime upepo hao!!!! Hawaachi kutapatapa. Poor thing
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Magazeti ya Tanzania yaliyo mengi ni famba i mean wanachakachua ili kukidhi matakwa fulani.
  Msitegemee kupata fikra chambuzi kuhusu tamko la UVCCM zaidi ya sifa na povu jiiingi ambalo jua likiwaka linapotea looote.
  Count me mwezi tu mtaona hali halisi
   
Loading...