Magazeti 473 yafutiwa Usajili


A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,732
Likes
2,290
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,732 2,290 280
720_500_988da7b57ca45ee81a8be7bf3c976a83.JPG

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na vyombo kuhusu kufutwa kwa usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo leo jijini
Dar es Salaam.

Kulia ni kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari.

==================

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akionesha kwa waandishi wa habari tangazo la serikali Na. 65 linaloonesha kusudio la kufuta viapo vya usajili wa magazeti ambayo hayajachapishwa kwa muda wa miaka mitatu kwa mujibu wa sheria ya magazeti leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Flora Mwenyembegu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na vyombo kuhusu kufutwa kwa usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Bibi.

Zamaradi Kawawa na Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Flora Mwenyembegu.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 kupitia tangazo lake lililochapishwa katika Gazeti la Serikali lenye namba 195, (Supplement No. 23) la tarehe 10/06/2016 kutokana na Magazeti hayo kutochapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam.Mhe. Nnauye alifafanua kuwa kutokana na kufutwa kwa viapo vya usajili wa magazeti hayo, mtu yeyote atakayechapisha au kusambaza magazeti yaliyotajwa katika tangazo hilo kwa njia ya nakala ngumu au kieletroniki atakuwa anakiuka sheria ya magazeti sura ya 229 kifungu cha 6 na hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Iwapo kuna mmiliki wa gazeti ambaye angependa kuendelea na biashara hii baada ya kufutwa magazeti hayo, milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo” alisisitiza Mhe. Nnauye.

Akifafanua Mhe. Nnauye amesema kuwa wamiliki wa magazeti 473 yakiwemo Alasiri, Pambamoto, Mipasho, Mirindimo, na Taifa Tanzania ambao viapo vyao vimefutwa, wahakikishe kwamba hawavunji sheria kwa kuanza biashara hii ya magazeti bila kufuata taratibu za kujisajili upya na endapo watakiuka maelekezo hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa mujibu wa kifungu cha 23 (1), Waziri mwenye dhamana ya kusimamia sekta ya Habari amepewa mamlaka ya kufuta hati za viapo zilizoandikishwa na gazeti ambalo halikutolewa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo baada ya kutangaza kusudio la kuyafuta magazeti husika kupitia Gazeti la Serikali.

Wizara imefanya mapitio ya viapo vya usajili wa magazeti yote na Ofisi ya Waziri mwenye dhamana ya Habari imejiridhisha kuwa kuna idadi ya magazeti 473 ambayo yamesajiliwa lakini hayajachapishwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Kufuatia hali hiyo, tangazo la serikali Na. 65 la tarehe 22 Machi, 2013 lilitolewa kwa ajili ya kutangaza kusudio la kufuta viapo vya usajili wa magazeti 550 na kupewa fursa ya kujitetea au kuonyesha nia ya kuendelea kuchapisha.

Baada ya tangazo hilo magazeti 77 yalionyesha nia yakuendelea kuchapisha,kwa mantiki hiyo hadi sasa kufuatia orodha ya wakati huo pamoja na kupewa muda mrefu zaidi ya unaotakiwa kuna magazeti 473 ambayo hayachapishwi na yamekosa sifa ya kuendelea kutambulika na msajili wa magazeti kwa mujibu wa sheria.

Aidha Mhe.Nnauye ametoa pongezi kwa wamiliki wa vyombo vya habari ambao wamekuwa wakifuata sheria na taratibu zinazosimamia tasnia ya habari ili kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwani Serikali inathamini sana mchango wa huduma ya vyombo hivyo.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Msajili wa Magazeti iliyopo chini ya Idara ya Habari (MAELEZO), Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria. Hata hivyo licha ya magazeti na majarida kusajiliwa yapo baadhi yameshidwa kuchapishwa na wamiliki mara baada ya kusajiliwa na mengine yalichapishwa kwa muda mfupi na kuacha kabisa uchapishaji.


Chanzo: Michuzi
 
U

uungwana vitendo

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2013
Messages
1,164
Likes
266
Points
180
U

uungwana vitendo

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2013
1,164 266 180
hakuyataja????
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,805
Likes
64,826
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,805 64,826 280
Kama yalikuwa hayachapishwa kwa muda wote huo wa miaka 3 basi ni haki yao.Kwa kifupi wamempa Nape pa kutokea
 
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
8,435
Likes
5,374
Points
280
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
8,435 5,374 280
Magazeti ambayo hayajachapishwa miaka mitatu mfululizo haiwezi kuyapa Uhuru kick
 
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
6,467
Likes
3,100
Points
280
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
6,467 3,100 280
Sioni tatizo hapo kama magazeti yenyewe yalishajifungia kwa miaka mitatu na hayalipi kodi!
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,755
Likes
49,642
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,755 49,642 280
Amefungia Magazeti ambayo hayajachapishwa kwa miaka mitatu, labda itakuwa motomoto, mfanyakazi n.k.
 
I

IkuluKwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
539
Likes
389
Points
80
I

IkuluKwetu

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2016
539 389 80
Amefungia Magazeti ambayo hayajachapishwa kwa miaka mitatu, labda itakuwa motomoto, mfanyakazi n.k.
Hayajafungiwa, yamefutwa kutoka kwenye orodha ya magazeti nchini which means ukitaka kuirejesha sokoni una-apply upya usajili. Magazeti kama HEKO!
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,755
Likes
49,642
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,755 49,642 280
Hayajafungiwa, yamefutwa kutoka kwenye orodha ya magazeti nchini which means ukitaka kuirejesha sokoni una-apply upya usajili. Magazeti kama HEKO!
Soma vizuri kichwa cha habari mkuu
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,755
Likes
49,642
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,755 49,642 280
Hayajafungiwa, yamefutwa kutoka kwenye orodha ya magazeti nchini which means ukitaka kuirejesha sokoni una-apply upya usajili. Magazeti kama HEKO!
Nimeelewa mkuu ni maongezi tu
 
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Messages
4,438
Likes
591
Points
280
mizambwa

mizambwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2008
4,438 591 280
Kama ni miaka mitatu hayapo hewani, ina maana hizo kampuni zilishafungwa. hivyo si kweli kuwa ameyafungia isipokuwa amefuta katika orodha yao ofissini. Kwani endapo kama gazeti la kila siku lisipochapishwa siku tatu lazima watu tuulize sembuse miaka mitatu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,383
Likes
31,625
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,383 31,625 280
Zama za UHURU na MZALENDO zinarudi msisahau VIBONZO vya CHAKUBANGA. kipanya tumeshamchoka
Kuna ule mgazeti mkubwa kama dirisha.. Lilokuwa mzalendo?
 
Mr.Junior

Mr.Junior

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Messages
9,166
Likes
4,796
Points
280
Mr.Junior

Mr.Junior

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2013
9,166 4,796 280
Hayajafungiwa, yamefutwa kutoka kwenye orodha ya magazeti nchini which means ukitaka kuirejesha sokoni una-apply upya usajili. Magazeti kama HEKO!
Hayajafungiwa, yamefutwa kutoka kwenye orodha ya magazeti nchini which means ukitaka kuirejesha sokoni una-apply upya usajili. Magazeti kama HEKO!
Kasheshe.
 
R

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
4,719
Likes
2,099
Points
280
R

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
4,719 2,099 280
wakati wa uchaguzi na usajili kuna magazti mengi yanaibuka na mara nyingi huwa hawafati maadili ya uandishi wa habari
 

Forum statistics

Threads 1,236,764
Members 475,220
Posts 29,267,984