Ushauri wa bure kwa muweka post:-
Nikupe dili la biashara kwa uzoefu wangu wa hapa Zanzibar na Mainland.
Watu lazima tuamke na tuache biashara za kizamani za kusubiri mteja mlango.
Zanzibar kiwastan wa eneo la mraba,ndio inaongoza kwa kuwa na Yard nyingi za magari ndani ya mji,Mjini Magharibi.
Cha kushangaza,hakuna hata yard moja yenye website,zaidi ya watu kusubiri wateja mlango.
97% ya soko la magari Linategemea wateja kutoka Mainland.Na dunia kama kijiji unapo mfeed mtu maelezo ya kutosha kuhusu bidhaa ndio jinsi unavyoweza kumshawishi aweze kuwa na dhamira sahihi ya ununuzi.
Niliwahi kumpa mtu hili wazo tena ni mmiliki wa Yard,lakini jibu lake ni kwamba yeye anauzoefu wa miaka mingi na hayo mambo yamekuja juzi tu ya mitandao.So,haimuathiri kitu.
Lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi Yard hapa Zanzibar haziuzi gari zaidi ya mbili kwa mwezi.Sasa unajiuliza mtu unaweka mamilioni ya pesa halafu unashindwa kufanya juhudi ya kutangaza biashara yako katika hali ya ushindani wa soko la sasa.
Watu wengi wa Bara wanania na hamu kubwa ya kuja kununua magari na bidhaa nyingine huku,lakini wanashindwa na pia wanasita kuja kununua gari huku kwa kukosa information za kutosha.
Nakushauri mleta mada,kama ni dalali basi najua ni ngum kwako,ila kam una Yard basi badilika uwe kisasa zaidi.
Maana najua kwanini picha hujaweka,hii ni kutokana na mazingira ya bisahara zetu hapa unguja hasa kwa dalali.
Tabia ya Biashara za hapa Zanzibar ni kuiga,akianza mmoja basi watu mia watafuata,hembu tubadilike.