Magari ya washawasha kugeuzwa ya Zimamoto

MUGASHA THE HERO

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
327
204

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu washawasha yaweze kutumika kuzima moto.
Kauli hiyo ilitokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliyeuliza ni kwanini Serikali inanunua magari ya washawasha yasiyo na tija ambayo hutumika nyakati za uchaguzi tu badala ya kununua magari ya zimamoto.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema magari ya washawasha bado yana tija kwani Serikali inafanya taratibu ili magari hayo yatumike kuzima moto kwenye majanga na isiwe kwa washawasha pekee na kuwataka wabunge hasa wa upinzani kuondoa fikra za kuyapinga magari ya washawasha kwani sasa itakuwa ni neema kwao badala ya kutumika kwa kudhibiti vurugu pekee.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Serikali ilinunua magari ya washawasha 777 kwa bei ya kati ya Sh150 milioni na Sh400 milioni, hata hivyo taarifa zingine zilisema magari yaliyotumika wakati wa uchaguzi ni 50.
Awali Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliuliza swali la msingi kwamba ni lini Serikali itapeleka huduma ya zimamoto katika mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.
Naibu Waziri Masauni alisema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika halmashauri ya Mji wa Tunduma lina kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Momba katika Mkoa wa Songwe, kinachohudumia wilaya yote ukiwamo mpaka huo.
Alisema kwa sasa kituo hicho kina gari moja ambalo nalo liko kwenye matengenezo mjini Mbeya likiendelea kufanya matengenezo huku askari wakiendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.
Masauni alisema ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya zimamoto katika maeneo ya nchi ikiwamo Tunduma, mpango huo unategemea upatikanaji wa fedha kwa Serikali.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbozi, alimuomba mbunge wa eneo husika avute subira ili waweze kuona namna bora ya kufanya kwani bajeti ya Serikali ni ndogo na vituo vinavyotakiwa kujengwa ni vingi.
 
Kwa kias flan yanaweza saidia shughul za kuzima moto coz yana pressure ambayo ni kubwa lkn gar la zimamoto linatakiwa liwe na vifaa vya maokoz na vifaa vingne kwa ajil ya kaz hyo lkn wao wameona kwakuwa linaweza kurusha maji kwa kutumia hose (mipira ya kupitishia maji) na juu pale ina monitor bs linaweza saidia lkn magari ya zimamoto Ni gharama kubwa gar moja lililo na vifaa vyote c chin ya 1 billion bt serikal inatakiwa kutengeneza mazingira rafk kwa zimamoto Kama upatikanaji wa maji kwan hlo ndo tatizo kubwa nchin pia na mingine folen ni tatzo kwa zimamoto pia wanunue na maboza kwan magar ya zimamoto hayana uwezo wa kubeba maj meng
 
Hii serikali yetu bhana, unapotokea moto unahitaji attention ya haraka, sasa magari ya washa washa yanatembea kama jongoo, halafu yana nozzle moja tu ya kurusha maji tena hayaja tengenezwa kwa malengo ya kuzima moto bali kwa ajili ya kutawanya watu.
Leo unaposema yatazima moto naona kama ni ile ile mizuka. Kama haya magari maalum ya kuzima moto yana mwendo kasi na bado wananchi wana lalamika kuchelewa kufika kwenye tukio je itakuwaje kwa washa washa?
 
Hiyo ndiyo Serikali ya ccm, ina tenda kwanza halafu yanapoanza kutokea malalamiko ndiyo inaanza kuchukua mawazo ya wadau mweeeeeeeee sijui wakoje
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu washawasha yaweze kutumika kuzima moto.
Kauli hiyo ilitokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliyeuliza ni kwanini Serikali inanunua magari ya washawasha yasiyo na tija ambayo hutumika nyakati za uchaguzi tu badala ya kununua magari ya zimamoto.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema magari ya washawasha bado yana tija kwani Serikali inafanya taratibu ili magari hayo yatumike kuzima moto kwenye majanga na isiwe kwa washawasha pekee na kuwataka wabunge hasa wa upinzani kuondoa fikra za kuyapinga magari ya washawasha kwani sasa itakuwa ni neema kwao badala ya kutumika kwa kudhibiti vurugu pekee.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Serikali ilinunua magari ya washawasha 777 kwa bei ya kati ya Sh150 milioni na Sh400 milioni, hata hivyo taarifa zingine zilisema magari yaliyotumika wakati wa uchaguzi ni 50.
Awali Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliuliza swali la msingi kwamba ni lini Serikali itapeleka huduma ya zimamoto katika mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.
Naibu Waziri Masauni alisema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika halmashauri ya Mji wa Tunduma lina kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Momba katika Mkoa wa Songwe, kinachohudumia wilaya yote ukiwamo mpaka huo.
Alisema kwa sasa kituo hicho kina gari moja ambalo nalo liko kwenye matengenezo mjini Mbeya likiendelea kufanya matengenezo huku askari wakiendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.
Masauni alisema ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya zimamoto katika maeneo ya nchi ikiwamo Tunduma, mpango huo unategemea upatikanaji wa fedha kwa Serikali.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbozi, alimuomba mbunge wa eneo husika avute subira ili waweze kuona namna bora ya kufanya kwani bajeti ya Serikali ni ndogo na vituo vinavyotakiwa kujengwa ni vingi.
Me sijaelewa huyo alie kua anajibu nini.Maana.Awawezi kujibu mpaka wataje upinzani.
 
Mambo ya moto mtaendelea kushangaa tu kwasababu mmekumbatia ufisadi wa plastics kila kona mpaka magorofa yenu plastics, viti, magodoro ni plastiki mashule yanaungua mnashangaa moto mkali! Hakuna mchawi, ni ujinga wenu wa kushupalia fire extinguishers katika vigari binafsi badala ya kuzuia majanga kwenye majengo kama mabweni, shule, maofisi viwandani nk. Ni magodoro, mapazia, makochi, makapeti, hata rangi zenu za mafuta zinachangia ukali wa moto kwenye majengo. Halafu mnajivunia TBS na vikaragosi vyenu vya AQRB na zimamoto wasiojua wanachotakiwa kufanya! Msione majuu kuna'gaa; Kumeundwa!
 
Kivipi wakati hayajatengenezwa kwa ajili hiyo.Think twice Mkuu.
Yote mfumo wake ni mmoja yanarusha Maji, unachofanya ni kufunga horse pipe labda kama umesahau kabla ya ujio Wa magari haya tulitumia magari ya fire kuzima vurugu kinachongezwa ni kemikali ya kuwasha.

Tofauti ya haya yametengenezwa kuruka viunzi. na pingamizi za barabarani. Tunasema yarstumika sababu hayataacha kusudio la awali na kwa sababu idara hizi mbili sasa ziko chini ya wizara moja na chini ya mkuu Wa jeshi la polsi no rahisi Ku coordinate
 
Tulipowaambia hapakazi tu hamkuelewa?

Jamani wa ajabu ni watanzania

Kwa sababu huwezi ukawa unadanganywa na watu haohao kila siku kwa uongo huohuo alafu bado unawachagua

nonsense
 
ujinga wa idadi kubwa ya watanzania ndio umetufikisha hapa,yaani kila jambo wanalishangilia bila hata kufikilia kwa mapana
 
Mimi huwa naona magari ya fire yanarusha maji kwa kuyazungusha pande zote tena yakiwa yametawanyika kama mvuke. Sithani kama ule mvuke utaweza kuzima moto.
 
Kwa kias flan yanaweza saidia shughul za kuzima moto coz yana pressure ambayo ni kubwa lkn gar la zimamoto linatakiwa liwe na vifaa vya maokoz na vifaa vingne kwa ajil ya kaz hyo lkn wao wameona kwakuwa linaweza kurusha maji kwa kutumia hose (mipira ya kupitishia maji) na juu pale ina monitor bs linaweza saidia lkn magari ya zimamoto Ni gharama kubwa gar moja lililo na vifaa vyote c chin ya 1 billion bt serikal inatakiwa kutengeneza mazingira rafk kwa zimamoto Kama upatikanaji wa maji kwan hlo ndo tatizo kubwa nchin pia na mingine folen ni tatzo kwa zimamoto pia wanunue na maboza kwan magar ya zimamoto hayana uwezo wa kubeba maj meng
Kwasababu gari la kuzima moto gharama yake ni kubwa so wakaona wanunue haya ya washawasha ili waje wayabadilishe yawe ya kuzima moto.
Uuuuwiii.

Hivi unajua pressure ya maji ya kuzima moto ?
Kama pressure ile ya washasha ingekuwa sawa na pressure ya maji ya kuzima moto basi watu wangekuwa wanakufa sana
 
Kivipi wakati hayajatengenezwa kwa ajili hiyo.Think twice Mkuu.

Kwa kweli hawafikirii mara mbili magari ya zima moto yanatengenezwa mahusi yakiwa na vifaa maalum vya kuzima moto.

Inamaana unavyo geuza gari la washawasha kuwa la zima moto kuna vipuri maalum vitatakiwa viwekwe ikiwa pia ni kubadili muundo wa gari lenyewe ambayo ni gharama kubwa. Je kutumia gharama zaidi kurekebisha haya magari pesa zinatoka wapi kama sio matumizi mengine yasiyo na tija.
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Hizo nyumba na masoko yanayoungua kila siku siwakate bima za moto? Kwanza sijawahi ona nyumba imezimwa moto na hayo magari,
 
Mimi nina mawazo tofauti kidogo.Yafanyiwe modification Chasises ziwekewe bodies za kubeba takataka Daresalaam.Uchaguzi ukikaribia body zake za washawasha zinaweza kurudishwa wahusika wakipenda.Ziwe MULTI-PURPOSE.

Jiji la Daresalaam ni chafu ni chafu hatari,kuna tatizo la utupaji taka hovyo lakini pia kuna tatizo kubwa la uzoaji taka,magari hayatoshi.
 
Back
Top Bottom