Tetesi: Magari ya Toyota kutengenezwa Tanzania

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
423
MAGARI YA TOYOTA KUTENGENEZWA TANZANIA
Kuna tetesi nimeziona kwenye mitandao kuwa Waziri wa Viwanda wa Tanzania amekutana na CEO wa Toyota nchini Japan nakukubaliana na CEO wa Toyota kujenga kiwanda cha magari ya Toyota Tanzania under license.

Uamuzi wakujenga kiwanda cha magari Tanzania ni uwamuzi mbaya kiuchumi ukizingatia aina ya uchumi wetu.Tanzania inawekwa katika nchi maskini zaidi duniani (Least Developed Countries -LDCs). Nchi hizi ni nchi zilizonyuma kiteknolojia na kimaendeleo ya viwanda.

Niliposikia tetesi hizi nilishangaa sana kama kweli bado wataalamu wetu wa uchumi na biashara wanaishauri serikali ipasavyo au huenda hawapewi nafasi yakushauri.Rais wa Tanzania JPM anazungumza mapinduzi ya viwanda jambo ambalo ni nzuri sana.Tulikuwa tunamsubiri kiongozi wa aina hii mwenye muono thabiti wa nini anataka kufanya na kukizungumza bila aibu.

Pamoja na kwamba dhamira ya Rais na Serikali ni njema lakini nilazima tuwe na utulivu wa hali ya juu nakuweka mkakati unaoweza kuleta mapinduzi hayo ya viwanda. Kiuhalisia ni kwamba kipaumbele cha kwanza cha Tanzania kwenye kuendeleza viwanda hakiwezi kuwa kiwanda cha magari.Hayo ni maamuzi ya kupenda sifa bila uhalisia. Kabla yakuanzisha kiwanda fulani kama kweli unataka kichangie kukuza uchumi unaangalia vitu vyamsingi hususani linkages (backward and forward linkages) ambazo kile kiwanda kinaleta kwenye uchumi.Backward linkages inamaanisha uwepo wa viwanda vingine au wawekezaji au mazingira yatakayowezesha kusupply kiwanda kipya na raw materials na inputs nyingine wezeshi.Mfano ukitengeneza kiwanda cha nguo Shinyanga kuna clear linkage kwakuwa utanunua pamba za wasukuma na utaajiri watu wajamii zile kufanya kazi kwenye kiwanda. Vilevile wazalishaji wa chakula watauza vyakula kwa wafanyakazi wa kiwanda na hivyo kupelekea kustumulate uchumi katika eneo lile. Kwenye forward linkage unazungumzia uwepo wa viwanda vingine ambavyo vitafaidika na bidhaa zizalishwazo na kiwanda kipya.

Unapoweka kiwanda cha magari ka kipaumbele cha maendeleo ya viwanda Tanzania mimi sikuelewi.Hatuna wataalamu wa uzalishaji wa magari,ni raw materials gani zakutengeneza magari ambazo zinazalishwa na viwanda vya ndani ambazo zaweza kujustify backward linkage? Angalau kwenye spare za magari naweza kuelewa kidogo.Lakini si linkages peke yake tunazoangalia bali kuna theory za uchumi na biashara za kimataifa zinazo saidia kufanya maamuzi ya uwekezaji kwenye uzalishaji.Kuna Theory ya mchumi maaruufu wa siku nyingi aitwae David Recardo, yeye anazungumzia kitu kinaitwa Comperative Advantage.Huu ni uwezo wa nchi moja kuzalisha bidhaa kwa bei nafuu zaidi kuliko nchi nyingine.Hebu tujiulize kweli kwakuangalia kiwango cha teknolojia, skills,mazingira ya uwekezaji, resource searching techniques n.k ni rahisi zaidi kuzalisha gari Tanzania kuliko Japan? Je kwenye hii aina ya uwekezaji Taifa litafaidika kweli kiuchumi ukilinganisha na uwekezaji kwenye maeneo mengine? Siyokwamba nakataa tanzania isizalishe magari...kimsingi nijambo la heshima nchi kuzalisha magari au hata ndege.Lakini natazama uhalisia na uwezo wetu wakufikiri nakuweka vipaumbele. Hebu nikupe mifano ya baadhi ya maeneo ambayo serikali ingeweza kuweka vipaumbele vya viwanda nakupata tija kubwa zaidi;

i) Viwanda vya vyakula: Kwanini serikali isiwekeze katika viwanda vya vayakula ambavyo Japan inaagiza kutoka nje.Sisi tuzalishe kwa wingi na ubora vyakula,matunda , mboga mboga tuuze Japan.Wao waendelee kutuuzia magari sisi tunawauzia vyakula.Tukikamua matunda yetu ya Mheza i.e maembe,machungwa n.k ambayo wakati wa msimu huoza tukayafanya yakawa juice zenye ubora Japan watanunua.Tukikausha mbogamboga zetu kwa ubora na hata matunda tukawauzia Japan watanunua.Tukiweka ubora nakuongeza thamani vile vitu tunavyozalisha hapo tutakuwa tumeanza kwa ubora,.Viwanda vya bidhaa za vyakula vina linkages nzuri na uchumi na uwekezaji wake si aghali kama magari. Tukiwekeza kwenye viwanda vya chakula tutazuia kuoza kwa mahindi maghalani na tutaweka mikakati yakupoteza mazao baada ya kuvuna (post harvest loss).Hii itasaidia sana kuinua uchumi kwakuwa asilimia 80% ya Watanzania wako kwenye kilimo na si kwenye ufundi wa magari.

ii) Viwanda vya samani za ndani (furniture): Nijambo linalochekesha na kufedhehesha.Ukienda kwenye ofisi nyingi za serikali utakuta furniture zinazotumika zimetoka China.Si tu kwamba zimetoka China bali ukizichunguza utaona zimetengenezwa kwa vumbi la mabao na si mbao halisi.Kituko nikwamba Tanzania tunavuna magogo kule Njombe,Iringa,Makambako n.k tunauza magogo mazima mazima China na nchi zingine kwa bei yakutupa.Wachina wanachana magogo yetu wanatengeneza furniture bora sana wanauza Marekani na Ulaya kisha zile vumbi za mbao wana zi press wanatutengenezea meza ya ofisini ambayo hata kwenye mawizara zinatumika..naam...yamkini hata wizara inayosimamia viwanda wanatumia meza ya vumbi za mbao. Furniture hizi zinanunuliwa kwa bei ya ghali sana na serikali lakini ni mavumbi ya magogo yetu ya Tanzania.

Kwa mawazo yangu hapa ndipo tungeanzia.Haiwezekani Waziri akasirishwe na yeye kutumia gari kutoka Japan wakati anatumia meza ya vumbi la mbao za Tanzania kutoka China. Ningeshauri serikali idhibiri uuzaji wa magogo nje ya nchi na ihamasishe utengenezaji wa samani (furniture) za kiwango cha dunia.Hata kama italazimika kuleta wataalamu waviwanda vya mbao kwakuanzia kutusaidia kufundisha ubora katika bidhaaa za mbao.Kwa aina hii ya viwanda tunaweza kuuza furniture dunia nzima na wakulima wa miti wakapata pesa nzuri zaidi na sekta ya kilimo cha miti ikanufaika.Lakini pia tutahamasisha viwanda vidogovidogo vya samani za mbao ambavyo vitapata materials kutoka kwenye hivi viwanda vikubwa.Hatuhitaji kutumia kwanza gari linalotengenezwa Tanzania, tunataka kwanza tukalie kiti kinachotengenezwa Tanzania. Hapo ndipo pakuanzia.

iii) Viwanda vya nguo: Nilisikia hivi karibuni marais wa Africa mashariki wamekubaliana kusimamisha uagizaji wa nguo za mtumba kutoka nje.Wanataka kuzalisha nguo kwa ajili ya watu wao.Hapo ndipo pakuanzia. Hebu tuweke viwanda vya nguo na kutumia pamba yetu kutengeneza nguo nakuuza nchini na nje ya nchi.Hebu tutengeneze viwanda vya bidhaa za ngozi kama viatu,mikanda na kadhalika tuokoe ngozi zinazo oza mitaani.Tukikuza sector ya ngozi hata wafugaji watafaidika.Nijambo la aibu tunauza pamba nje kwa bei ya kutupwa wazungu wananunua wanatengeneza nguo wanazivaa kisha wanazitupa wanazikusanya tena wanatuletea kama mitumba tunanunua kwa bei ya juu kuliko tuliyo uzia pamba.Hapa tunahitaji tu kufikiri vizuri.tayari kuna dhamira ya kisiasa kutoka kwa Rais wetu.Tumsaidie bila uoga na kumshauri vizuri.Tusiwe watu wa ndiyo mzee.Kama wataalam tunawajibika kwa nchi yetu.

iv) Bidhaa za vyakula zitokanazo na mifugo: hapa Tanzania siku hizi hasa kwenye miji mikubwa kumekuwa na restaurant za kisasa kama KFC, Marry Brown n.k tunakula sana kuku pale.Hawa kuku hawazalishwi Tanzania. Supermarket tunanunua nyama ziko packed hazizalishwi Tanzania.Tunakunywa maziwa ya box hayazalishwi Tanzania.Hivi tuna shida gani hasa.Sisi ni kati ya nchi yenye ng'ombe wengi sana.kwanini tunywe maziwa ya Newzealand? Serikali iweke mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye viwanda hivi na ufugaji wa kisasa habari yakula makuku ya South Africa tuachane nayo.Sasa kiwanda cha gari chanini wakati mama kule kijijini anauwezo wakufuga ng'ombe wa maziwa na kuku na tukimhakikishia soko na viwanda vipo atazalisha sana na ataweza kupeleka watoto shule.Ni lini kiwanda cha magari kitampatia mama kama huyu hela yakumpeleka mtoto shule? naamini bado hatujawaza vizuri.

Wakati mwingine tunatafuta utatuzi wa matatizo yetu kwa jirani kumbe jibu limo ndani ya nyumba.Wakati mwingine tunaangalia mambo ya mbali sana wakati masuala ya msingi yamo ndani ya nchi.Historia ya mapinduzi ya viwanda inaonyesha nchi zilianza na viwanda vya msingi kabla yakwenda kwenye high-tech industries. Nchi yetu ni labor intensive na tuna hitaji kufanya uwekezaji wa viwanda vyenye kuhitaji watu wengi kwenye uzalishaji.Namaanisha ile Value Chain ya bidhaa imeshirikisha watu wengi. Tunaweza kufanya jambo sahihi kwa namna isiyo sahihi na tukapata majibu yasiyo sahihi. Lazima tutafakari namna yenye tija zaidi kabla hatujafanya jambo.

Masoko ya bidhaa za viwanda nilivyopendekeza yanatoka wapi?

Aina ya bidhaa nilizopendekeza ndizo zinazohitajika zaidi na soko la Africa.Hata bila kuuza nje ya Africa tayari tunaweza tukaliwekea mkakati soko la Africa kama nchi na tukaendelea kwa kasi sana.Kwa sasa Africa inaelekea kuwa soko moja.Tanzania ni mwanachama wa East Africa Community (EAC) na jumuhia hii iko kwenye kiwango cha Soko la Pamoja yaani Common Market.Soko la pamoja linatoa fursa nyingi na uhuru wa watu,bidhaa,huduma na mitaji. Soko la EAC kwasasa lina nchi 6 na zaidi ya watu millioni 150.Tanzania ni mwanachama wa Sounthern Africa Development Communityu (SADC) soko lenye nchi 15 na watu zaidi ya million 250.SADC iko kwenye level ya Free Trade Area ambayo inatuwezesha kuuza bidhaa zetu kwa nchi zote mwanachama bila ushuru. Mwaka 2015 July marais wa nchi za Africa 26 walitengeneza muungano mwingine wa kiuchumi unaoitwa The Grand Tripartite Free Trade Area ambayo ni muunganiko wa jumuhia tatu za kiuchumi COMESA-EAC na SADC.Muunganiko huu unatengeneza soko la watu zaidi ya million 600. Hili ni soko kubwa sana ambalo Tanzania tukiwekeza kwenye viwanda nilivyovitaja hatuwezi kulimaliza hili soko.Consumer behavior au tabia ya walaji wa Africa inafanana kwa kiasi kikubwa.

Africa inafanya biashara ya ndani kwa asilimia 10 peke yake na asilimia 90 ya bidhaa na huduma zinauzwa nje ya bara letu.Hata hivyo Africa inachangia chini ya silimia 3 ya biashara yote ya dunia.Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kuna fursa kubwa ya kukuza soko la ndani ya Africa na Tanzania kwa aina ya raslimali tulizo nazo tunaweza kulifaidi soko la Africa tukiwekeza vizuri kwenye viwanda sahihi.Hebu tuachane na habari za magari,gas,mafuta na madini kwa muda.Watu wengi wanafurahi sana kusikia ugunduzi wa mafuta,gas na madini wanafikiri Tanzania itakuwa tajiri kwa aina hizo za uwekezaji.Mimi ugunduzi tu haunifurahishi bila mikakati thabiti.Hebu jiulize toka kugunduliwa kwa migodi ya dhahabu,almasi,tanzanite n.k Tanzania imekuwa tajiri? sekta hizo zinachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa? jiulize na ujijibu.Hilo la mafuta,gas na madini ni mada ya siku ingine leo nilitaka tu nizungumzie suala la kiwanda cha magari Tanzania.

Nasisitiza Tanzania kwa sasa haiitaji kiwanda cha magari.Hicho si kipaumbele chetu kwa aina ya uchumi wetu.

Kama kuna jipu kubwa zaidi linalohitaji kutumbuliwa basi ni jipu la namna tunavyo fikiri na kuweka vipaumbele vyetu.

Flash back literature 29/05/2016
Imeandaliwa na: Elibariki Shammy
Elibariki ni mtaalam,mchambuzi na mshauri wa biashara za kimataifa
Anapatikana kwa
Simu: +255767477205
E-mail: bkshammy@yahoo.com
 
una hoja lakini tambua nafasi ya sekta binafsi katika uchumi.
wafanyakazi wa viwanda watatumia vyakula tunavyozalisha, ajira kwa vijana katika nafasi zisizoza kitaalam, kodi, umeme na maji hawawezi kutoa japan.

gharama za ununuzi wa gari kwa watanzania itapungua kwa kuondoa gharama za usafirishaji na tutauza magari nje kimsingi tutapata fedha za kigeni.


ujenzi wa kiwanda cha magari una multiplier effect kwenye uchumi.!
 
Nafikiri wewe unaogopa kwamba gari ni kitu kikubwa sana la hasha! hiyo ilikuwa zamani, Siku hizi gari ni kitu kidogo cha kawaida mno na tena uwekezaji katika kiwanda cha magari ni sahihi kabisa kwa sasa Tanzania na uchumi wetu utakuwa sana. Vipi kama tunawekeza kwenye pikipiki au kiwanda cha baiskeli bado una shida? Inua akili yako juu tunaweza hata kuwekeza kwenye mitambo ya nyuklia na tumeanza kuichimba sasa. Kuwa tayari kwenda kwa mwendo kasi yaonekana upo conservative sana.
 
Nilitamani sana fatilia hoja zako lakini ulipoanza sema ni uamuzi mbaya kusema kweli sijasoma mengine!..
Unaposema ni uamuzi mbaya then waende china mtasema hatuna sera nzuri investors wanatukimbia, whatever the cost lets try to leapfrog technologically..
Acha tupate gari zetu mpya straight from the industry labda itatupunguzia mizigo used barabarani!.

Toyota acha wajenge kwa hela zao mradi hazitoki mfukoni kwa serikali (usiwapangie).
 
Mkuu uko vizuri lakini mtizamo wako ulifaa miaka 30 iliyopita,
Kiwanda cha gari ni sahihi Kwa sasa Tz kwani kuna mchchuma huko Ludewa (kama sijakosea) ni mgodi wa chuma utaajiri watu na 60% watakuwa wa Tanzania chuma kitabaki nchini na sio kwenda Japan na ukumbuke wafanyaka wote hao ndio watakuwa chachu kwa uanzishwaji wa viwanda vingine, gari nyingi sana zinaingia kupitia bandari ya dar es salaam kwenda nchi za Congo ,zambia, Malawi n.k wote hawa wataacha fedha za kigeni hapa nchin
 
Sijasoma m bango wote huo, kichwa cha habari chajitosheleza kwa kifupi hakuna kiwanda cha magari kitakachotufaa. Mostly watanzania hatuna uwezo wa kununua gari jipya, sisi tunaweza kununua used tu. Scania walikuwa wana assemble pale Tamco Kibaha, pamoja na tractor za Valmet, ila kutokana na bei wakafunga kiwanda, matajiri wengi wa maroli wananunua used rollies.
ni afadhali waje wahindi au wachina angalau tunaweza kununua magari yao ya Tata au Jiefang, angalau bei zake ni affordable.
Lakini Toyota Mh, itanunua serikali na wakina Bahresa...
 
Magari yakitengenezewa hapa yatakuwa cheap sana ukienda Japan magari mapya ni cheap lakini tatizo ni kodi na kusafirisha mpaka hapa Tz
Weka link tujionee hiyo cheap
 
Hoja ya viwanda ikilalia upande wa kuangalia tu raw materials zinazozalishwa nchini tutapoteza lengo au tutashindwa kufanikiwa.

Hata kama viwanda haviwi soko la raw materials kwa nchi ila vinaweza kuwa chachu ya kuongezeka nguvu kazi na pia :

1. Kuongeza our forex reserves au even kuongeza thamani ya shilingi yetu if properly managed
2. Kupunguza BOP deficit
3. Kupandisha GDP ya nchi
4. Kuwa stimulant wa viendesha uchumi vingine au sectors zingine.
5. Tax revenue if well managed pia
 
Umekalili rudi ukasome Tena faida za kiwanda chochote kile tambua kua kiwanda hicho kupitia uzalishaji wake pamoja na magar yatakayouzwa ndan na nje ya nchi itawezesha serikali kulipa kod (2) magari mengi yatauzwa nje ya nchi hii itaongeza exportation na kupelekea balance of terms of trade (3) kitatoa ajira hata km ni kwa vibarua lkn ajira hizi zitapelekea transfer of technology ambapo vijana watakao kua wamepata ajira watacopy technology (4) hiyo forward na backwards linkage ipo kwan tz hatuna viwanda vya chuma, je magari yatakayotengenezwa na kiwanda hicho hayawezi kuuzwa kwenye viwanda vingine ACHA KUKALILI NDUGU RUDI SHULE UONGEZE UPEO WA KUFIKIRI
 
Mtoa mada aliyoyasema ni kweli, kiwanda cha magari ya Toyota si katika vipao mbele kwa nchi yetu, kwani asilimia kubwa ya watanzania hawawezi kumudu kununua gari jipya, wengi wetu tunanunua magari yaliyotumika, na ukizingatia kipindi hiki kigumu ambacho wengi wanalalamika pesa imepotea, na wengi wetu mishahara haituruhusu kumudu kununua zero km car.
Kwa sasa tunaweza kufurahia tumeanzisha viwanda vingi, lakini vitaweza kuendelea? Watu wanalalamika hawana pesa sasa hizo bidhaa zinazotengenezwa na hivi viwanda nani atanunua? Bora tuanzishe viwanda vyenye kukidhi mahitaji yetu kutokana na hali yetu ya uchumi na kidogo kidogo tujisogeze kwenye viwanda vikubwa, kwani si kila kiwanda kinafaa nchini kwetu, tuangalie nchi zilizokurupuka katika viwanda sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi tu na kubwa zaidi ni air pollution & environmental pollution. Naomba mkuu wa nchi na serikali yake ihakikishe Tanzania ya viwanda ni viwanda vyenye kuleta manufaa kwa jamii ya watanzania katika chakula, mavazi, malazi, afya na elimu, tukiweza kujitosheleza hapo huko kwengine tutafika bila ya tabu. Kama kutakuwa na kiwanda cha kutengeneza matrekta yatakoyoweza kuwasaidia wakulima ya bei nafuu bora kwani yatawasaidia wakulima wengi ambao bado wanatumia jembe la mkono kwa kilimo.
 
Back
Top Bottom