Magari ya Tanzania yamekamatwa na Serikali ya DRC CONGO

Nyalutubwi

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
573
172
Taarifa kutoka kwa Madereva wa Tanzania wanaorudi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinaeleza kuwa Kuna malori mawili ya Kampuni ya Primefuels Tanzania yanashikiliwa na Serikali ya Jimbo la Kivu kusini katika mji wa BUKAVU kwa sababu na makosa ambayo hayajaeleweka.

Madereva hao wanasema kuanzia juzi maofisa hao walifika na kuamuru madereva hao washuke kwenye Magari yao bila kuwaeleza sababu na baadaye Milango ya Magari ikafungwa na kuwaacha madereva hao wasijue la kufanya.

Wenye taarifa zaidi kuhusu suala hilo tunaomba mzitoe ili tuwaokoe ndugu zetu huko Congo.
 
Matukio ya namna hii yamekuwa yakikithiri sana huko Congo.., sijui wanachotaka ni nini!
 
Back
Top Bottom