magari mapya 30 ya tume ya katiba mpya

Eh nilidhani ni magari ya kubebea wagonywa kumbe ni yakatiba mpya na mchakato ukiisha nani atayachukuwa
 
Ilibidi wanunue gubasi, liwabebe basi. Hayo mengine anasa.
 
mie sioni tatizo, wewe ulitaka wazunguke nchi nzima kwa miguu au?

Hakuna ambaye angependa wapate tabu maana tunatarajia kazi nzuri toka kwao kwa ajili ya Tanzania mpya. Ila kama kweli wamenunuliwa magari mapya kuna maswali ya kujiuliza je, huko serikalini hakuna magari mazuri ambayo yangeweza kutumika? au ofisi za wilaya au mikoa hakuna magari ambayo yangeweza kusaidia hawa wateule kufanya kazi katika mkoa husika? Kama yapo tungeweza kuokoa fedha nyingi maana hapo unazungumzia kwa wastani mil 120 x 30.
 
Nimefungua haraka haraka nikadhani ni magari ya kubebea wagonjwa kumbe ni ya katiba by the way huo mchakato ukiisha ayo magari yatakwenda wapi
 
Hakuna ambaye angependa wapate tabu maana tunatarajia kazi nzuri toka kwao kwa ajili ya Tanzania mpya. Ila kama kweli wamenunuliwa magari mapya kuna maswali ya kujiuliza je, huko serikalini hakuna magari mazuri ambayo yangeweza kutumika? au ofisi za wilaya au mikoa hakuna magari ambayo yangeweza kusaidia hawa wateule kufanya kazi katika mkoa husika? Kama yapo tungeweza kuokoa fedha nyingi maana hapo unazungumzia kwa wastani mil 120 x 30.

JF
Tusiweke punda nyuma ya Mzigo hautaondoka! Kwanza hawajatengeneza kanuni, tume haina Hadidu za rejea. Hata ukamilifu wake bado lakini LUkuvi anakimbilia kuagiza Magari. Kwa ujinga wangu nashauri tune itumie public transport, Usafiri wa kawaida ili waweze kuchukua mawazo ya watu hata kwenye mijadala ndani ya daladala.

Tatizo ni kwamba kuna wajumbe wa tume ambao hata kutembea ni tabu. Huu utamaduni wa kununua Magari uko kwenye damu ya Watanzania . Look at the huge number of DFP vehicles on the road.
Pesa nyingi zinatumika kwenye Magari rejea taarifa ya CAG. Magari yanakula sehemu kubwa sana ya pato la Watz right from the family level. This is the problem.

Tungeimarsha mfumo wa Usafiri wa Reli, anga na hata mabasi hakuna haja ya Kila mtu/ mradi kununua gari. Tutoke hapo!
Charity begins at home siku moja toka nje uaangalie ukubwa wa msafara Rais Kiwete unakuwa msururu Magari yasiyopungua thelathini. Hayo Magari wanatakiwa Kila mjumbe na gari lake this is more than crazy!
 
mmesahau kila mjumbe na gari lake,dereva wake na full tank muda wote! Eti jana lukuvi ndo analalamika kwamba kuna matumizi mabaya kwenye mafuta ya mabosi,walikuwa wapi? Madereva wa serikali wamegeuza magari ya umma kuwa ya kutanulia wao na vimke vyao ambavyo havijasoma hata shule! Tena omba bosi asiwe mpenda starehe,dereva anaguka yeye ndo bosi. Gari linapakiwa bar mpaka saa kumi za usiku.
 
Kila la kheri wakafanye kitu ambacho tutasahau kabisa cost tulizo tumia.
 
Inatia wasiwasi kwani hiyotume iliyochaguliwa ina wajumbe wangapi??je gari moja linabeba watuwangapi??kwanini yawe 30??Naombeni mwenye ufahamu juu ya haya maswali anijuze.
 
Tatizo letu watanzania tumezoea kulalamika. Sasa mnaopinga mnataka hilo zoezi lifanyike vip? Watumie Daladala?? Wajumbe wa hiyo tume kwenye mazingira ya kawaida ya kazi zao za sasa hawatumii dala dala, leo uje uwapandishe dala dala, utategemea nini? Mi naona mnawaona hao wajumbe kama wanafunzi au watu wasio na mbele wala nyuma bila kuandalia hadhi zao mmoja mmoja ndio maana mnadiriki kuwaambia wapande dala dala.

Chamsingi hapa naona tungejadili ni aina gari za magari yamenunuliwa na hiyo Fund imetoka wapi. Saa nyingine unaweza kukuta ni hela za donnors.
 
JF
Tusiweke punda nyuma ya Mzigo hautaondoka! Kwanza hawajatengeneza kanuni, tume haina Hadidu za rejea. Hata ukamilifu wake bado lakini LUkuvi anakimbilia kuagiza Magari. Kwa ujinga wangu nashauri tune itumie public transport, Usafiri wa kawaida ili waweze kuchukua mawazo ya watu hata kwenye mijadala ndani ya daladala.

Tatizo ni kwamba kuna wajumbe wa tume ambao hata kutembea ni tabu. Huu utamaduni wa kununua Magari uko kwenye damu ya Watanzania . Look at the huge number of DFP vehicles on the road.
Pesa nyingi zinatumika kwenye Magari rejea taarifa ya CAG. Magari yanakula sehemu kubwa sana ya pato la Watz right from the family level. This is the problem.

Tungeimarsha mfumo wa Usafiri wa Reli, anga na hata mabasi hakuna haja ya Kila mtu/ mradi kununua gari. Tutoke hapo!
Charity begins at home siku moja toka nje uaangalie ukubwa wa msafara Rais Kiwete unakuwa msururu Magari yasiyopungua thelathini. Hayo Magari wanatakiwa Kila mjumbe na gari lake this is more than crazy!

Mkuu Asante kwa mawazo yako mazuri,tatizo liliopo uzalendo ulishapeperuka siku nyingi(haupo tena).Mfano hivi unafikiri huyu Lukuvi alifikiri kabla ya kutenda?Nini kilimsukuma aagize magari hayo?inawezekana kabisa hawa viongozi wetu wamezoea u'boss.Hali ndivyo ilivyo Tanzania kila iitwapo Leo fedha zetu walipa kodi zinateketezwa na wakati huo huo mkuu wa nchi anaenda kutembeza bakuli nje.
 
Magari mapya 30 + Mishahara minono. Halafu katiba yenyewe ikipelekwa zenji inachanwa vipande vipande mbele ya macho yao!.
 
Basi liwabebe waandamane kama kumbikumbi? likiwapata ajali wote kwisha!!

ahadi yao tu itakua imetimia,,,wote wanaopata ajali kwenye gari/basi moja huwa wanakufa????refer ajali ya Selasini juzi,rejea ajali za mabasi,ndege na meli
 
Back
Top Bottom