Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali mpya nchini Ghana inayatafuta magari 200 yaliyokuwa yakitumiwa na afisi ya rais ambayo yanadaiwa kutoweka, msemaji wa rais amesema.
Chama tawala kilihesabu magari hayo mwezi mmoja kabla ya kuingia madarakani baada ya kupata ushindi uchaguzini mwezi Desemba.
Imekuwa kawaida kwa baadhi ya maafisa wa serikali inayoondoka kutorejesha magari ya serikali, na hulazimu serikali mpya kuyatwaa kwa nguvu nchini Ghama.
Waziri mmoja katika serikali iliyoondoka ya John Mahama hata hivyo amesema kuenezwa kwa habari kwamba wenzake walitekeleza uhalifu ni makosa.
Aliyekuwa waziri wa usalama Omane Boamah ameambia mwandishi wa BBC Thomas Naadi kwamba hiyo ni "mbinu inayotumiwa na serikali mpya kuipa sababu za kununua magari mapya."
Msemaji wa rais Eugene Arhin aliambia wanahabari kwamba maafisa wa serikali mpya walipata magari:
- 74 kati ya196 aina ya Toyota Land Cruiser
- 20 kati ya 73 aina ya Toyota Land Cruiser Prado
- 11 kati ya 24 aina ya Mercedes
- Mawili kati ya 28 aina ya Toyota Avalon
- Mawili kati ya sita aina ya BMW.
Alipokuwa anatoa taarifa yake, Bw Arhin alifichua kwamba afisi ya rais ilifaa kuwa na magari zaidi ya 300 lakini hakueleza magari hayo hutumiwa vipi.
Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic Party alishinda uchaguzi mkuu mwanzoni mwa Desemba na kuchukua hatamu kutoka kwa John Mahama, wa chama cha National Democratic Congress.
Chanzo: BBC/Swahili