Magalasha ya CHADEMA

Magalasha ya CHADEMA

mkuu hoja zako zidi ya hiki chama zinasomeka wazi
wewe ni wale watu wa kutafuta makosa zaidi, hilo sio tatizo
lakini una mwamko wa kuponda na kubomoa na sio kujenga.

kuna wabunge hapo umesema hawatarudi na wengine wamechaguliwa kwa
sababu ni waimbaji .
sasa kama wananchi wa mbeya wamependa kuwa na mwakilishi muimbaji kwa nini leo wewe una waita magalasha?

wewe mbunge wako wa jimbo yuko kundi gani?
mkuu kwa sasa unaeleweka wewe ni mkatisha tamaa rudia post zako za hivi karibuni
ni kama vipi MS kazamia account yako

Mbunge wangu ni zaidi ya galasha,ni zuzu maana watu walipo
uliwa mgodini nyamongo yeye alienda na magamba yake kule,..
kilicho endelea toka siku hiyo ni aibu tupu
 
Kwa evaluation yangu hadi sasa,wabunge wafuatao
hawafanani na chadema kabisa,msaada wao kwa chadema ni sifuri

1.Rose Kamili
alihamia chadema baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni
ccm,toka aingie bungeni amekua kimya kweli tofauti na nilivo kua nikimsikia enzi zile
akiwa diwani wa ccm,...alikua machachari kweli.
Ukimya wake una weza kutafsiriwa kwamba,..."chadema hapanifai kama kule nilikokua"

2.Sugu au Mr.II au Mbilinyi
Huyu nae,nashindwa kumtofautisha na komba (yule muimba kwaya wa ccm)!
Naamini wananchi walimchagua sababu ya kuimba kwake na sio kuamini kwamba
ana uwezo wa kuwa wakilisha bungeni.
Kaongea mara kibao bungeni,hakuna siku aliongea point hata moja zaidi
ya kufuka kama wabunge wa ccm

3.Joseph selasini
Huyu nae sijui historia yake kisiasa,ila naamini akirudi kugombea leo hii jimboni
kwake hashindi ng'o!
Ni mtu asiye na msimamo hata kidogo juu ya anacho kiamini,ana geuzwa na upepo
mdogo sana,...watu kama hawa ni magalasha

4.Shibuda
huyu sababu ya kuingia chadema ni sawa na rose kamili,
sababu ya ukimya wake ni sawa na kamili pia.
Ingawa yeye mara nyingi kaonesha kwamba yuko na
chadema kwa bahati mbaya bila kuficha. hili ndio galasha kuu ndani ya chadema

Ni hao kwa sasa,ntaleta wengine,...
Am still watching


Mkuu naona unawaone bure hawa Wabunge....

Kimsingi mpaka sasa ni Mbowe, Zitto, Tindu Lissu, Mnyika na Halima Mdee pekee wanaoibeba Chadema kwa kutoa michango yenye hoja za maana, ni hawa Wabunge watano tu walioonyesha uwezo wa uwakilishi wenye level ya kutumainika na kutia moyo, wengine woote waliobaki wamebaki kuwa ma-zeroo bungeni ilmuradi wameongeza idadi ya Wabunge wa Chadema...,hivyo kuwataja hawa wachache ni kuwaonea.

Ila nitawapa kigodo benefit of doubt Godbless Lema na Wenje kwa juhudi zao za nje ya Bunge, wengineo woote ni mizigo mizito bungeni na nje ya bunge...
 
kaka ni mapema mno kuwahukumu,kumbuka ni mwaka wa kwanza tu ndio unaisha bado miaka minne,tuwape muda na sidhani kama bungeni ukitaka kuongea unapewa nafasi tu,kuna list naonaga anaisoma spika,hii inaonesha sometimes muda wa kuongea unakosekana(not sure)ndio maana wabunge wengine wanachangia kwa maandishi,..sometimes unaweza ukafanya mambo makubwa jimboni kwako bila kuongea bungeni na unaweza kuwa muongeaji bila matendo,..anything is possible

Really?
okey najua watatetewa kwa hali na mali ila ukimya wao una
ujumbe ndani ambao hamuuoni,...
 
kwa mara ya kwanza leo umechemsha kaka

Tegemea mimi kuchemsha sana na kuivisha pia,..
naamini siku nikuwa upande wako utaweka "like" kwenye post yangu,,...until then keep waiting
 
Naona kuna kaukweli kidogo wabunge waliotajwa wajiangalie!
SUGU mbunge wangu unagombana na Fiesta umeshamaliza matatizo ya wanambeya.
Uwe makini Mbeya si watu wakupelekwa pelekwa tuuu wanahitaji mbolea ya ruzuku kaisimamie!

Sijaongelea fiesta na jafarai na clouds yenu,...
nimeongelea umakini wake katika kuwakilisha wananchi wake
na umakini wa kile anacho ongea akipewa nafasi,...
fiesta ni burudani kama burudani zingine na kila mtu ana burudika
 
wewe kijana ,pepa vipi? pole na pepanaona upsteaz kuna mushkeli tayari

Pepa zinaenda fresh mtakatifu,i hope unaishi vyema kwa matumaini
jombaa,mbona mtaani kwetu haupo siku hizi vipi?
 
We ulitaka wafanyeje wakati werema keshasema kuongea bungeni ni kutafuta umaarufu? Wanapigana vita vya ardhini ndo maana
 
Kwa evaluation yangu hadi sasa,wabunge wafuatao
hawafanani na chadema kabisa,msaada wao kwa chadema ni sifuri

1.Rose Kamili
alihamia chadema baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni
ccm,toka aingie bungeni amekua kimya kweli tofauti na nilivo kua nikimsikia enzi zile
akiwa diwani wa ccm,...alikua machachari kweli.
Ukimya wake una weza kutafsiriwa kwamba,..."chadema hapanifai kama kule nilikokua"

2.Sugu au Mr.II au Mbilinyi
Huyu nae,nashindwa kumtofautisha na komba (yule muimba kwaya wa ccm)!
Naamini wananchi walimchagua sababu ya kuimba kwake na sio kuamini kwamba
ana uwezo wa kuwa wakilisha bungeni.
Kaongea mara kibao bungeni,hakuna siku aliongea point hata moja zaidi
ya kufuka kama wabunge wa ccm

3.Joseph selasini
Huyu nae sijui historia yake kisiasa,ila naamini akirudi kugombea leo hii jimboni
kwake hashindi ng'o!
Ni mtu asiye na msimamo hata kidogo juu ya anacho kiamini,ana geuzwa na upepo
mdogo sana,...watu kama hawa ni magalasha

4.Shibuda
huyu sababu ya kuingia chadema ni sawa na rose kamili,
sababu ya ukimya wake ni sawa na kamili pia.
Ingawa yeye mara nyingi kaonesha kwamba yuko na
chadema kwa bahati mbaya bila kuficha. hili ndio galasha kuu ndani ya chadema

Ni hao kwa sasa,ntaleta wengine,...
Am still watching

Unatafuta kutukanwa na wenye chama chao!
 
We ulitaka wafanyeje wakati werema keshasema kuongea bungeni ni kutafuta umaarufu? Wanapigana vita vya ardhini ndo maana

Kwa hiyo werema ndo ana dictate wabunge wa chadema wafanye nini?
akiwaambia wamekuja bungeni kwa sababu hawana kazi ingine
ya kufanya wataondoka bungeni sio?
 
je na huyu Papa wa ufisadi , mnausikiaga mchango wake
62206_101116039952044_100001609443743_5955_5865122_n.jpg
I hate this man! Nachukia na chama chake
 
I hate this man! Nachukia na chama chake

Usi mchukie yeye,chukia roho ya wizi aliyo nayo na umuombee
it's healthy for you na Mungu ata kubaliki,maybe atabadilika na kurudisha vyote alivo iba
 
Mkuu Speaker, Si uwe fair utuwekee hapa na magalasha ya CCM na vyama vingine??

Hahaha,mkuu ccm nitajaza thread kwa majina,...
hawa ni magalasha lakini naamini wanaweza kubadilika wakiamua au
wakisaidiwa kujua nini cha kufanya (sio shibuda lakini)
 
Hawatakubali. Hawajui kujikosoa. Kwao kila kitu ni safi.
 
Back
Top Bottom