Magaidi washambulia bunge la Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,174
2,000
Kuna tetesi kuwa magaidi wameshambulia bunge la Iran na Haram ya Imam Khomeini
Moto umewaka.
---------------------

The Tasnim news agency is reporting that seven people have now died in the attack on the Iranian Parliament.

The Fars and Mehr news agencies are reporting on their feeds: “A person entered Iranian parliament today and started shooting at the guards. He shot one of the guards in the leg and ran away."

Iranian state TV has reported that there were four attackers in parliament with one person killed and eight people injured.

The situation is still ongoing, according to the broadcaster.
--------------

Habari zaidi..

Watu wawili akiwemo afisa wa usalama wameripotiwa kuuawa huku watu wengine wanane wakijeruhiwa baada ya watu waliojizatiti kwa silaha kushambulia majengo ya Bunge la Iran na Haram ya Imam Khomeini MA, katika mji mkuu Tehran.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, watu wanne waliokuwa wamejizatiti kwa bunduki za AK47 na bunduki moja ndogo wamefyatua risasi ovyo wakilenga walinzi wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ambapo mlinzi mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Hata hivyo shirika la habari la ISNA limenukuu mbunge mmoja wa Tehran, Elias Hazrati akisema kuwa hali hiyo imedhibitiwa na mvamizi mmoja ametiwa mbaroni.

Wakati huohuo, shirika la habari la Fars limeripoti kuwa, mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya watu watatu waliobeba silaha kuvamia Haram ya Imam Khomeini MA, viungani mwa Tehran. Mmoja wa wavamizi hao ameuawa na maafisa usalama, mwingine ambaye anasemekana kuwa mwanamke amejiripua huku wa tatu akijeruhiwa na kukamatwa na vyombo vya usalama.

Duru za kiusalama zimeripoti kuwa, fulana lililosheheni mada za miripuko la wavamizi hao katika Haram ya Imam Khomeini MA limepatikana na kuharibiwa.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,191
2,000
Duh! Mvurugano Uarabuni na Uajemi! Hawa watu waliwalea wenyewe matokeo ndio hayo. Shetani always hafugiki; kuna siku atakugeuka wewe mwenyewe. Matokeo yake ndio hayo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom