MAFUTA YAMESHUKA,UMEME WANASHUSHA MBONA NAULI WAMEKUWA KIMYA

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
16,358
22,506
Kila mtu anajua bei ya mafuta ilivyoshuka nab ado inaendelea kushuka hii imepelekea shirika la umeme kuomba bei ya umeme ishushwe ingawa kazi hii ilitakiwa ifanywe na baraza la walaji linalotakiwa kutetea watumiaji umeme sasa hilo baraza sijui lina kazi gani kwani halina msaada wowote ila tunashukuru angalau Tanesco wameonyesha usitaarabu.

Lakini wote tunajua nauli ikipanda kidogo vyama vya usafirishaji vinavyowakilisha daladala na magari ya abiria kwenda mikoani vinakimbilia SUMATRA kuomba nauli ziongezwe lakini mpaka sasa sijasikia chombo chochote au hata magazeti yakidai nauli ipungue kutokana na bei ya mafuta kushuka.

Je nani atamtetea huyu mwananchi wa kawaida kumpunguzia makali ya maisha?
 
Back
Top Bottom