Wakuu tusipende kucheza sandakarawe na maisha yetu..., tunajua kabisa kwamba vitu vingi ni sumu ila vikifanyiwa treatment vinakuwa salama mfano
Maharage yana sumu (ukila mabichi) lakini yakipikwa ile sumu inatoka
Mihogo vilevile ina sumu ila ikifanyiwa treatment inakuwa salama
Kisamvu kina sumu ila ukikipika sana kinakuwa salama
Mwarobaini ukitumia sana inaweza ikaleta infertility
Sasa wakuu umeshaambiwa mafuta ya ubuyu yana sumu (kwahio usiyanywe) ila unaweza kutumia externally, au kama unaweza kuyafanyia process kuondoa hizo sumu basi ni salama..., sasa cha maana badala ya kulalama ni kuchukua opportunity ya kuweza kuondoa hizo sumu ili iwe salama.
Kumbuka pia kuna vitu hapo zamani tulidhani ni salama kumbe baadae tukafahamu kwamba sio salama