Mafuta ya taa kwenye chakula, kuuwa Albino, ukeketaji, majini, hirizi, yote sisi

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
635
Mbona Watanzania tumejaa na imani za ajabu ajabu mno?! kuwawekea watoto wetu mafuta ya taa mashuleni, kuuwa albino, kukeketa, kuuwa bibi zetu wenye macho mekundu, kuogopa sensa, kuganga sehemu za biashara, wanawake kutuwekea limbwata (sumu), kuvaa mahirizi, kuamini majini, kuamini manabii feki kama kina gwajima, kikombe Loliondo, kakobe, lwakatare, joshua n.k.
TUNA MATATIZO KWENYE AKILI? JE TATIZO NI ELIMU AU NINI?! TUNATISHA!
Haya yote ndiyo yamesabibisha umaskini, shida, kutokuendelea, na ndio sababu hata wakandarasi wanababaisha tu, waalimu, askari na wafanyakazi wengi kuwa vyeti feki sababu ya uvivu wa kufikiri na kuogopa kutoa jasho kwa lolote tulifanyalo, kila sekta nchini ina kasoro, kuomba kazi wepesi kuifanya shida, ubabaishaji, wizi, utoro na kutokuwajibika..
WATANZANIA TATIZO LETU NINI HASA?
KARIBUNI
 
Umeonyesha utupu wako kwa kuchanganya masuala ya ulimwengu wa macho na ulimwengu wa roho!.

Wenye ufahamu huongelea lile wanalolijua tu!.

Umeshindwa kuonyesha ufahamu katika jambo hata moja uliyoyataja. Hivyo huwezi kuwa na suluhu bila kuelewa unachokisema.

Taftua maarifa kwanza. Kumcha Mungu ndiyo chanzo cha maarifa. Siyo katika confusions zako.
 
Mafuta ya taa tumelishwa sana enzi za shule lakini bado watu walikuwa na ashki ya kungonoka.
 
Mafuta ya taa kwenye maharage ya Tabora Boys.
Second master alikua anasema yanasaidia kupunguza hamu ya ngono.
 
Umeonyesha utupu wako kwa kuchanganya masuala ya ulimwengu wa macho na ulimwengu wa roho!. Wenye ufahamu huongelea lile wanalolijua tu!. Umeshindwa kuonyesha ufahamu katika jambo hata moja uliyoyataja. Hivyo huwezi kuwa na suluhu bila kuelewa unachokisema. Taftua maarifa kwanza. Kumcha Mungu ndiyo chanzo cha maarifa. Siyo katika confusions zako.
Hata wewe pia kwenye replies zako zote, umeonyesha maarifa ya kuponda na kujifanya kutetea yasiotetewa bila maarifa, nakuona unafanya yako pia! Zuzu kabisa, watu wanaona sasa sio kama zama zile, endelea kutumika mzembe wa akili kabisa wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom