mizambwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2008
- 4,422
- 1,790
Wana JF kuna mafuta machafu yaliyoingizwa nchini na TPDC na kuyauza katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda yamerudishwa nchini kwasababu mafuta hayo ni machafu kupindukia na nimepita ktk mpaka wa Kabanga nimekuta kuna malori kama matano ikabidi niende Rusumo nikakuta pia malori mawili moja la kitanzania na lingine la kinyarwanda mali ya Merez la kitanzania ni kampuni ya Bridgeway na nimeambiwa yapo mengine Kampuni ya Worldoil na Liberty yanakuja.
Source mimi mwenyewe. Pia napendekeza mwandishi wa habari aje apige kambi hapa awarushie hiyo taalifa live bila chenga
Aibuuuuuuuuu tanzania aibuuuu kwa serikali aibu kwa TBS na TPDC
hii ni taarifa nzuri sana kwani kuna ndugu zetu Madereva wamehamia Rwanda toka MWezi Feb 2012, ambao walipeleka haya mafuta.
Familiya zao zinaishi kwa shida sana.
Nashauri TBS wale wote waliohusika na kupima haya mafuta na kusema ni masafi wachukuliwe hatua.
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!