Mafuta huambaa juu ya Maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta huambaa juu ya Maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jun 2, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Awali ya yote nianze kwa kumsifu Masako kwa jinsi alivyowaalika watu wenye mitizamo tofauti ktk kipindi cha Kipima joto cha ijumaa (jana) na zaidi ni jinsi alivyokuwa wazi kuruhusu maoni mbalimbali juu ya suala la Muungano wetu.


  Marekebisho mawili ni kama ifuatavyo:


  1. Mada ya majadiliano ingekuwa kuhusu Chanzo cha manung├║kilo Zanzibar na suluhisho lake kuliko kuuliza kaswali ka kindergarten eti kama kikundi cha fujo Zanz kiko juu ya sheria jibu ambalo hata kila mtoto analijua!


  1. Mwakilishi wa Polisi Zanzibar au mwakilishi wa Chombo cha Usalama mwenye taarifa ya kilichotokea naye angealikwa ili pia aeleze na kujibu maswali yaliyoibuka mfano: Sababu ya kumkamata Kiongozi wa Kikundi walichokipa ulinzi wakati wanakutana na kujadili juu ya suala la Muungano pasipo ukiukwaji wowote.

  Uchambuzi wa haraka:

  Uchambuzi wa Mh. Risssu, una uzito na mashiko wakati hoja za Mwakilishi wa Kituo cha haki za Binadamu na aliyefika amechelewa zilikuwa nyepesi sana na hivyo wakabaki wakiambaa ambaa juu kama mafuta juu ya maji!

  Hoja ni kuwa Wananchi waachwe wazungumze kama wanautaka Muungano na uwe wa aina gani. Nashauri Terms of Reference za Tume ya kukusanya maoni zirekebishwe Bungeni.
  Na hakika ingestahili iwe Tume ya kupata maoni juu ya Muungano kwanza kabla ya kukusanya maoni mengine juu ibara nyinginezo katika Katiba. Yaani, Wananchi watapata kutoa michango yao vyema juu ya Katiba wakiwa wamejua ni Katiba ya Serikali au Shirikisho la aina gani .


  Kauli za yule mzee Kiongozi wa Wanaharakati aliyesema kuwa ndiye anaongoza madai ya uhalali wa Muungano sizichukuliwe kama vitisho tu! Tumsikilize pia Prof. Shivji anapochambua neno uhalali wa kisheria na wa kijamii!
   
Loading...