Mafuta asilia kwa ajili ya kukuza nywele zako na kuzifanya ziwe laini

ben brancoII

Member
Mar 19, 2017
40
27


Watu wengi hupenda sana nywele zao ziwe katika muonekano mzuri na zenye afya tele,katika hali ya kutafuta mafuta ya kuweza kuziboresha zaidi watu wengi hujikuta wakitumia gharama nyingi katika kununua mafuta mbalimbali yenye makemikali na hatimaye kujikuta wanapata athari ktk nywele zao bila kutegemea.


Le nitazungumzia mafuta mafuta mazuri ya asili ambayo yana uwezo mkubwa wa kujaza nywele zako,kuzifanya ziwe imara na zenye kupendeza muda wote

MAFUTA YA PARACHICHI

Mafuta haya yana virutubisho vingi kama vile A,B,D na E,Protin,iron,magnesium ambazo husaidia kukuza nywele
Mafuta haya pia hurekebisha nywele zilizokatika,yanalainisha na kungarisha nywele na pia kuzilinda kutokana na kuungua na jua kali.
pia unaweza kuyatumia kwa kuchanganya na shampoo wakati unaosha nywele zako.


MAFUTA YA MNYONYO


Mafuta haya yana vitamin E na protini kwa wingi ambayo inasaidia kukuza nywele na kuziepusha na kukatikakatika,kama nywl zinakusumbua jaribu mafuta haya sasa uone maajabu yake,

~huondoa mba kichwani mwako
~kuponya vidonda vya magonjwa ya ngozi kichwani
~zinakuza nywele zako mara3 zaidi ya ukuaji wa kawaida
chukua haya mafuta na uwe unamassage polepole kichwani
wengi waliotumia mafuta haya wanakiri nywele zao kukua kwa haraka kuliko kawaida

MAFUTA YA NAZI


Mafuta haya husaidia sana kuzipa nywele unyevunyevu kama zikiwa ni nywele kavu sana,unaweza kutumia mafuta haya kama conditioner,ukishaosha nywele zipake haya mafuta yanasaidia kukuza nywele pia huondoa mba
 
Asante sana kwa hili maana nywele zangu zinapukutika sio kukatika huku.. Tena vipisi vidogo vidogo
 
mafuta ya parachichi yanatengenezwaje? mi natumia ya nazi nachanganya na castor pamoja na argan oil, nywele zinakua laini na haziwashi
 
Back
Top Bottom