RAHA KAMILI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 203
- 83
Mhandisi Cosmas Kinasa akizungumza machache wakati akifunga rasmi semina ya ujasiriamali ya "Manjano Dream-Makers" kwa wanawake wa mkoa wa Mbeya akimwakilisha meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya. Mafunzo ya ujasiriamali hayo yametokewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali, vipodozi na urembo kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana naMhandisi Cosmas Kisana Akizungumza Machache Wakati akifunga Rasmi Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Mbeya Kwa Niaba ya Meneja wa Sido Mkoa wa Mbeya.Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 30 kutoka Mkoa wa Mbeya Yamemalizika. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya ni Miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara Kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo kama hayo yatafanyika pia kwenye mikoa ya Mtwara,Tabora na Kigoma mwaka huu wa 2017.
Washiriki walionufaika kwenye mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mhandisi Cosmas Kinasa.
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru Mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.