Mafunzo ya kuendesha asasi ndogo za kifedha

Mafunzo ya kuendesha asasi ndogo za kifedha

Chakarika Mafunzo

New Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4
Reaction score
1
CHAKARIKA ni wataalamu na wazoefu wa shughuli za uendeshaji wa shughuli za asasi za utoaji mikopo. Tumeaandaa kifurushi cha mafunzo kwa ajili ya wamiliki/watendaji wakuu na maafisa mikopo ili kuweza kuboresha utendaji. Tunafahamu kuwa Taasisi nyingi zimeanzishwa na watu ambao hawana utaalamu wala uzoefu katika sekta hii hivyo tumeona ni vyema kuwapatia mafunzo ya msingi ili kuongeza ufanisi na kupanua Huduma za kifedha.

Tofauti yetu na wafundishaji wengine ni kuwa sisi tunafundisha uhalisia kwa mazingira halisia na sio nadharia kutoka sehemu zingine. Mafunzo yetu ni mahsusi kwa kila Taasisi na yanaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili na yanazingatia uwezo wa kielimu na kitaaluma kwa wafanyakazi . Bei zetu ni nafuu sana kulingana na uwezo wa kifedha wa Taasisi hizi, kwani nyingi ndio zinaanza na hazina mitaji mikubwa.

AINA YA MAFUNZO TUNAYOTOA:

  • NGAZI YA MMILIKI AU MTENDAJI MKUU WA TAASISI

  • Namna ya kuaandaa sera mbalimbali za Taasisi. Mfano, Sera ya mikopo, sera ya usimamizi wa rasilimali watu, sera ya fedha/Uhasibu nk

  • Taratibu za kuanzisha, kusajili na kuendesha asasi ya kifedha

  • Kujifunza takwimu za msingi za kukusaidia kufanya tathmini ya utendaji wa maafisa mikopo na Taasisi kwa ujumla

  • Kufanya tathmini na upembuzi kubaini kama Taasisi inajiendesha kwa faida au hasara

  • Kufanya tathmini na kuibua au kuzuia mianya ya ubadhirifu au wizi

  • Jinsi ya kutunza mafaili na mpangilio mzuri wa nyaraka

  • Kufanya usaili na kusaidia kuajiri wafanyakazi wa Taasisi za mikopo

  • Mambo ya msingi kuyatenda ili kuzingatia sheria za nchi


  • NGAZI YA MAAFISA MIKOPO

  • Jinsi ya kupata wateja wapya na kubuni Huduma mpya

  • Jinsi ya kufanya tathmini ya biashara, mkopaji na wadhamini wake

  • Jinsi ya kuaandaa faili la maombi ya mkopo, kujadiliwa na kupitishwa na kamati

  • Mbinu za kutunza mkopo ili usiharibike na kuwa mkopo mbaya (mkopo karisaji)

  • Jinsi ya kufuatilia na kudai marejesho kwa wateja waliochelewesha mkopo

  • Kujifunza takwimu za msingi za kukusaidia kufanya tathmini ya utendaji wa maafisa mikopo na Taasisi kwa ujumla

  • Kufanya tathmini na upembezi kubaini kama Taasisi inajiendesha kwa faida au hasara

  • Kufanya tathmini na kuibua au kuzuia mianya ya ubadhirifu au wizi

Kama unahitaji baadhi ya mafunzo hayo unaweza kuwasiliana kwa namba hii 0620307161 au kwa email hii chakarikamafunzo@gmail.com Hata kama mafunzo ni kwa mtu mmoja tupo tayari kutoa Huduma hiyo. Pia tunaweza na tunapendelea kutoa mafunzo katika eneo la utendaji la Taasisi husika ili kupata nafasi ya kujifunza kwa vitendo zaidi.

Ofisi zetu zipo Maghorofa ya Urafiki Shekilango Kitalu H, Nyumba namba 24 mwishoni kabisa mwa jengo la kituo cha polisi Urafiki kama unatokea Ubungo.

Karibuni sana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom