Mafundi wa Tanzania mtabadilika Lini?

Mafundi wa Tanzania mtabadilika Lini?

Ikiwa Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda kama wasemavyo wangu ni wakati wa mafundi (fundi ujenzi,welding,umeme,fenicha nk) kuacha umagumashi.

Mafundi wa mitaani waongo,wezi,matapeli,wadhurumat,hawana bei standard,wanalipua kazi,hawafanyi kwa wakati.Yaani wamekaa kiujanjajanja.Mafundi badilikeni.

Hatutakuja kuendelea maana unakuta mfano kitu flani kumeharibika kinahitaji repair kidogo.Ni bora hata ununue kipya,vinginevyo itakugharimu sana.Wengi hususiwa na wateja wao.Ni bora ununue kabati mchina fomeka kuliko kukimbizana na fundi.

Ingekuwa vizuri huko vyuoni kama VETA wafundishe ethics za fundi.

Wadau mnasemaje?

Nitafute Mimi kwa ufundi ujenzi plasta nk
 
hata ma contractor hawana bei standard wanatofautiana experience, quality na hata mahitaji yako. pia nafkiri hoja pekee sio kwa fundi peke yake bali hata mhusika unam treat vp fundi. mmekubaliana kazi mil 1, unamlipa laki 5 na haja anza kazi, kesho akikosa hela ya kuwalipa vibarua wake unalalamika.
 
Kama ndugu zangu mlio kwenye ujenzi ndio mnaumia kweli maana ninavyowasikia huku mitaani wanavyojisifia mimi mpaka napata hasira kabisa.....

Kwanini ndugu zangu msifanye hata window shopping ya vifaa hivyo at least hata wiki mbili kabla ya ujenzi wako.....

Unaenda dukani na fundi ndio huko huko anakwenda kukumaliza....maana wale jamaa maduka mengi wanafahamika....wanafanya wizi huo wakishirikiana na vijana wa dukani wasio waaminifu.....yaani kifaa cha elfu mbili unaweza ukaambiwa elfu kumi......kifaa cha elfu kumi unaambiwa elfu ishirini......

Ukimuuliza fundi lazima atakuelekeza kwenye duka la mwizi mwenzie....yaani wewe upo njiani wenzako wameshapigiana simu kuwa uchinjwe tu......

Ushauri wangu

Usiende kwenye duka la fundi mliloelewana au mtume mtu kesho yake aende akaulizie bei alafu ulinganishe na bei uliyoambiwa.....

Kama ukienda kwenye duka alilokuambia usinunue vitu siku hiyo hiyo ulizia tu bei........

Jitahidi ujue mahitaji ya ujenzi wako kabla ya kumuita fundi au kabla hujaanza ujenzi......

Unaweza ukamuita fundi aje akufanyie vipimo vya mradi wako na mahitaji ya vifaa huku ukimsisitizia kuwa bado hujajipanga kuanza ujenzi hivi karibuni....hiyo itamvunja moyo fundi na kukupa vipimo vya uhakika na mahitaji halisi ya vifaa vyako.....

Baada ya hapo kama huna haraka anza kununua mwenyewe vifaa taratibu....na ukifika huko madukani usigande sana na bei za duka moja...tembelea maduka mengi ili upate unafuu wa bei.....

NB; Kinachowaponza mafundi ni tamaa...
Ni kweli Unapojenga vifaa vyote nunua mwenyewe baada ya kuuliza bei kwenye maduka kadhaa
 
Poor excuse Mkuu. Then you have to learn to negotiate. Na kama nimekuumiza bei..well tell me in my face..mzee hii pesa unayoitoa hutapata kazi ya kiwango unayoitaka. So the choice is yours. Otherwise wengi tumekuwa wababaishaji. Na unajua hata mhitaji wa huduma anakulipa kutokana na anavyokuona, previsous kazi zako etc.

Hivi mfano nataka fundi wa tiles...ananiambia mzee kazi yangu niliyoifanya ni pale Serena hotel au nilibandika Tanga stones pale mlimani city...(mfano)...hivi unajua hata ku-mapproach mtu kama huyo itabidi nijipange? kwa sababu I know he represents quality.

Always, binadamu ndo ana determine value yake.

naona tunaongea kitu icho icho..
 
Hili suala haliko kwa mafundi tu mkuu..hata watu au sehemu usizofikiria. UAMINIFU na UADILIFU ni mtihani sana hapa Bongo.

Niliwahi kupeleka saa yangu kwa matengenezo katika duka moja maarufu sana maeneo ya mjini karibu na askari monument. Nilipofika pale nikakuta wahindi wawili mtu na baba yake...na mafundi wa kibongo wako pembeni.

Wakaichukua saa waangalie tatizo ni nini. Baada ya muda kidogo yule Muhindi (Mtoto) akanifuata na kunijulisha ile saa imekufa utumbo...kwa hivyo gharama ya kuweka mashine mpya ilikuwa Tsh 400,000/=....niliishiwa nguvu palepale. Maana hiyo saa thamani yake mpya haikufika hiyo bei ya marekebisho.

Nilichofanya nilitoka kwa nje pembeni kuna fundi viatu. Na mimi nikatumia akili yangu ya Kitanzania nikapata namba ya yule fundi mtaalam wa pale ambaye ni Mbantu. Nikaelekezwa nimpigie simu baada ya saa 12 jioni. Nilifanya hivyo na kesho yake mapema nilikutana nae kabla hajaingia kazini nikamkabidhi saa. Jioni tukakutana akanikabidhi saa ikiwa inafanya kazi...nikamlipa 50,000/=. Akaniambia tatizo lilikuwa ni spring betri ilivuja ikapata hitilafu. Na haikuwa tatizo la kubadili mashine kama nilivyoelezwa awali.

Watanzania tunaumizwa kila kukicha. Ni kuwa makini tu.
Wanaitwa Babla
 
Fundi aliyeniacha hoi alipelekewa mbao 8 zikiwa bado hazijakauka vizuri sasa baada ya wiki kadhaa jamaa akafuatilia kufika kwa fundi mbao zimebaki 4 kumuuliza fundi mbao mbona zimebaki 4? Fundi baada ya kukauka vizuri zimebaki hizo jamaa akabaki anacheka tu asijue hata la kumfanya?
Mhhh. Hujatia chumvi kidogo?
 
Uelewe wa watu ktk mambo yakifundi ni mdogo kuna watu si mafundi hana msingi wowote ktk ufundi ajipachika tu. Pia wateja hawajui thamani ya vitu kmfano mtu anataka kitanda mbao mninga gharama ya mbao tu, 420,000. Mteja anataka kwa 600,000. Kazi hiyo fundi iinamchukua siku 7.kweli fundi atafanya hiyo kazi kwa viwango?
 
Halafu kuna kitendo flani cha mafundi wengi hasa hawa wa vitu vya umeme mfano television, Ukimpelekea na kumwambia tatizo utamuona kaifungua halafu katoa kifaa flani halafu anaanza kukigongagonga na bisibisi sambamba na kukipuliza

Sasa ukijaribu kuangalia anachokifanya hapo mara nyingi ni ujanja ujanja tu na maneno mengi, mwisho wa matengenezo atakutaja bei ya ajabu ajabu tu ilhali alichofanya hapo huoni kama kina thamani hiyo..mafundi tunawahitaji lakini sometimes mnakosa ukweli na uaminifu kwenye kazi zenu
Tv peleka sehemu kama Samsung Center au Sony au Lg center kule safi yani uhakika
 
Back
Top Bottom