muhomakilo jr
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 15,835
- 14,727
Hao ndo majanga,atakwambia lete machozi ya simba,mkojo wa mamba,au kama huna pa kuvipata lete fedha nikatafute mwenyewe...Fundi mganga wa kienyeji
Hao ndo majanga,atakwambia lete machozi ya simba,mkojo wa mamba,au kama huna pa kuvipata lete fedha nikatafute mwenyewe...Fundi mganga wa kienyeji
Ikiwa Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda kama wasemavyo wangu ni wakati wa mafundi (fundi ujenzi,welding,umeme,fenicha nk) kuacha umagumashi.
Mafundi wa mitaani waongo,wezi,matapeli,wadhurumat,hawana bei standard,wanalipua kazi,hawafanyi kwa wakati.Yaani wamekaa kiujanjajanja.Mafundi badilikeni.
Hatutakuja kuendelea maana unakuta mfano kitu flani kumeharibika kinahitaji repair kidogo.Ni bora hata ununue kipya,vinginevyo itakugharimu sana.Wengi hususiwa na wateja wao.Ni bora ununue kabati mchina fomeka kuliko kukimbizana na fundi.
Ingekuwa vizuri huko vyuoni kama VETA wafundishe ethics za fundi.
Wadau mnasemaje?
hata ma contractor hawana bei standard wanatofautiana experience, quality na hata mahitaji yako. pia nafkiri hoja pekee sio kwa fundi peke yake bali hata mhusika unam treat vp fundi. mmekubaliana kazi mil 1, unamlipa laki 5 na haja anza kazi, kesho akikosa hela ya kuwalipa vibarua wake unalalamika.
Tena hawa ndio usiseme mkuu. Nilimpa tenda kijana wa mtaani kunijengea kibanda kidogo cha kuku wa kienyeji wa kula nyumbani. Eeeeh bwana weee...nilikoma. Utafikiri nilikuwa najenga mradi wa uDART.Wale unaojuana nao utakuta wanalalamika ukimpa kazi mtu mengine.Utaskia "boss umeninyima fursa mi wa mtaani kwako "
wakisoma comment yako watajifunza sio kila wakipokea kazi cha kwanza ni kuomba advanceMafundi wa Kenya proffessinal zaidi. Anafungua kifaa anafanya uchunguzi(unalipia uchunguzi), halafu pale pale anakwambia hiki hiki kibovu. Inayo hiari kwenda kununua spare au unamwachia hela ashugulikie. Nimedili na mafundi Kenya mara ya kwanza TV na ya pili DVD player. Nimepeleka mzigo asubuhi amini usiamini kabla mchana napigiwa simu niende kuchukua mzigo!