Mafundi wa Azam TV wamelala

Mafundi wa Azam TV wamelala

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
802
Reaction score
657
Ni muda mrefu sasa Azam TV inaonesha hali ya uchafu unaoingiliana na muonekana wa picha. Uchafu huo upo muda wote wa matangazo, ambapo awali mimi nilidhani tv yangu ina matatizo lakini kumbe tatizo hilo la kujivuruga kwa picha nililiona pia kwenye tv za jirani.

Lakini mara matangazo ya mpira ya CHAN kule Cameroun yalipoanza kwa kurushwa na tv ya ZNZ 2 hali ya kuvurugika kwa picha ilipotea kabisa. Ndipo nilipokuja kugundua sasa kuwa tatizo la kujivuruga kwa picha ni kwa Azam tu.

Sasa ni jambo la ajabu kuona hii hali ikiendelea kwa muda mrefu bila kufanyiwa marekebisho na mafundi wa Azam tv. Tatizo la Azam tv ni kwamba mtu mdogo akitoa malalamiko hayawezi kufanyiwa kazi hadi wakubwa waseme kuwa kuna shida kama hiyo ndio linafanyiwa kazi.

Tunatoa rai uongozi wa Azam waliangalie hili tatizo na kuliondoa.
 
Azam Media wabadilike kwakweli, yaaani Picha zinaganda na kuvujia utadhan tuko karne ya 18! Anyway kinachofanya niendelee kuangalia Azam ni VPL pekeee. Ikitokea hata kesho katokea mshindani wa kweli wa Azam kwenye VPL baaaaasi.
 
Kumbe shida ni wao? Nimebadilisha nyaya mara kibao nikidhani huenda zina shida duuh,kwa kweli inaboa sana aisee
 
Back
Top Bottom