Mafisadi wanafurahije bunge kutoonyeshwa live?

andy90

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
270
105
Katika hali ya kuuzunisha Mh.Rais unawaangusha wanyonge wa nchi hii hasa walioanza kuamini wewe ni jembe ingawaje mimi binafsi bado sijaona cha kusifia saaaanaa.

Kwa kifupi ni kuwa kutoonyeshwa kwa bunge live kuna wapa haueni wale wapiga dili na mafisadi kwani wengi wao tuliwafaham pale wabunge walipokuwa wakiwataja hazarani pale bungeni mf. Escrow, EPA, N.k hayo yote yalitoa somo kwetu wananchi na tukawafahamu wabunge waliomstari wa mbele kukemea ufisadi na wale wabunge mandumilakuwili tuliwafahamu,

Sasa iweje leo hii ambapo Mh.Rais umetanabaisha kwa utumbuaji na Majipu pamoja na kuwataja hazarani Mafisadi serikali yako kupitia wazir husika mseme hapana \bunge kuonyeshwa live?

Sisi wananchi tuamini vip dhamira yako ya Mafisadi kutajwa Hadharani,,,?? Iweje muogope bunge kuonyeshwa live ikiwa mnajiamini ni wasafi na mna nia njema ya kusafisha nyumba umpya,,

Mh. Rais naomba liangalie swala hili upya bila hivyo utawafanya Mafisadi wafurahie na kufanya sherehe kubwaaaa sana zenye shagwee.

Nawasilisha.
 
Kwa kifupi ni kuwa kutoonyeshwa kwa bunge live kuna wapa haueni wale wapiga dili na mafisadi kwani wengi wao tuliwafaham pale wabunge walipokuwa wakiwataja hazarani pale bungeni.

Msimamo wa UKAWA ni kuwa huwezi kumwita fisadi mtu ambaye hajahukumiwa na mahakama.UKAWA walikuwa wakimwita Lowasa FISADI bungeni baadaye wakageuka wakasema sio fisadi sababu hajahukumiwa na mahakama.Sasa hivi wanamtetea kwa nguvu zote kuwa si fisadi wakati walimtamka kuwa Fisadi bungeni.

Ili kuepusha ugeu geu wa kijinga kama huo na kulifanya bunge lionekane kama kikao cha wapuuzi wasio serious na vitu wanavyosema ndio maana ikaonekana kuwa ni heri vitu vyao wavijadili wenyewe vizuri na kwa uhakika wakivitoa nje viwe vyenye ushahidi na vilivyojitosheleza kuliko kulifanya bunge kama kikao cha wambeya ambao leo wanasema hiki kesho kile.Sasa hivi lazima wanavyosema vihaririwe kwanza virushwe baadaye ili kama mtu akimwita mtu fisadi ithibitishwe kwanza kama mahakama imemhukumu kabla ya kurusha LIVE

UKAWA wameshusha mno hadhi ya bunge hasa kwa Suala la Lowasa.
 
Aaah!!ukawa !!!!!!mbowe ndio baba yao kila analosema nyumbu wanakimbia anyway wabunge wa ukawa asilimia kubwa ni wasomi viazi
 
Siasa tuache pembeni kukataa kuonyesha live shughuli za bunge ni kasoro ya wazi katika utendaji wa serikali mpya full stop. Tulielewa kidogo Rais Magufuli alipoongelea gharama kubwa za TBC katika kulipia matangazo. Lakini mtu yeyote mwenye akili ya wastani anaona kuwa hiyo haikuwa sababu. Issue hapa ni kuua uhuru wa kupata habari na kutoa habari. Kwa kifupi ni kuua demokrasia. Swali ni kuwa serikali inaogopa nini? Kama ni Chadema kupiga kelele bungeni au kusususia mbona ni mambo ya kawaida hata kwa mabunge ya wakubwa. No bana ... kuna kitu! Whatever it is ni doa kwa serikali ya Magufuli.
 
Katika hali ya kuuzunisha Mh.Rais unawaangusha wanyonge wa nchi hii hasa walioanza kuamini wewe ni jembe ingawaje mimi binafsi bado sijaona cha kusifia saaaanaa.

Kwa kifupi ni kuwa kutoonyeshwa kwa bunge live kuna wapa haueni wale wapiga dili na mafisadi kwani wengi wao tuliwafaham pale wabunge walipokuwa wakiwataja hazarani pale bungeni mf. Escrow, EPA, N.k hayo yote yalitoa somo kwetu wananchi na tukawafahamu wabunge waliomstari wa mbele kukemea ufisadi na wale wabunge mandumilakuwili tuliwafahamu,

Sasa iweje leo hii ambapo Mh.Rais umetanabaisha kwa utumbuaji na Majipu pamoja na kuwataja hazarani Mafisadi serikali yako kupitia wazir husika mseme hapana \bunge kuonyeshwa live?

Sisi wananchi tuamini vip dhamira yako ya Mafisadi kutajwa Hadharani,,,?? Iweje muogope bunge kuonyeshwa live ikiwa mnajiamini ni wasafi na mna nia njema ya kusafisha nyumba umpya,,

Mh. Rais naomba liangalie swala hili upya bila hivyo utawafanya Mafisadi wafurahie na kufanya sherehe kubwaaaa sana zenye shagwee.

Nawasilisha.
Hata nami bado sjaingia kwenye mkumbo wa kusifia sifia na nashukuru kwa kuwa na msimamo huo maana hadi leo hii ulimwengu ungeni cheka
 
Msimamo wa UKAWA ni kuwa huwezi kumwita fisadi mtu ambaye hajahukumiwa na mahakama.UKAWA walikuwa wakimwita Lowasa FISADI bungeni baadaye wakageuka wakasema sio fisadi sababu hajahukumiwa na mahakama.Sasa hivi wanamtetea kwa nguvu zote kuwa si fisadi wakati walimtamka kuwa Fisadi bungeni.

Ili kuepusha ugeu geu wa kijinga kama huo na kulifanya bunge lionekane kama kikao cha wapuuzi wasio serious na vitu wanavyosema ndio maana ikaonekana kuwa ni heri vitu vyao wavijadili wenyewe vizuri na kwa uhakika wakivitoa nje viwe vyenye ushahidi na vilivyojitosheleza kuliko kulifanya bunge kama kikao cha wambeya ambao leo wanasema hiki kesho kile.Sasa hivi lazima wanavyosema vihaririwe kwanza virushwe baadaye ili kama mtu akimwita mtu fisadi ithibitishwe kwanza kama mahakama imemhukumu kabla ya kurusha LIVE

UKAWA wameshusha mno hadhi ya bunge hasa kwa Suala la Lowasa.
Mtamuongelea lowasa hadi mataya yenu yata pinda kama panga boi lkn mwenyewe yupo hadi sasa ana dunda na badala yake tunawashuhudia makada na wafadhiliwenu wakuu ndio wana buruzwa kwa pilato,mbona huyo fisadi mkuu mnaye muita lowasa hajaguswa hata kwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi?
 
M

Mmawia!!!sio hivyo ndg yangu hawa wapinzani wanakera sana!!!
Hata mimi naona wanakera kweli kweli kwani wanaendelea kuivua serikali yetu nguo na watanzania wanaelewa hayo madhambi ya watawala ndio maana tumeamua kuwapiga pini ili wasionekane wanavyo ivua serikali yetu tukufu nguo!!!
 
Wanaotaka kuoneka live wakaombe kazi katika vituo vya Tv
1461579283446.jpg
unaona raha mwenyewe
 
Nape na Mukama si ndio walikuwa wanazunguka wanawaita Rostam, Chenge na Lowasa mafisadi? Au umesahau? Mbona umechagua kuwalaumu UKAWA?

Msimamo wa UKAWA ni kuwa huwezi kumwita fisadi mtu ambaye hajahukumiwa na mahakama.UKAWA walikuwa wakimwita Lowasa FISADI bungeni baadaye wakageuka wakasema sio fisadi sababu hajahukumiwa na mahakama.Sasa hivi wanamtetea kwa nguvu zote kuwa si fisadi wakati walimtamka kuwa Fisadi bungeni.

Ili kuepusha ugeu geu wa kijinga kama huo na kulifanya bunge lionekane kama kikao cha wapuuzi wasio serious na vitu wanavyosema ndio maana ikaonekana kuwa ni heri vitu vyao wavijadili wenyewe vizuri na kwa uhakika wakivitoa nje viwe vyenye ushahidi na vilivyojitosheleza kuliko kulifanya bunge kama kikao cha wambeya ambao leo wanasema hiki kesho kile.Sasa hivi lazima wanavyosema vihaririwe kwanza virushwe baadaye ili kama mtu akimwita mtu fisadi ithibitishwe kwanza kama mahakama imemhukumu kabla ya kurusha LIVE

UKAWA wameshusha mno hadhi ya bunge hasa kwa Suala la Lowasa.
 
La
Hata mimi naona wanakera kweli kweli kwani wanaendelea kuivua serikali yetu nguo na watanzania wanaelewa hayo madhambi ya watawala ndio maana tumeamua kuwapiga pini ili wasionekane wanavyo ivua serikali yetu tukufu nguo!!!
Lakini serikali ilitoa utaratibu mzuri kwamba bunge litaonyeshwa live kipindi cha maswali na majibu baada ya hapo ili kuwapatia wananchi wengi nafasi ya kufanya kazi bunge litakuwa linaoneshwa via recorded na wakiwa wamehariri ili ule upuuzi wa kuzomea zomea usionekana kwa vizazi vyetu then hata watoto wakapuuzia bunge wakiona ni wapiga kelele wakati ni mhimili mkubwa wa serikali
 
Hakuna kitu hapoo
 
Fujo za wapinzani bungeni badala ya kuwashushia hadhi zinawaongezea umaarufu kwa wananchi hapo lazima tujiulize ni kwa nini... Kwa kuliona hilo serikali ya ccm ikaona mbinu ni kuondoa matangazo live ya mijadala bungeni. Hii inaoneka hata mikutano ya hadhara ya wapinzani itakapoanza kufanyika itawavuta watu tofauti na inavyoelezwa kwamba kwa sasa wananchi wamemkubali Magufuli na kuachana na UKAWA.
 
Nape na Mukama si ndio walikuwa wanazunguka wanawaita Rostam, Chenge na Lowasa mafisadi? Au umesahau? Mbona umechagua kuwalaumu UKAWA?

Waliyaongelea nje ya bunge sio ndani ya Bunge.Mimi naongelea UKAWA walioongea ndani ya bunge.
 
Back
Top Bottom