CHADEMA mkoa wa Mara walaani Bunge kutorushwa live

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Tarime. Sakata la Bunge kutoonyeshwa 'live' limeendelea kuwatesa wananchi. Mara hii, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Mara, kimetoa tamko la kulaani kitendo cha Serikali kutorusha matangazo moja kwa moja kwenye Televisheni ya Taifa (TBC).

Katibu wa chama hicho wa mkoa huo, Chacha Heche aliwaambia madiwani wa Chadema kuwa kuwa kutorushwa kwa matangazo hayo ni kuminya uhuru wa habari.

Heche alisema Chadema haikubaliani na utaratibu mpya wa urushaji matangazo kwa kuwa unakiuka uhuru wa wananchi kupata habari, hivyo wanaupinga na kuulaani.

“Rais Magufuli alisema atawatumbua majipu watendaji hadharani mbele ya wananchi, sasa iweje sisi wananchi tuliowachagua wabunge watuwakilishe bungeni matangazo yao yarushwe usiku tena kwa saa moja wakati wamekaa zaidi ya saa 10, jambo hili halikubaliki hata kidogo,” alisema Heche.

Madiwani wa kata za Kibasuka na Nyarukoba, Loyce Manyata na Bisendo Matiko walisema kupitia matangazo yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja yaliwasaidia kufahamu na kujifunza mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.
 
Back
Top Bottom