Mtu kama sitta, ni mzoefu wakuvuruga bunge, hata mwalimu NYERERE alimshtukia mwaka 1994. Sir hio nyeti imebainika kufwatia mambo mbalimbali spika huyo amewahi kuyafanya katika kipindi chake cha uongozi. Hata NYERERE aliwahi kukasirishwa na mwenendo wa SITTA, alielezea MAONO yake kupitia kitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA, imebainika swala la kutaka mashauriano na muafaka ili kuzuia mgawanyiko katika asasi nyeti anazoziongoza si jambo kubwa kwa SAMWEL SITTA, kama kwa mheshimiwa huyu angekua anajua ukubwa na hadhi ya ofisi aliyopewa, asingelitumia makanisa na vyombo vya habari kujitukuza. Kwa watu wanaomjua na historia ya SITTA yanayo tokea leo hii na yeye akiwa katikati ya matukio hayo siwezi kumshangaa. Uchunguzi unarudi nyuma, miaka ya nyuma kama kiongozi wa chuo kikuu cha DSM, SITTA alishiriki na kupanga maandamano ya kupinga kuanzishwa kwa jeshi la kujenga taifa (JKT) tukio hilo liliishtua serikali, alioiongoza MWALIMU NYERERE na taifa zima, ambapo vijana wake waliotumia pesa za wakulima na wafanyakazi, walitakiwa kua na moyo wakujitolea kujenga nchi yao na kwa kuchangia kwa namna yeyote maendeleo ya nchi. Watu waliohojiwa wanasema wanakumbuka wanafunzi hao walioandaliwa na SITTA waandamane huku wakibeba mabango yaliosomeka "AFADHALI YA MKOLONI" tukio kama hilo lilimuudhi sana MWALIMU NYERERE, mpaka alikifunga chuo kikuu na mpaka leo hajaomba radhi kwa yale yaliotokea 1966, uchunguzi mwingine unaonyesha akiwa waziri wa sheria na katiba katika serikali ya awamu ya pili. SITTA alishirika kwa kiwango kikubwa kulivuruga bunge kwa kuishauri serikali kukubali hoja ya kundi la G-55 la kubadilisha mfumo wa muungano, MALECELA ambae alikua alikua waziri mkuu alilazimishwa kuachia nafasi yake na kushikiliwa na CLEOPA MSUYA. Uchunguzi unaonyesha kua bunge la sasa au la miezi iliopita lilikua linaongozwa na SITTA ulikua unaturejesha enzi za mwelekeo wa siasa zakirasimu ambazo daima hupendelea kukitupa chama kando bila kujali matokeo ya muda mrefu. Ni wazi jambo la bunge kua na makundi na chama (CCM) kudhoofika havimsubui SITTA. Tunachopata kutoka kwake ni kwamba yeye yuko sahihi, wengine wote wanayempinga ni mafisadi. Na kwa namna yoyote anaongozwa na YESU. YESU NI WAWOTE ANAWEZA KUBINAFSISHWA??? ------Ninawahoji!!!!!!..........