Mafisadi na waharifu kufaidi BRN, masikini kukiona picha kamili hii hapa

donimuya

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
272
55
BRN tumeuiga kutoka Malaysia katika mpango wao waliouita BIG FAST RESULTS (BFR) hebu tulinganishe vipaumbele vya hii mipango miwili halafu tujiulize kama wenzetu wamefanikiwa je kwa hivi vipaumbele vyetu unapata hisia gani? kusoma hatujuwi je hata picha hutuoni? hasa tukizingatia kuwa matatizo makubwa tuliyonayo ni pamoja na ufisadi, uharifu mbalimbali na mengineyo

BIG RESULTS NOW (BRN)
1) Nishati na Gesi Asilia
2) Kilimo
3) Maji
4) Elimu
5) Usafirishaji
6) Resources Mobilization

BIG FAST RESULTS (BFR)
1) Kupunguza Uharifu
2) Kupambana na Ufisadi
3) Kuboresha matokeo ya wanafunzi
4) Kupandisha kiwango cha maisha cha watu wenye kipato cha chini
5) Kuboresha miundo mbinu ya msingi vijijini
6) Kuboresha usafiri wa umma, and addressing the cost of living.

JE NDUGU ZANGU WANAJF katika vipaumbele vyetu unadhani tumeweka misingi imara ya kusimamia utekelezaji, kulinda kitakachopatikana, kupima matokeo na kujuwa ni nani aliyefaidika na brn?
 
...daah kaazi kweli,macc kuishi nayo ni sawa na kulala kwenye shimo la siafu...
 
Watanzania siku zote hatukosi mipango mizuri.....kivumbi ni utekelezaji wake sasa.....kila mtu mkubwa anataka apige deal
 
CCM kwa speed ya kuko copy hawajambo .Una copy huku hujui misingi yake .Hapo walienda Malaysia wakala per diem kurudi wana anza uchuro .Hivi ile GO GREEN iliishia wapi na yale matrekta Manji na Riz walichukua mradi ?
 
Kwani hii Degree ya "Slogan" inatolewa na chuo gani Duniani? Siasa ni kilimo, Kilimo cha kufa na kupona, Ari mpya kasi mpya, ari zaidi kasi zaidi, Mkukuta, Kilimo Kwanza, Kujivua Gamba, BRN!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Labda kama tumebuni wenyewe lakini kama tumekopy hamna kitu hapo make yametushinda mengi sana tena rundo ...hatuwezi kwasababu wenzetu wameanza safari hatujuhi walianzia wapi,walijiandaa siku ngapi eti leo tunajifanya kudandia gari kwa mbele ...tusipokaa chini na kuandaa mambo yetu kwa kutizama aina ya maisha na watu tunaoishi Tz hatutaweza kufanya lolote kama nchi labda kama mtu mmojammoja tena kwa dili.
 
CCM kwa speed ya kuko copy hawajambo .Una copy huku hujui misingi yake .Hapo walienda Malaysia wakala per diem kurudi wana anza uchuro .Hivi ile GO GREEN iliishia wapi na yale matrekta Manji na Riz walichukua mradi ?

Mkuu waMalay wamekaa hapa Tz Zaidi Ya miezi mitatu
 
Ni leo asubuhi nilikuwa nasikiliza redio moja ivi,mtangazaji aliwa-interview watu kadhaa wa eneo la mwananyala,almost %100 ya wale watu walisema hawajui nini maana ya "BIG RESULTS NOW"
Kilimo kwanza ilianzishwa sikuona tofauti mpaka leo,hii ni shida ya mipango,malengo bila utekelezaji.
 
Angalia hivi vimetego Malaysia kipaumbele chao katika elimu ni kuboresha matokeo ya wanafunzi, kitu ambacho kinapimika, lakini sisi kipaumbele chetu katika elimu tumesema tu elimu haiko wazi, ifanye nini? Wenzetu wanaongelea kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha chini (which is measurable), sisi tunasema tu kilimo au mobilization of resources, without point out where or to whom, for what purpose. yaani kuna vimitego vingi vya kijinga. NA KAMA KAWAIDA WAJINGA NDIO WALIWAO, watoto wa mjini wanasema imekula kwetu.
 
nafikiri nimeeleweka vizuri tu mkuu kwa anayefahamu mambo yanavyoenda ngazi zote za serikali ya sasa .... hapo wanatoa idea nzuri lakini utashangaa hela yote inaishia kwenye semina, makongamano, kujengeana uwezo, safari, kujifunza, etc .... walichopanga hakifanyiki na hata hivyo vichache vitakavyofanyika ni ubabe, hakuna quality, ufisadi ndani yake!

Uko sahihi mkuu manurse baadhi wamekula ela ndefu kwenye semina bt mi navyoelewa sector ya afya tatizo ni vitendea kazi ari ya kufanyakaz imeshuka sabab ya mazingira sio rafik ivo vingin ni temporaly thing never work...ayo ndo maCCM yanapenda kuonekana kuliko kutoa matokeo chanya kwa ordinary citizen
 
Angalia hivi vimetego Malaysia kipaumbele chao katika elimu ni kuboresha matokeo ya wanafunzi, kitu ambacho kinapimika, lakini sisi kipaumbele chetu katika elimu tumesema tu elimu haiko wazi, ifanye nini? Wenzetu wanaongelea kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha chini (which is measurable), sisi tunasema tu kilimo au mobilization of resources, without point out where or to whom, for what purpose. yaani kuna vimitego vingi vya kijinga. NA KAMA KAWAIDA WAJINGA NDIO WALIWAO, watoto wa mjini wanasema imekula kwetu.

Napingana Na wewe, naomba tu niseme kuwa tatizo lililopo NI kuwa taarifa hazitolewi wazi km zilivyo, Kila wizara iliainisha mambo Ya kufanya Na jinsi Ya kupata mapato Ya kuwezesha mkakati Kwa miaka mitano.
 
Unadhani taarifa haziwekwi wazi kwa bahati mbaya? hivyo ndivyo vimetego vyenyewe. wewe hebu jiulize Malaysia katika mpango wao wa BFR vipaumbele vyao viko wazi and measurable, sisi tuliowaiga katika mpango wetu wa BRN vipaumbele vyetu vyote havipimiki.
SASA NIAMBIE USIRI HUU NI WANINI? KWA MANUFAA YA NANI?
Kama ilivyokuwa katika maisha bora kwa kila mtanzania, baada ya kuingia madarakani wakabadilika eti huwezi kupata maisha kwa kukaa vijiweni!! hivi wakulima, wauguzi, walimu nk wamekaa vijiweni? na je maisha bora wameyaona?

VIMITEGO VYA NINI KAMA KWELI TUNA DHAMIRA NZURI?!
 
BRN wanayoiita haitaonyesha matunda yoyote
mi naipenda sana nchi yangu Mungu azidi kuibariki Tanzania maana hawa wakurugenzi wetu wakikaa hakuna posho office lazima watakaa waseme kuwa kuna mradi wana anzisha hivyo watenge pesa za research,semina makorokoro kibao so long watapata chao cha juu.
Hakuna kitu kama big results now neither big results kesho kama tutazidi kufumbia macho uovu wa serekali na watendaji wake
 
Unadhani taarifa haziwekwi wazi kwa bahati mbaya? hivyo ndivyo vimetego vyenyewe. wewe hebu jiulize Malaysia katika mpango wao wa BFR vipaumbele vyao viko wazi and measurable, sisi tuliowaiga katika mpango wetu wa BRN vipaumbele vyetu vyote havipimiki.
SASA NIAMBIE USIRI HUU NI WANINI? KWA MANUFAA YA NANI?
Kama ilivyokuwa katika maisha bora kwa kila mtanzania, baada ya kuingia madarakani wakabadilika eti huwezi kupata maisha kwa kukaa vijiweni!! hivi wakulima, wauguzi, walimu nk wamekaa vijiweni? na je maisha bora wameyaona?

VIMITEGO VYA NINI KAMA KWELI TUNA DHAMIRA NZURI?!

Vinapimika Na realistic kabisa, ttzo la kutoiweka wazi Ndo nashindwa kulipatia jibu,
 
Vinapimika Na realistic kabisa, ttzo la kutoiweka wazi Ndo nashindwa kulipatia jibu,

Tatizo hapa ni uelewa tu, hebu niambie elimu utaipimaje? labda wangesema elimu itagharamiwa na serikali, hivyo isipogharamia tutafahamu au kuboresha ufaulu wa wanafunzi, ufaulu usipoongezeka tutajuwa.
HEBU TUACHENI LONGOLONGO, HUU MPANGO NI WA KIULAGHAI
 
Angalia hivi vimetego Malaysia kipaumbele chao katika elimu ni kuboresha matokeo ya wanafunzi, kitu ambacho kinapimika, lakini sisi kipaumbele chetu katika elimu tumesema tu elimu haiko wazi, ifanye nini? Wenzetu wanaongelea kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha chini (which is measurable), sisi tunasema tu kilimo au mobilization of resources, without point out where or to whom, for what purpose. yaani kuna vimitego vingi vya kijinga. NA KAMA KAWAIDA WAJINGA NDIO WALIWAO, watoto wa mjini wanasema imekula kwetu.
ki ukweli mi nakubaliana na wewe, mipango yetu haipimiki (non-measurable) big result ktk elimu ni ipi, je kuongeza ufaulu wa wanafunzi na ktk level zipi na kwa kiwango gani(minimum) kwa muda upi.Lakini pia tatizo naliona ktk masomo yalioteuliwa kwa kufanyia big result ni manne tu (basic mathematics,biology,kiswahili na english) labda kwa vile ni common kwa kila shule na kila mwanafunzi lazima ayasome. lakini ukija ktk uhalisia watawala wanakwambia ni masomo yote wakati semina inatolewa ktk hayo manne tu, ni mkanganyiko mwingine.Kwa aliyesema kuwa kila wizara iliweka vipaumbele vyake, inawezekana lakini havikuwa analyzed hasa kwa watendaji au watekelezaji i.e walimu kwa maana ya sekta ya elimu.Wakati wa ufunguzi wa semina za brn mbozi na momba bosi mmoja alisema serikali imetoa baadhi ya maeneo ya kuzingatia ila wao kama mkoa wa mbeya tunatekeleza ktk maeneo yote ya elimu.how?
BRN inahitaji maelezo ya ziada kwa watendaji na wananchi kwa ujumla otherwise itakuwa comedy
 
Back
Top Bottom