Mafisadi na hatma ya Tanzania

Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,034
1,003
Ina huzunisha sana kama sio kutia huruma sana kwa nchi yetu ya Tanzania kuwa hapa tulipo. Kwani tuna mali asilia nyingi sana lakini ni masikini wa kutupwa kuliko.

Hii ni kwa sababu ya watu wa chache tu wasiopungua kama 40 hivi wenyenye nguvu za kuwatala watu zaidi ya milioni 40 kwa mabavu,wizi,ufisadi,uzandiki,ufirauni,uzushi,husuda,kiburi,choyo na mengine mengi ambayo yanaifanya Tanzania kuwa maskini wa kutupwa eti wakiguswa kwa kuhojiwa wana sera yao kuwa tunahatarisha amani!

Mi binafsi siioni hiyo amani uchwara kama ipo wakati mali zetu zinaisha na nchi inakuwa taabani kwa kikundi cha miungu mtu wachache na familia zao kulimbikiza fedha na mali nyingi kama vile dowans na mengine mengi yanayo leta kechefuchefu.

Huku watanzania wakifa kwa matatizo lukuki kwa sababu ya kukosekana huduma za msingi lakini huku wakiimba "amani na utulivu" jamani wazungu walivyo sema hili ni bara la giza ni kweli kabisa. Kwani inaonyesha kuwa akili zetu nyeusi kwani hazifikirii.

Hivyo kujinusuru kwetu ni kulitoa tabaka la miungu mtu kwa mabavu na vita kali hapa hakuna kulemba wala kupamba huu ni ujinga mkuu kikundi kidogo kutawala watu wengi kwa mabavu.

"UGHAIBUNI WANAULIZWA KWANINI NYIE NI MASKINI WAKATI MNA MALI ASILI? JIBU LAO HATA MIMI SITUJUI" Hivi tutafika kweli?
 
Rekebisha kichwa cha THREAD hapo juu na isomeke; Tanzania na hatima ya MAFISADI.

Mafisadi ni wakupita tena ni wa kuondolewa ila Tanzania ni wa milele. Hivyo si jukumu la Mafisadi kutolea dira hatima ya taifa letu bali ni taifa letu (wewe, mimi na wale) kutolea jibu mafisadi, familia zao na washirika wao.

Sawa?
 
Kwa hali inavyoendelea sasa kuhusiana na uchumi kiujumla kuwa mbovu,hali ya maisha kwa wananchi kuwa duni propaganda za serikali kujaribu kuficha ukweli italiangamiza hili taifa, kwa yaliyotokea kwa Mr. Ulimboka ni kiidhhiirisho kuwa tanzania hakuna haki,hakuna amani, leo nimesikia katibu wao nae kaanza kupigiwa sim na watu asio wajua kesho tutasikia mwenyekiti wa waalimu kafanyiwa kama Olimboka, serikali inasema udaktari,uuguzi n.k ni kazi za kujitolea. Swali ni je unaweza kulazimishwa kujitolea?

Leo hii madaktari wanaweza wakatoa notisi ya saa 24 ya kuacha kazi ya serikali maana ujuzi wao uko kichwani na sio hospital na waalimu hivyo hivyo, je hatma ya taifa itakuwaje?
 
Tumshukuru mwenyezi mungu kwa uzima na baraka anazotujalia hadi kuiona hii leo.

Ni jukumu la kila mtanzania kukaa na kutafakari kuhusu hatma ya nchi hii. Ilipoanza kongo baadhi ya watanzania walisahau ile methali mwenzako akianza kunyolewa .... Na leo hii ndiyo vurugu zimeshaanza kusini mwa nch yetu,mda si mrefu utasikia kanda ya ziwa(north mara).mererani n.k

swali la kujiuliza ni je viongozi tuliowapa wajibu wa kutetea wananchi na mali zetu wanafanya nini hadi raia kufikia hali waliyonayo, je ni hatua gani waliyochukua ili kuifanya nchi hii ikarudia katika hali yake ya amani iliyokuwanayo.je safari za rais zinafaida gani kwa nchi ilihali wananchi wanauana.

Kaa chini tafakari na ombea nchi yako
 
Tumshukuru mwenyezi mungu kwa uzima na baraka anaotujalia hadi kuiona hii leo.
Ni jukumu la kila mtanzania kukaa na kutafakari kuhusu hatma ya nchi hii. Ilipoanza kongo baadhi ya watanzania walisahau ile methali mwenzako akianza kunyolewa .... Na leo hii ndiyo vurugu zimeshaanza kusini mwetu,mda si mrefu utasikia kanda ya ziwa(north mara).mererzni n.k
swali la kujiuliza ni je viongozi tuliowapa wajibu wa kutetea wananchi na mali zetu wanafanya nini hadi raia kufikia hali waliyonayo, 4.NI LAZMA KILA MTU AFANYE KAZI KWA BIDII NA ATIMIZE KILA WAJIBU UNAOMKABILI YEYE KAMA RAIA WA TZ
 
Back
Top Bottom