Mafisadi CCM wageuka mbogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi CCM wageuka mbogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 8, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Mafisadi CCM wageuka mbogo


  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 01 June 2011

  [​IMG][​IMG] Lowassa, Rostam wamkoromea Msekwa


  [​IMG]


  SASA ni piga ni kupige ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wanakataa kujiuzulu, MwanaHALISI limeelezwa.


  Taarifa zinasema walipoitwa mbele ya viongozi wakuu wa chama hicho – makamu mwenyekiti Pius Msekwa na katibu mkuu, Wilson Mukama - wanaoitwa na CCM kuwa “watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini,” walishikilia msimamo kuwa hawawezi kujiuzulu kwa kuwa hawana hatia.

  Wanaotakiwa kujiuzulu na viongozi wakuu wa CCM ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge. Mkutano wa kuwashawishi wajiuzulu, ulifanyika Alhamisi na Ijumaa wiki iliyopita katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba, Dar es Salaam.
  Taarifa zinasema katika mkutano huo, Msekwa na Mukama waliomba Lowasa ajiuzulu ili kukiokoa chama hicho, lakini yeye alipinga kwa hoja kuwa hana hatia.

  MwanaHALISI lilipowasiliana na Msekwa kutaka kufahamu kilichojadiliwa katika mkutano wake na viongozi hao, haraka alisema, “…Umetoa wapi habari hizo?”

  Alipoelewa ni vyanzo vya ndani ya chama na serikali, Msekwa alisema, “Hayo ni mambo ya ndani ya chama. Hatuwezi kuyaleta magazetini.”
  Lowassa alipoulizwa juu ya kuwapo kwa kikao hicho, alisema ni kweli wamekutana. Hata hivyo, alisema hawezi kueleza walichojadili kwenye vyombo vya habari.

  Rostam hakupatikana kueleza upande wake. Hata hivyo, MwanaHALISI limeelezwa na mtoa taarifa wake kuwa mbunge huyo wa Ingunga alitoka kwenye ukumbi wa mkutano akiwa amenuna na kuvurumisha “maneno makali.”

  Anasema Rostam alitoka pale akiwa amenuna na kusema yeye hana hatia yoyote na kwa hiyo hastahili kushambuliwa. Amesema yote yanayotokea sasa yanatokana na uadui wa siasa za urais wa mwaka 2005 na ule wa 2015.


  Hili linatokea wakati uongozi wa juu wa chama hicho ukishindwa kukabidhi barua ya kuwataka watuhumiwa hao wajiuzulu.
  Kuchelewa kwa utekelezaji wa maazimio ya kuwawajibisha Lowassa, Rostam na Chenge kumezaa majungu na umbeya. Hivi sasa taarifa zinasema, Mukama anadaiwa kugoma kuandika barua ya kuwataka watuhumiwa hao kuachia nafasi zao za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) wanazozishikilia.

  Baada ya Mukama kugoma kuandika barua hizo kwa hoja kuwa kilichoamuriwa na NEC hakifahamu kwa kuwa alikuwa hajateuliwa, ndipo Nape Nnauye, katibu wa itikadi na uenezi alipoandika barua hizo na kuzipeleka kwa Msekwa.

  Naye Msekwa alizipokea barua na kuzirekebisha. Akazirejesha kwa Nape ili azipeleke kwa Mukama kuzisaini. Mukama akagoma. Zikapelekwa kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, ambaye taarifa zinasema, “amezifungia kabatini.”

  Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kikao hicho, Lowassa alifika Lumumba saa nne asubuhi. Mazungumzo kati yake, Msekwa na Mukama inakadiriwa yalichukua takribani saa moja.

  Katika mazungumzo hayo, Msekwa ananukuliwa akimweleza Lowassa “unatakiwa ujiuzulu nyadhifa zako za uongozi katika chama ili kutekeleza maagizo ya NEC na falsafa ya chama ya kujivua gamba.”

  Akijibu hoja hiyo, mtoa taarifa anasema Lowassa alijibu, “Kuhusu Richmond (kampuni feki ya kufua umeme wa dahurula), ukweli unafahamika…Katika hili, mimi sina makosa. Rais anafahamu hilo na kila mmoja anajua hivyo.”

  Anasema Lowassa alisema kama kuwajibika kwa makosa yaliyotokana na Richmond tayari amefanya hivyo kwa niaba ya chama chake na serikali pale alipoamua kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu.
  Anasema mbali na kueleza hilo, Lowassa alisikika akisema, “nilikutana na Rais Kikwete. Aliyonieleza si haya.”

  Alisema Rais Kikwete alimweleza kuwa hakuna maazimio yoyote ya NEC yaliyomtaka kujiuzulu. Akahoji, “Sasa nimwamini nani, ninyi mnaotaka nijiuzulu au rais aliyesema hakuna azimio kama hilo?”

  Habari zinasema mara baada ya Lowassa kuwaeleza viongozi wake msimamo juu ya mazungumzo yake na Kikwete, ndipo Msekwa aliposikika akisema, “Lowassa acha mbio za urais.”

  Naye Lowassa hakumkawiza Msekwa. Alijibu, “Lini nimetangaza kugombea urais? Lakini hata kama ninataka kufanya hivyo, ni haramu kugombea nafasi hiyo? Je, kuna mliowaandaa?”

  Ni kauli hiyo ya Lowassa, iliyomshutua Msekwa na kusema, “Hapana. Hapana. Hakuna tuliyemuandaa…Haya mambo ya urais yatatuvuruga.”
  Akihitimisha hoja zake kabla ya kumalizika kwa mkutano huo, mtoa taarifa anasema Lowassa alikitaka chama chake kuisaidia serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi, badala ya kufanyia kazi kile alichoita, “majungu ya wanasiasa.”

  Naye Chenge taarifa zinasema aliwaambia viongozi aliokutana nao kuwa yeye si fisadi na hafahamu maana ya ufisadi. Akataka kama tuhuma wanazomtuhumu wanaweza kuzithibitisha wamfikishe mahakamani ili aweze kujitetea. Hakuna maelezo ya ziada.


  Hata hivyo, watu waliokaribu na kiongozi huyo wanasema, Chenge amejipanga kuhakisha kwamba hang’oki katika kiti chake cha NEC; ikibidi kuondolewa kwa nguvu ametishia kuondoka CCM na kujiunga na upinzani.

  Kwa upande wa Rostam Aziz, taarifa zinasema alitakiwa kujiuzulu ujumbe wa NEC kwa tuhuma za kuingiza nchini kampuni feki ya Richmond na baadaye Dowans.

  Mtoa taarifa anasema, mara baada ya kuelezwa tuhuma hizo, Rostam alihoji, “Haya ni maamuzi ya NEC?” Naye Msekwa akajibu, “NEC imetaka chama kijivue gamba kuanzia ngazi ya taifa hadi chini kwa kuondoa watu wote wanaotuhumiwa ufisadi.”

  Habari zinasema, katika mazungumzo kati ya viongozi hao na Rostam, hakuna mahali popote ambapo Msekwa na Mukama walitaja ushiriki wa mbunge huyo wa Igunga, katika wizi wa fedha za umma kupitia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

  Kampuni ya Kagoda ni miongoni mwa makampuni 22 yaliyothibitika kuchota mabilioni ya shilingi kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Gazeti hili limeshindwa kufahamu mara moja kilichosababisha Msekwa na wenzake kushindwa kumweleza Rostam ushiriki wake katika Kagoda. Hata hivyo, kwa zaidi ya miaka minne sasa, CCM imekuwa ikituhumiwa kunufaika na fedha za EPA hasa Sh. 40 bilioni zilizoibwa na Kagoda.

  Wakati suala hilo likichukua sura hiyo, taarifa zilizofikia gazeti hili zinasema baadhi ya vigogo wa chama hicho wamepanga kupeleka hoja katika vikao vijavyo vya (CC) na (NEC) kushinikiza kufukuzwa ndani ya chama hicho wanaoitwa, “wasaliti ndani ya chama.”

  Wanaopangiwa mkakati wa kufukuzwa ni spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta na mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe wanaotuhumiwa kuanzisha Chama cha Jamii (CCJ) wakati wakiwa bado wanachama na viongozi wa CCM.

  Wengine ni Nape Nnauye, Victor Mwambalaswa na Daniel Porokwa.
  Habari kutoka ndani ya CCM zinawanukuu makada mawili; rais mstaafu, na mjumbe mmoja wa NEC wakitaka chama chao kuwafukuza waasisi wa CCJ kwa kukosa uaminifu.

  MwanaHALISI limeelezwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CCJ, Dickson Ng’hily kwamba Sitta na Mwakyembe waliokuwa waanzilishi wa chama hicho, walimkatiza masomo yake nchini Afrika Kusini ili kusaidia kupatikana usajili wa chama hicho.

  Ng’hily ambaye mahojiano yake yatachapishwa kikamilifu katika toleo lijalo amesema, aliyemwingiza yeye CCJ ni Sitta na Dk. Mwakyembe na anasikitishwa na hatua ya viongozi hao kutaka kuficha ukweli.

  “Hawa watu ndio waanzilishi hasa wa CCJ. Mimi na Makonda tulipewa jukumu la kutafuta usajili wa chama. Lakini naona wenzangu wameamua kuficha ukweli kwa maslahi binafsi. Hii si sahihi,” ameeleza.

  Ng’hily anaonyesha nyaraka za muhtasari wa vikao walivyoshiriki viongozi wakuu wa CHADEMA, John Mnyika, Anthony Komu na Tundu Lissu kuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki katika majadiliano ya kuunganisha nguvu kati ya CCJ ya Sitta na CHADEMA.

  “Tulikubaliana kama CCJ itakosa usajili, basi mheshimiwa Sitta atagombvea urais kupitia CHADEMA. Lakini kama tutafanikiwa kusajili chama chetu, basi Sitta angegombea urais kupitia CCJ na CHADEMA wangetuunga mkono,” anaeleza Ng’hily.

  Kuibuka kwa Ng’hily kuelezea ushiriki wa Sitta na Dk. Mwakyembe katika kuanzisha na kusimamia usajili wa CCJ kumekuja wiki tatu baada ya Fred Mpendazoe kumtaja Nape Nnauye kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa kwanza wa CCJ.

  Mpendazoe aliuambia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Njombe kuwa yeye, Sitta na Mwakyembe ndio walianzisha CCJ; bali yeye alitangulia kutoka CCM ili kurahisisha usajili wa chama hicho. Wenzake walikuwa wamfuate baadaye.
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kikwete, Msekwa na Mukama hawawezi kusaini hizo barua kwa sababu hawakuziandika na kamwe hawangethubutu kuziandika - sababu ziko wazi kabisa kwa wenye macho. Mtu pekee anayeweza kuzisaini ni huyo Kijana Nape ambaye ujinga, upofu na ukurupukaji wake wa kitoto ulimsukuma aziandike bila kujiuliza kwa nini hilo jukumu aachiwe yeye. Sasa kama kweli anajiamini, badala ya kukaa na kulala akiiota Chadema, azisaini na awape watuhumiwa halafu ashuhudie CCM ya wenyewe ilivyo na mshikamano, thubutu !
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mag3 kinachomsukuma Nape ni hasira. Unakumbuka ni EL aliyemwekea zengwe UVCCM na mtifuano ulikuwa mkali Nape akitaka mali za UVCCM ambazo mmoja wa wadhamini ni EL ziwekwe hadharani ikiwa ni pamoja na mikataba tata ya jengo la UVCCM, EL akitaka kumuondoa ili awekwe kijana wao kuimarisha safu ya NEC na CC kuelekea 2015.Ilikuwa kidogo tu NEC ya mafisadi imtimue lakini unyeti wa suala lazima ukaonyesha yangeibuka yasiyoandikika magazetini
  Sasa Nape amekamata mpini anahangaika na 'watu wake'.
  Mambo mazito kama haya Mwenyekiti huwa ndiye mwamuzi, nadhani tutajifunza kuwa urais ni taasisi yenye majukumu mazito na mengine yakiigusa hata familia, 'u-best' matatizo yake ndiyo haya.
   
 4. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Duh!'

  William @ NYC, USA.
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hadi hizo siku tisini zifike tutaona sarakasi za kutosha si yetu macho na masikio. Nape akumbuke zege likikorogwa halirudi kuwa cement sijui atarudishaje maneno yake maana ka inavyoonekana hamna kujivua gamba wala kuosha gamba
   
 6. K

  Kipopori Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Moto wamewasha wenyewe,acha uwaunguze,hakuna wa kunyoosha kidole ,asiye na dhambi awe wa kwanza kutupa jiwe,mafisadi yana speed kuliko bacelona Nape naMUKAMA hamuwawezi, waachieni chadema muone moto wake,viva cdm.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  JK need to come out on matters like these, haya ndiyo mambo tunahitaji tuone waandishi wa ikulu wakitoa matamko.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh!!!! Kazi ya kulivua gamba ilivyokuwa ngumu. Kikwete anaihofia, Mukama kaigomea, Nape ndiyo hivyo tena na Msekwa wamemkoromea! sasa tusubiri tuone nini kitachofuata katika kutafuta mbabe ndani ya chama cha magamba katika jitihada zake za kulivua gamba.
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Dah huko juu kweli kunafutuka...moto unawaka!!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huu mchezo unahitaji umakini wa hali ya juu, inakoelekea mambo yatakuwa mazito zaidi.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm Makao makuu ni muunganiko wa genge la viongozi wenye akili nyepesi sana, hawana huthubutu. Hawaaminiki, wanalolisema silo wanalomaanisha.
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,852
  Likes Received: 11,973
  Trophy Points: 280
  Tulimwambia Nape hizo mbio hazitafika popote ndani ya CCM ona sasa yameanza kumgeuka Katibu mwenezi mzima anakuwa kwenye hatihati ya kunyang'anywa kadi ni aibu kwake na kwa waliomchagua.
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Maendeleo hayaji bila msuguwano - kwamba ili kitu kiwe na changes lazima kuwe na struggle ndani yake. Kubomoka kwa CCM ndio nafuu ya watanzania waliowengi yaani mabadiliko ya kweli kuendea maisha bora kwa kila mtanzania! Mfano kusipokuwa na struggle ndani ya yai la kuku - shell kuendelea kuwa ngumu na kifaranga kutokukuwa tusingekula kuku, lakini kifaranga anakuwa shell inapinga kupanuka lakini mwisho wa siku shell inapasuka na kifaranga kutoka na baadaye tunafaidi supu ya kuku na nyama yake.
   
 14. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukweli EL ameshika mpini na wao makali, hamshangai kwanini anamwambia Msekwa nilijiuzulu uwaziri mkuu kwaajili ya kunusuru chama na serikali, yeye kama waziri mkuu asingejiuzulu kwasababu ya makamu mwenyekiti au kiongozi mwingine yeyote wa ccm ila mwenyekiti na pia asingejiuzulu kwasababu ya waziri wa nishati au mwingine yeyote ila mkuu wa kaya - kwa utashi wangu hiyo ndio tafsiri sahihi sasa hawa jamaa wa ikulu sijui wamelisoma hili gazeti? Kama ndivyo tunasubiri walitolee ufafanuzi au kukanusha
   
 15. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  NAPE HANA UBAVU WA KUWAONDOA rachel KWA YEYE NI MTU MDOGO SANA KISIASA,NA MAFIRADI WANA NGUVU KUBWA SANA,MWENYE UWEZO NI swaiba WAO MWENYEKITI,JE ATADHUBUTU KUWAONDOA?NA MWENYEKITI KUWAONDOA MAFISADI NI SAWA NA KUKATA TAWI ULILOKALIA NAYE ataanguka!!
   
 16. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapa Nape anakabiliwa na tatizo la ugumu wa kulamba matapishi aliyokwisha yatapika kisha tamka na kutaja siku 90 za magamba kujivua pia kisha taja majina ya magamba yenyewe alifanya hivyo kwa kukurupuka bila kutafakari nini tafauti ya CCM na Mafisadi alipokuja kugundua kua CCM na ufisadi ni kitu kimoja ndani ya CCM na tofauti katika majukwaa sasa amegundua kua ubavu wake mdogo.Kwani kama ni ufisadi asilimia kubwa ya viongozi ni mafisadi na wamefaidika na wanaendelea kufaidika kwa njia moja au nyingine na ufisadi na wengine wameingia madarakani kwa pesa au msaada wa mafisadi KUJIVUA KWA KWELI MAGAMBA KWA CCM KUKIVUNJA CHAMA NA KUKIUNDA UPYA VINGINEVYO NI MAZINGAOMBWE NA USANII .MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 17. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  I am totally lost. Yani CDM ninayoiamini ilikuwa tayari kumsimamisha au kum-support fisadi Sitta kugombea urais! Sitta huyuhuyu anayetuhumiwa na Dr Slaa leo kwa ufisadi sawa na nduguye Rostam? Sitta huyuhuyu aliyemshambulia sana Dr Slaa kwenye sera ya kutoa elimu bure? CDM mnahitaji umakini zaidi ili tuendelee kuwaamini.
   
 18. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  MAPACHA WATATU SI MCHEZO, WANAITAJI MTU MAKINI SANA KTK MAHOJIANO, NADHANI WAMEAMUA SASA KUWA NA MSIMAMO MMOJA. Kazi ipo!
   
 19. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  siku tisini zinakwisha keshokutwa june 10,let us keep in waiting
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nahisi Mzee Msekwa anatumika kufunika kombe maana sijaelewa anafanya nini kwenye front line politics za siku hizi, hasa baada ya kukitumbukiza hiki chama kikongwe kwenye mfumo wa majungu na fitna. Wanakuharibia sifa Mzee wangu ungana na wenzako, Msuya, Warioba, Malecela,Salim Ahmed Salim. Achana na watu wa mipasho.
   
Loading...