Mafisadi CCM lazima wavue gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi CCM lazima wavue gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Nov 7, 2011.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

  Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

  “Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

  “Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo,” alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

  Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

  Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

  Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

  Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

  Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

  Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi ana kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

  Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.

  Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.

  Website Rasmi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM
  My take:- Mh. MUKAMA anayakumbuka haya ? kikao kipo karibu sasa basi tutekeleze hili kwa heshima ya chama
   
 2. IGUDUNG'WA

  IGUDUNG'WA JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 1,964
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  sitta na nape lazima wavue gamba
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,437
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Not again
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,752
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hakuna jipya
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hali iliyopo nadhani Arusha kwenye uchaguzi wa madiwani hawataruhusiwa kukanyaga kama walivyo pigwa stop Igunga
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,749
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160
  Hii chama isiisumbue nchi. Watu wasilazimishe kutawala wakati hawana uwezo tena. Tafadhali tunaomba mpumzike ili nchi iweze songa mbele. Maugomvi yenu yamedumaza uchumi,biashara,siasa na jamii yote ya watanzania.
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  yaah, hakuna jipya ktk hili ila tunajaribu kuwakumbusha ahadi zao kama chama tawala ukichukulia maanani kuwa kikao ndiyo kipo mlangoni ili basi wakumbuke UZITO wa kauli walizo zitoa ili wazitekeleze kwa vitendo otherwise they are perished
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  CDM ndiyo kiboko yenu hawalopoki hivyo ila wanafanya maamuzi na kuyatangaza
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,643
  Likes Received: 2,558
  Trophy Points: 280
  Kikao cha ccm hichoooooooo!
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,623
  Likes Received: 375
  Trophy Points: 180
  vueni gamba fasta. Nalog off
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,056
  Trophy Points: 280
  CCM inatafuta huruma ya Chadema. Kweli CCM mambo yamewaendea mrama
   
 12. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,741
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Gamba halivuliki bila mwenyekigoda kujivua gamba kwanza. Yeye ndo fisadi nambali wani, inakuwaje anataka kuwaengua wenzie yeye abaki?
   
 13. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 931
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi bado kuna wahitimu wa vyuo vikuu bado ni wana CCM?
   
 14. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Wapo sana tu, wakati wengine wanajenga taifa wao busy kujenga matumbo.
   
 15. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wapo wengi sana
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mukama, tafadhali usijisumbue kurudia rudia kauli hii. Wenye akili wameshaeleqwa na wanafahamu ni nini kinafanyika. Ni vema ukautumia muda wako kufanya mambo mengine
   
 17. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Anasemaje na wale wanaohusika na kuzikatizia pesa zilizorudishwa na Wezi wa EPA na kuchotwa na Mafisadi wengine kama Simon groups ambamo ndani yake tunajua kuwa yumo mtoto wa "Kigogo Mkuu"?
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na wale waliopewa makanga, kofia fulana vikofia na ubwabwa je? Halafu walipewa na nani? Nyie mna mpango mzima wa kuua CCM ili mkimbilie CCJ. Tutapata wapi pilau mkiwafukuza mafisadi?
   
 19. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 60
  This song isn't cute anymore! Kwani hakuna single nyingine? You people are just playing with our minds ninashauri porojo hizi ziwezinajadiliwa kwanye vikao vyenu vya ndani huku nje watu wamechoshwa na ngonjera zenu! Mwaka mzima imekuwa gamba, gamba,gamba hao wanaovuliwa gamba wenyewe mlishawaambia au ndio mnataka wakajisomee taarifa hizi kwenye media? Shame. Ukishaamua, chukua hatua!
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,838
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  usihof mkuu zitabakia kofia,vilemba kanga na tshirt
   
Loading...