Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, habari iwe kwenu.
Rais Magufuli yupo Chato ambako ametembelea kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais. Akiwa Chato, Rais Magufuli pamoja na mambo mengine amechangamana na ndugu, jamaa na marafiki akiwemo rafiki wake wa karibu, Raila Odinga ambapo wametumia nafasi hiyo kubadilishana na kupanuana mawazo.
Ziara ya Raila huko Chato hakika imewashtua wengi ikiwemo Serikali ya Kenya. Ikumbukwe kuwa Raila anamtembelea Rais Magufuli katika kipindi ambacho Serikali ya Kenya inafanya juhudi kubwa kuishawishi Uganda isitishe mpango wake wa kushirikiana na Tanzania kujenga bomba la Mafuta kutoka Ziwa Albert hadi Bandari ya Tanga juhudi ambazo hazijazaa matunda.
Aidha, Mpaka sasa CHADEMA hawajafanikiwa kujua sababu za Rais kwenda kupumzika Chato katika kipindi ambacho utumbuaji wa majipu umeshika kasi na bado hajamaliza kuunda Serikali yake ambapo hajafanya uteuzi wa nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, wakurugenzi wa Halmashauri nk. Wapo wanaobeza uamuzi huo wa Rais kwenda kusalimia kwao Chato huku wakihoji ikiwa Rais anaitendea haki kauli mbiu yake ya Hapa Kazi tu.
Kinachowashangaza zaidi CHADEMA na mawakala wao ni kasi ya Polisi na TAKUKURU katika kutekeleza majukumu yao. Katika kipindi cha Rais kuwa nje ya Ikulu, TAKUKURU wamefanya maamuzi mazito ya kumfikisha mahakamani aliyekuwa Kamishna wa TRA na wenzake ambapo mpaka sasa wapo rumande. Pia TAKUKURU wamewafikisha mahakamani wabunge kadhaa wa CCM na wengine wapo njiani kwa tuhuma za ufisadi. Ikumbukwe pia kuwa Rais akiwa Chato ametangaza kupunguza mishahara ya watendaji wakuu wa serikali na mashirika ya umma ambao wanalipwa mishahara mikubwa ya hadi milioni 40 ambapo amesema kuwa ukomo wa mishahara utakuwa milioni 15 tu.
Mpaka sasa Rais Magufuli kila analofanya Rais linampa credit na kumpandisha chati. Wapinzani wanaumia sana kuona hivyo. Fimbo pekee wanayoendelea kuishikilia ni sakata la MCC ambalo hata hivyo linaonekana kupungua nguvu kutokana na wananchi wengi kusisitiza kuwa Tanzania ifike mahala tuachane na misaada bali tusimame kwa miguu yetu.