Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kama vile ilivyo kwenye uhusiano wa DART na Daladala ambapo mpaka leo hii bado Daladala zinaendelea kuhudumia sambasamba na DART ambapo zilipaswa zikome siku ambayo DART ilianza kazi rasmi ni sawa kabisa na tatizo la Mafao ambapo Mfanyakazi hukatwa kila mwisho wa Mwezi, hapa pia kama vile DART Serikali ilipaswa itoe huu uamuzi wa kuzuia watu kuchukuwa mafao yao tangu siku ya kwanza Mafao yanaanzishwa TZ lkn hawakufanya hivyo na miaka yote wamekuwa wakiruhusu mtu kuchukuwa mafao yake wkt wowote atakapo wakati hakuna nchi Duniani inayofanya hivi, Mafao siku zote hulipwa pindi muda wa kustaafu kisheria unapofika na kuna sababu ya Msingi kabisa kuwa hivyo!
Lakini kwa kuwa sisi ni watu dhaifu na hili utaliona kila mahali kwenye jamii yetu hata kwenye familia zetu hatuwezi kutatua hata matatizo madogo tu, mtu akigombana na Mke wake inachukuwa Wazazi ktk kijijini kuja kusuluhisha jambo dogo tu wao wenyewe hawawezi!
Na hili linatugharimu sana hatuwezi kuchukuwa maamuzi ya maana na muhimu ingawaje wkt mwingine tunajua kabisa kwamba huko mbele kama tusipochukuwa uamuzi sasa itakuja kutugharimu lkn bado tunalisogeza tatizo mbele, kwa mfano bomoa bomoa haikupaswa kusimama kwani siku moja ni lazima tuje kubomoa nyumba tu, sasa nina uhakika kwa kuwa Daladala hazijaondolewa jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo itakavyokuwa ngumu kuwaondoa kwa maana watu watazoea na kupinga Daladala kuondolewa hivyo mradi kuwa umekufa rasmi, kwa maana lengo la DART ni kuondoa Daladala na kuboresha usafiri kama vile Serikali inavyopata shida sasa leo na Mafao wanavyotaka kufanya ni sawa lkn walililea hili tatizo muda mrefu na watu wameshazoea kuchukuwa hela zao sasa ukiwaambia leo hii unasitisha watagoma, ni kwa nini hili halikufanyika wakati Mifuko inaanza?
Nina uhakika tulijua kwamba hivi ndivyo inavyopswa kuwa kwa maana siyo sisi tuliogundua huu mfumo na Dunia nzima ni hivyo kwamba fedha hulipwa pindi mtu anapofikisha umri wa kustaafu, hili lingetupunguzia matatizo leo hii!
Ni kwa nini sisi kama jamii hatuwezi kutatua matatizo?