Mafanikio yanaweza kubadili mtazamo wamtu

Mafanikio yanaweza kubadili mtazamo wamtu

belionea

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
1,053
Reaction score
923
Maranyingi mafanikio yanaweza kubadili mtazamo wamtu. Mwanaume akiwa amefanikiwa, ana mali na ana uwezo anaweza kumtazama mwanamke kama bidhaa, kama kitu na sio mtu.

Hii inatokea sana kwa wanaume ambao wanatabia ya kujiandaa kikamilifu kimaisha kabla hawajaoa, atahakikisha ananyumba, anagari, anakazi nzuri, ana viwanja, kilakitu kwake kimekaa sawa kasoro mke tu, then anaanza kumtafuta mke sio kama mtu mwenye nafasi muhimu kwenye moyo wake bali kama kitu kilichobaki ambacho bado hana. Inasaidia sana na inaumuhimu wa pekee kuanza pamoja, kuchuma pamoja, kutoa jasho pamoja, kuyaona na kuyashiriki mapito yote pamoja.

Labda hii itawasaidia wale akinadada ambao husubiri mwanaume ambaye anakila kitu kasoro mwanamke tu, wao hujiingiza kwashangwe kubwa wakidhani wamepata mchongo kumbe mchongoma, siku mbili tatu zikipita mwanaume anaanza kuheshimu mali yake kuliko uwepo wako halafu unaanza kulalamika wakati ulilijua hilo fika.

Open your eyes and see
 
Back
Top Bottom