MAFANIKIO YAKO..

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
Mwanamama ,Natalie Wynne Pace katika kitabu chake cha ,Put Your Money Where Your Heart Is: Investment Strategies for Lifetime Wealth from a #1 Wall Street Stock Picker,katika ukurasa wa 25 anasema,

''Moja kati ya kitu muhimu katika uwekezaji ,ni kuwekeza pesa katika kitu unachokipenda na kukijua kwa undani,na kutizama wazo lako kwa njia ya fikra na si kutizama wazo kwa macho,''.

Millard Afrael Ayo ,ni moja kati ya watangazaji bora wanao nivutia nchini Tanzania sababu ya uwezo wake wa kutangaza ,radio na ubunifu wake bila kuiga style ya mtangazaji yeyote yule kama wafanyavyo watangazaji wengi wanao chipukia.

Millard Afrael Ayo kwa sasa ana umri wa miaka 30 , moja kati ya vijana ambao wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na kuwa Role Model wa vijana wote wanaohitaji kujiajili ,pamoja na vijana walio ajiriwa .

Millard Ayo ameamua kuwekeza pesa katika vitu anavyo vipenda na kutizama wazo lake la ukwekezaji kwa njia wa fikra na kumfanya aweze kustawi na kuwa bora kila siku zinavyozidi kwenda.

Millard Ayo ,kwa kila mwezi anaingiza kiasi cha $10,000 kupitia blog yake ya millardayo.com ,ambayo kwa mwezi inatembelewa na watu zaidi ya 100,000 .kwa muijibu wa mtandao wa
.http://wikipaedia.comofficialwebsite.com/2017/01/millard-ayo-bio.html

Internet television au online television yake inayoitwa Ayo TV,ni moja ya ubunifu mzuri na wenye tija ambao vijana wengine ,tunatakiwa kujifunza kutoka kwake ,na kuanza kutumia mitandao ya jamii kama mrija wa kutuingizia pesa na badala yake kuachana na kasumba ya kupost picture za starehe,pombe na kuonyesha nguo na makalio.

Darasa-Serikali inatakiwa kutambua mchango wa vijana wenye mawazo chanya ya uwekezaji,na kuwapa mikopo kwa kuweka vigezo na masharti yenye tija ili kuongeza nafasi za vijana kujiajiri kupitia mawazo yao ya biashara.

Vijana-Ifikie wakati tutengeneze utamaduni wa kuzima social media kila ifikapo saa 4 usiku kwa kijana yeyote mwenye njaa na kiu ya mafanikio ,na kuanza kuandika mawazo ya biashara na kuyasajili ,ili kuanza kujiajili na kuuza mawazo yetu kwa watu wenye uhitaji.

Mipango huaribika kwa kukosa,shauri,lakini kwa washauri wengi,hufaulu,tuwekeze nguvu na akili kwenye maarifa na kujifunza kuitawala mitandao ya jamii na kuepukana na kuwa watumwa wa anasa,mitandao ya jamii na kuwa na addiction ya ngono.

Naandika post nyepesi zisizo na tija ila zinaweza kukusaidia ,chukua mazuri yangu na mabaya niachie mimi.Libraries were full of ideas–perhaps the most dangerous and powerful of all weapons.[HASHTAG]#MillardAyo[/HASHTAG]
 
Somo zur sana ila
Uslolijua n kwamba vjana
Wengi kinacho watatiza n
Capital na hata akipata

Hyo pesa kusave n ngumu
Coz weng wanaipeleka kwenye bata/starehe
 
Back
Top Bottom