Mafanikio yako ni mabadiliko kwa wengine

Mafanikio yako ni mabadiliko kwa wengine

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
506
Reaction score
798
Mafanikio yako ni mabadiliko kwa wengine

Kitendo cha kupigania ndoto au malengo yako ni kitendo cha kuthamini kuumbwa kwako kutoka kwa Mungu, kitendo cha ku thamini wazazi wako na jamii kwa ujumla.

Unapofanikiwa kwenye maisha yako hayakunufaishi wewe pekee bali familia yako, wazazi wako na jamii kwa ujumla.

Ndoto au wazo ulionalo kichwani ni Mungu kaweka hivyo anza kuchukua hatua atakama hauna rasilimali(resource) zote.

Mungu kaweka ndoto hiyo kichwani kwako kwa malengo maalumu labda anataka wewe uwe mtu wa kwanza kuwa tajiri katika ukoo wenu na ubadilishe kabisa mtazamo wao.

Au kaona watu wanapata changamoto fulani hivyo wewe umepewa jukumu la kuwa msaada kwa kuleta njia ya kutatua hilo tatizo na kuweza kufanikiwa kupitia hilo wazo.

Chukua hatua unapofanikiwa jua unatengeneza njia kwa wengine kuona kwamba kila kitu kinawezekana ukiamini na kumtegemea Mungu.
 
Back
Top Bottom