Mafanikio ya Muungano wa Serikali mbili

Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
75
1. Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuthamini na kudumisha Muungano wetu ambao ni wa kipekee na kihistoria, uliounganisha nchi mbili zilizokuwa huru za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

2. Muungano huu ni nguzo ya umoja, mshikamano, amani na utulivu wa wananchi wa pande zote mbili.

3. Kutokana na umuhimu huo, Chama kimeendelea kuzielekeza serikali zake kuchukua hatua za kuulinda na kuuenzi Muungano wetu ambao ni adhimu na adimu kwa lengo la kuwawezesha wananchi kufurahia matunda yake.

4. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015-2020), mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongeza fursa za majadiliano ili kuimarisha ushirikiano wa pande zote mbili kwa manufaa ya Watanzania wote.

5. Hatua hizo zimeongeza wigo wa mashirikiano kwa kuongeza nafasi kubwa ya kubadilishana ujuzi, utaalam na uzoefu kupitia mafunzo, masuala ya sera na ushiriki katika masuala ya kimataifa.

6. Tumefanikiwa kufanya vikao vya mara kwa mara vya kisekta katika ushirikiano na kujadili masuala mbalimbali yenye manufaa kwa Muungano kama vile nishati, maji, madini, uchukuzi, utumishi na utawala bora, viwanda na biashara, maliasili na utalii, afya, maendeleo ya jamii, serikali za mitaa, kilimo, habari, utamaduni, sanaa na michezo, ardhi, elimu, fedha na mipango na mazingira.

7. Tumefanikiwa kufanya ziara za kikazi katika taasisi za Muungano na zisizo za Muungano kwa lengo la kujifunza utendaji kazi wa taasisi hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.

8.Tumefanikiwa kuandaa utaratibu maalum wa vikao vya Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ mwaka 2019 vya kushughulikia masuala ya Muungano. Kutokana na utaratibu huu zimeundwa kamati ndogo mbili ambazo ni Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara; na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ili kushughulikia masuala mbalimbali katika maeneo hayo.

9. Tumefanikiwa kufanya marekebisho ya gharama za umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO kwa kufuta kodi ya ongezeko la thamani na malimbikizo ya deni la kodi hiyo lenye thamani ya shilingi bilioni 22.9.

10.Tumefanikiwa kupitisha mwongozo Kuhusu Ushiriki wa SMZ katika masuala mbalimbali ya kimataifa na kikanda kwa lengo la kuongeza nafasi za masomo ya elimu ya juu na mafunzo mengine nje ya nchi na utafutaji wa fedha za misaada na mikopo ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

11. Tumefanikiwa kufikia maridhiano ya masuala mbalimbali yakiwemo utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili; gharama za kushusha mizigo (landing fees); upatikanaji wa fursa za ushiriki katika miradi ya maendeleo ya viwango na ubora wa bidhaa na maendeleo ya wajasiriamali.

12. Tumefanikiwa kuibua, kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali ya Muungano kama vile Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA); Mpango wa Kupanua Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania.

13. Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tanzania Social Action Fund -TASAF); na Mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Kanda ya Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth - SWIOFISH).

14. Tumefanikiwa kusimamia mgawo wa fedha ambapo SMZ imeendelea kupata gawio la asilimia 4.5 ya fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, PAYE, gawio la faida ya Benki Kuu ya Tanzania na fedha za Misaada ya Kibajeti.

15. Tumefanikiwa kupunguza KERO za Muungano, tumeboresha Muungano wetu.

MUUNGANO WETU NDIO UMOJA WETU, TUTAUENZI NA KUULINDA DAIMA.
Chagua CCM, Chagua Muungano!
MenukaJr.
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,364
2,000
Hizi sio faida za Muungano, mbona haya mambo ni kawaida tu hata Tanganyika na Uganda zina ushirikiano huu na amani na upendo, hayo mlioeleza ni mambo ya ushirikiano wa kimataifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom