Maeneo yapi yanafaa kujenga kwa sasa Dar es salaam

Maeneo yapi yanafaa kujenga kwa sasa Dar es salaam

Wacha uongo wewe,
Buyuni ni mbele ya Pugu unapita Chanika!
Buyuni ni kabla ya Chanika mjini japo ni kata hiyo ya chanika, wilaya ya Ilala. Ni mbele kidogo ya njia panda ya Dampo la Kinyamwezi.
 
Nenda Posta pale kuna majengo yanauzwa Tshs 200b - 1000b ununue na kuhamia kabisa, achana na mambo ya kujenga.
 
Nitafute ktk namba 0688000072 nikupeleke maeneo ya Mlamleni Kongowe utapata viwanja kuanzia laki 8,kuna wazaramo wana mashamba ya urithi tayari mm nishachukua

Habari za saa hizi wanajamii forum,
Mwenzenu natafuta eneo la kujenga kibanda changu cha kuishi na familia yangu,naombeni ushauri wapi naweza kupata kiwanja kwa bei nafuu.Pls pia ningependa kujua gharama za kiwanja kwa eneo husika.
 
USHAURI WA BURE.

ukishanunua kiwanja nunua mchanga trip moja ile ya gari ndogo halafu subiri kama wiki ndio uanze kujenga.

Ukiona hakuna mtu aliyekufata na kulalamika umenunua kiwanja chake basi ruhsa kujenga
 
Msaidieni huyu mtu antafuta Kiwanja Dar yani ilala kino, sinza, mwenge, ubungo etc, Mara Buyuni, ooh goba, aah kivule etc hivyo Si vijiji jamani? Kwi! Kwi! Kwi! Ye anataka Dar aisee Kama ni hivyo vijiji nenda tu kibaha ujue uko pwani,
 
Wacha uongo wewe,
Buyuni ni mbele ya Pugu unapita Chanika!
Kama kitu huna uhakika ni bora ukauliza... Unafahamu kuwa maeneo maeneo mengi majina yanajirudia..??? Kwa mfano Kongowe, ipo ya Kibaha na vile vile ipo ya Mbagala.... Sasa kama wewe unaifahamu Buyuni ya pugu, wenzio tunaifahamu Buyuni mbele ya gezaulole. So badala ya kuita ni uwongo, bora ungeuliza...

USHAURI WA BURE.

ukishanunua kiwanja nunua mchanga trip moja ile ya gari ndogo halafu subiri kama wiki ndio uanze kujenga.

Ukiona hakuna mtu aliyekufata na kulalamika umenunua kiwanja chake basi ruhsa kujenga

Maisha yangekuwa rahisi hivi....mbona kila cku ingekuwa ckukuu
 
utakutana na matapeli wengine wamo humuhumu usijelizwa ndugu fanya utafiti wao taratibu taratibu tuna vijisent vyao mkuu hela ngumu.
 
Kama kitu huna uhakika ni bora ukauliza... Unafahamu kuwa maeneo maeneo mengi majina yanajirudia..??? Kwa mfano Kongowe, ipo ya Kibaha na vile vile ipo ya Mbagala.... Sasa kama wewe unaifahamu Buyuni ya pugu, wenzio tunaifahamu Buyuni mbele ya gezaulole. So badala ya kuita ni uwongo, bora ungeuliza...

Noted!!
 
Nunua kiwanja maeneo ya Mbezi kwa Msuguri (Temboni, Msingwa) na Kifuru, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ndugu Oswald Sh. Richard kwa simu namba :
00255784342632 au +255767342632
E-mail : cosiastore@yahoo.fr

1. Kiwanja cha kwanza kipo Mbezi kwa Msuguri, umbali wa kilomita tatu toka barabara ya Morogoro. Kiwanja hiki kipo kando ya barabara ya Msingwa ambayo ni ya changarawe na inapitika. Kina mita 30x40, pia kina nyumba ya vyumba viwili na baraza mbili. Nyumba hii ina umeme. Pia maji yanapatikana mita mia tatu toka kiwanjani. Bei yake ni Tshs. 55 milioni.

2. Kiwanja cha pili kipo Mbezi kwa Msuguri pia. Kuna umbali wa km 2 kutoka barabara ya Morogoro. Barabara ya kuelekea kiwanjani (maeneo ya mtaa wa Temboni) ni ya changarawe na inapitika. Kina ukubwa wa 1350M[SUP]2 [/SUP]
Kimepimwa na hati miliki yake ipo mbioni kutoka. Pia kina uzio wa waya. Bei yake ni Tshs. 60 milioni. Kuna maji umbali wa mita 200 kutoka kiwanjani. Umeme upo.

3. Viwanja vingine vipo eneo la Kinyerezi-Kifuru, umbali wa kilomita 1 toka barabara ya Kinyerezi-Mbezi. Hivi vipo viwanja 14. Vina ukubwa usio sawa.Vipo vya mita 22x25, 20x23, 27x23 na 20x20. Bei zake ni Tshs. 7 millioni kila kimoja. Eneo hili limefikiwa na mradi wa Serikali wa kuwekewa umeme, na wameshaweka nguzo ila bado kuweka nyaya na hatimaye kukamilisha mradi. Maji ya uhakikika kwa sasa ni kama umbali wa kilomita 2.
 
Pata ushauri kote ila Goba ndio habari ya mujini sasa. Ukitaka kwenda kimara powa tu, makongo utokee mwenge powa tu, mwenge upitie mbezi beach powa tu, kwenda bagamoyo powa tu. Muda siyo mrefu barabara inatanuliwa na kuwekwa lami.
 
Habari za saa hizi wanajamii forum,
Mwenzenu natafuta eneo la kujenga kibanda changu cha kuishi na familia yangu,naombeni ushauri wapi naweza kupata kiwanja kwa bei nafuu.Pls pia ningependa kujua gharama za kiwanja kwa eneo husika.
mtoni kijichi ndo mpango mzima.kuna mkondo wa bahari,viwanja vimepimwa pia kuna hewa ya oxygen ya kutosha
 
Pata ushauri kote ila Goba ndio habari ya mujini sasa. Ukitaka kwenda kimara powa tu, makongo utokee mwenge powa tu, mwenge upitie mbezi beach powa tu, kwenda bagamoyo powa tu. Muda siyo mrefu barabara inatanuliwa na kuwekwa lami.

vp nina milion na nusu ctapata kiwanja ndugu?
 
Back
Top Bottom