Maeneo yapi yanafaa kujenga kwa sasa Dar es salaam

Maeneo yapi yanafaa kujenga kwa sasa Dar es salaam

Habari za saa hizi wanajamii forum,
Mwenzenu natafuta eneo la kujenga kibanda changu cha kuishi na familia yangu,naombeni ushauri wapi naweza kupata kiwanja kwa bei nafuu.Pls pia ningependa kujua gharama za kiwanja kwa eneo husika.
Njoo salasala nikuuzie nyumba vyumba vitatu.Ina umeme na maji ya bomba,gari inafika mpaka nyumbani na uwanja sqm 2000,bei 70 milioni.pia kuna kiwanja Wazo kwa mzee Makamba 35*40,bei 25 milioni.
0754 856277.
 
sasa kuna kiwanja nilinunua kama shamba huko maeneo ya kigamboni mwongozo mwaka jana sasa nahofia kufanya any development ya hicho kiwanja,naogopa ule mradi wa kigamboni new city usije ukatupitia na ikala kwangu
 
Kama ulivyoshauriwa na wengine, pembezoni ndio mpango mzima. Utaepukana na kero za kubanana, unajenga kwa nafasi.

Kuna viwanja vilipimwa na serikali miaka ya 2000 maeneo ya Buyuni, njia ya Chanika ulikuwa ni maradi wa viwanaj 20,000 watu wakakimbilia kununua wengine viwanja sita mpaka nane ila kujenga ikawa ngoma. Watu wengine, nikiwamo mimi tumejikongoja na kujenga nyumba na kuhamia kabisa. Sasa kuna watu walionunua viwanja vingi wanauza, unaweza kwenda kwa mtendaji akakupa namba za wauzaji.

Advantage nyingine ya viwanja vya Buyuni ni maji ambayo hayana Chunvi ambayo yanapatikana kwa kuchimba kisima chako maana hakuna Dawasco kule. Kuna watu wameanza kujenga super markets za nguvu na tayari PPF wamekamilisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu 641 ambazo ziko sokoni tayari. Barabara ni lami toka mjini na inaendelea kupanuliwa, umeme upo.

Mkuu Buyuni ni wapi huko? Au ni maeneo karibu na Kinyerezi?
 
Dar ni kubwa sana ingawa ni ndogo kulinganisha na mikoa mingine!
Sasa wewe angalia kulingana na mfuko wako ni wapi utamudu kununua kiwanja na kujenga.

Kuna maeneo hapahapa Dar yako nnje kabisa ya mji lakini bado viwanja vyake ni bei juu mno na vilevile yapo maeneo mazuri tu nnje ya kidogo jiji ambayo bei bado ni nafuu angalau kuanzia 1.5m ambavyo kwa sisi tuanzao maisha huwa vinatufaa.

Ishu ni kuwa mtembezi, jaribu kutokatoka nnje yajiji pande zote utafanikiwa kukutana na maeneo mazuri kwa unafuu wa bei!
 
kigamboni near bamba beach au njiani kuelekea bagamoyo kupitia tegeta.
 
Nenda pale mbelew ya lango la Ikulu alilotumia OBAMA kuna kiwanja kipo wazi na kinauzwa kwa bei poa kabisa. Kaulizie jamaa anayeitwa Salva kama unataka namba yake niPM.

Acha utani rafk angu,jamaa kauliza asaidiwe,kama huna cha kuchangia si ukae kimya?
 
Habari za saa hizi wanajamii forum,
Mwenzenu natafuta eneo la kujenga kibanda changu cha kuishi na familia yangu,naombeni ushauri wapi naweza kupata kiwanja kwa bei nafuu.Pls pia ningependa kujua gharama za kiwanja kwa eneo husika.

nina kiwanja cha title kibada, Ni pm
 
Habari za saa hizi wanajamii forum,
Mwenzenu natafuta eneo la kujenga kibanda changu cha kuishi na familia yangu,naombeni ushauri wapi naweza kupata kiwanja kwa bei nafuu.Pls pia ningependa kujua gharama za kiwanja kwa eneo husika.


Kama ni kibanda tu na siyo nyumba ya maana, basi kajenge Mbagala au Tandale.
 
Acha utani rafk angu,jamaa kauliza asaidiwe,kama huna cha kuchangia si ukae kimya?


Hajakosea kwani siku hizi ikulu wanakesha kina Juma Nature na wabwia unga wengine wa bongo fleva. Nchi haina kiongozi toka 2007, na sitashangaa kama ikulu yenyewe imepangishwa siku hizi.
 
Toangoma ni wapi mkuu?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kwani ujasikia mtu anaulizwa unakaa-twangoma? Basi ndio huko ni njia ya kwenda kigamboni kwa barabara kwa kupitia Mbagala.
 
Mkuu Buyuni ni wapi huko? Au ni maeneo karibu na Kinyerezi?

Hapana Buyuni ni kata ya Chanika. Unapita Gongo la Mboto kama unaenda Kisarawe kisha unapinda kulia ukifika njia panda ya Kigogo Fresh. Unaelelea Chanika. Unaweza ulizia njia inayoelekea kwa Waziri mkuu, au viwanja vya wachina(nyumba za PPF zimejengwa na wachina ndio maana pakaitwa kwa wachina.)
 
Back
Top Bottom