MAENEO NANE YA MTAALA NGAZI YA DARASA

Nov 23, 2018
49
87
MAENEO NANE MUHIMU YA MTAALA NGAZI YA DARASA.

Ulishawahi kuwaza kufanya kazi ya kutunga sera na kufanya maamuzi?. Ipi unadhani ingefaa kuwa sera bora ya elimu katika nchi yako? na vitu gani unadhani ni muhimu kuvizingatia wakati wa kuandaa programu ya mafunzo kwa shule ya msingi?

Mtaala katika maana ya jumla ni mambo yote ambayo mwanafunzi hujifunza shuleni. Katika makala hii nitajadili maeneo nane yanayozingatiwa katika uandaaji wa mtaala rasmi ngazi ya darasa.

Mipango ya Mtaala hufanywa katika ngazi kuu mbili :Ngazi ya serikali Kuu na ngazi ya serikali za Mitaa. Ngazi ya serikali kuu mpango wa mtaala huwa ni wa jumla tu, na hudhihirika kupitia sera mbalimbali zinazohusu elimu na mipango mingine inayochimbuka kutoka, kwenye ilani ya chama tawala. Katika ngazi ya serikali za mitaa majukumu ya mtaala yameshushwa zaidi hadi kwa mwalimu ambaye ndiye huvunjavunja muhtasari kupanga nini kifundishwe kwanza, kwa namna gani na kwa wakati gani.

1.JAMII
Jamii inayosimamiwa na serikali kuu na serikali za mitaa ina malengo mahususi juu ya elimu itolewayo kwakuzingatia mambo matatu; mahitaji yake, malengo yake na utamaduni wake. Serikali kuu ina sababu kwanini inatumia bajeti kubwa kugharamia elimu kwa kuandaa mipango ya elimu kazini na kuwalipa mishahara watumishi wa idara. Serikali za mitaa nazo kwa upande mwingine zina sababu kwanini inajenga madarasa na kuajiri walimu wapya ili kuboresha elimu. Wazazi nao wanasababu kwanini wanawapeleka watoto wao shuleni. Mwalimu anatakiwa ayazingatie mahitaji yote hayo wakati anaandaa Azimio la kazi na andalio la somo.

2.MAUDHUI
katika kila somo kuna umahiri na stadi mahususi ambazo mwanafunzi yabidi apate hivyo ni wajibu wa mwalimu kuhakikisha hilo linafanikiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza mtaala.

3.MALENGO YA UJIFUNZAJI
Malengo makuu (kwenye maazimio ya kazi) na malengo mahususi(kwenye maandalio ya masomo) sharti yazingatie nini mwanafunzi anaweza kutenda au kuwaza au kuhisi.

4.MTOTO
Kipaumbele kikuu cha mtaala ni mtoto. Mwalimu lazima awatambue vema wanafunzi wake kuzingatia mahitaji yao, historia ya makuzi yao, shauku na ndoto walizonazo kwenye maisha, uwezo wao, uzoefu walionao pamoja na motisha.

5.VITENDO VYA UJIFUNZAJI
Hivi ni vitendo vinavyofanywa na watoto katika mchakato wa ujifunzaji. Hapa mwalimu anatakiwa ajipange vema kwani si kila kitendo kinafaa kwa wakati wote. Mwalimu atumie muda mwingi kuandaa vitendo kwa kuzingatia maeneo matatu tuliyoyajadili :maudhui, malengo yake na mtoto anayemfundisha darasani.

6.NYENZO
Wakati mwalimu anaandaa somo ni wajibu wake kuamua aina gani ya vifaa vitumiwe na mwanafunzi ili kumsaidia ajifunze vema. Nyenzo hapa ni kama vile vitabu vya kiada, magazeti, ramani na wakati mwingine watu ni rasilimali muhimu kutumika kama nyenzo.

7.MPANGO
Kwa mwalimu mipango ni ada. Katika eneo hili mwalimu afikirie muda atakaotumia pamoja na mbinu ambazo zitazingatia maeneo tuliyoyajadili. Kwa mwalimu wa watoto wadogo kama mimi mpango pia uhusishe namna ya kudhibiti kelele na fujo nyingine zinazoweza kumtoa mtoto kwenye lengo.

8.TATHMINI
Tathmini inapaswa kuwa katika mawanda mawili.
Kwanza, mwalimu apange namna bora atakavyowapima wanafunzi wake kubaini ni kwa kiwango gani wamejifunza.
Pili, mwalimu ajitathmini mwenyewe ni kwakiwango gani ameweza kufundisha na ikiwa mbinu alizotumia zinafaa au zibadilishwe.

Hayo ndiyo maeneo nane muhimu ya mtaala katika ngazi ya darasa.

Mchoro unapatikana Kituo cha Walimu Liwale.

Mwl A. Raphael Longino
S/M Ngorongopa
Liwale-Lindi.
 
Nime-like ,ila sikusoma yote, nikipata muda nitarudi hapa
 
Back
Top Bottom