Maeneo hatari kwa mkoa wa Dar

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Kufuatia kuteuliwa kwa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hebu tumsaidie kumtajia maeneo hatari kwa Mkoa huu ambapo kwa namna fulani sisi Wananchi tumeyashindwa pamoja na juhudi zetu za ulinzi shirikishi.

Kutaja huko kutasaidia kwa kiasi fulani kumpa pakuanzia hasa ukizingatia hali ya usalama ndani ya jiji hili si ya kuridhisha.

Kuna maeneo hapa Dar unaweza ukaibiwa mchana kweupe tena na watoto wadogo tu wenye silaha za jadi kama vile mapanga, marungu na nondo. Karibuni tuyataje ili aweze kuyafahamu ukizingatia Mh. Nchemba ni mwanachama wa Jf. Karibuni...
 
Hakuna eneo hatari....


Kuna watu hatari katika eneo fulani..

Vipi kama watu hatari wakiondolewa eneo husika? Kichwa cha habari kitakuwaje?


Tafakari na wewe.... Anza wewe kuwa mwema, Jamii yote itabadilika taratibu
 
Darajani pale kuelekea Mwenge ukitokea Ubungo walinipora simu.

Mwigulu kaanzie pale wanirudishie simu yangu. Ilikuwa aina ya Nokia X2 na ilikuwa na vocha ya voda shilingi 1300.
jamani humu mna vituko
 
Back
Top Bottom