Maendeleo ya jamii ya wanarumu

Maendeleo ya jamii ya wanarumu

MKWELI12

Member
Joined
Oct 15, 2013
Posts
9
Reaction score
1
Narumu ni eneo linalopakana na Lyamungo,Machame na Kibosho. Na ni sehemu ya Wilaya ya hai. Ni vema kutambua kuwa jamii yoyote hapa duniani ipo katiaka mchakato wa maendeleo usiokoma. Ni ufinyu wa mawazo kuzungumzia maendeleo ya jamii Fulani kwa miaka 30 iliyopita kuwa ndiyo muonekanao wa sasa Kielimu,Kiafya, na Rasilimali. Narumu ya sasa kama jamii zingine imepiga hatua kubwa kimaendeleo na ni eneo wakazi wake wanaweza kujitambulisha bila chembe ya uoga uliowahi kuwepo zamani. Ikiwa kuna mchagia hoja hii atembelee kwanza jamii hii na kujionea kabla ya kuingia kwenye mjadala
 
Ulitaka kusema nini hasa mkuu....??

Rejea mjadala wa siku za nyuma na uchangiaji wake hapo chini ndiyo chanzo cha mimi kufunguka! Ni baada ya kubaini kuwa kuna watu wako nyuma ya habari........



1- When i met these little boys at a village called Narumu in Kibosho (Kilimanjaro Region) and asked them about who they wanna be in their future;the first one told me he wanna be a doctor,second one police,third one Engineer and fourth one a Teacher. But when am trying to look to the environments which they are living,studying and even socializing i get a doubt if they will be able to achieve their DREAMS and have a GOOD LIFE which they deserve. CORRUPTION,POOR EDUCATION,SELFISHINESS,etc............WE NEED TO CHANGE.



2- Tarafa ya Kibosho ni kubwa ila hili eneo la Narumu lipo a little bit behind other areas of Kibosho.
Ujumbe wako ni muhimu sana kwa watawala kuuzingatia,



3- NARUMU jamani si kibosho hii iko Wilaya ya Hai ila kuna mchanganyiko wa lafudhi ya Kimachame na Kikibosho. Kijiji cha Tela ndicho kimepakana na Lyamungo Sinde na hapo utakuta lafudhi ya lugha inabadilika ghafla. Kwa sisi tulizaliwa na kusomea maeneo ya vijiji vya jirani na Narumu tunaona mabadiliko makubwa sana kwani eneo la Narumu lililokuwa nyuma kielimu na kimaendeleo linapiga hatua kubwa sana kutokana na kuwa na wasomi wengi.

Hii picha pamoja na kuwa ni ya Narumu lakini bado Narumu ninayoifahamu sasa iko juu sana na kama kuna watoto wanamna hiyo ni wachache sana kulinganisha na kule Mwamapuli mpanda, Kaoze, Sakalilo,Zombana na mgazini(Ruvuma), sindeni, Bungu(Korogwe), maeneo ya Rugu kule Karagwe n.k

Hata hivyo mkuu naamini Jamii Forum ni ya members wastaarabu. Hebu fafanua usemi wako kuwa Aliyezoea UTUMWA Uhuru huwa mzigo
 
Back
Top Bottom