Maendeleo ya CHADEMA Njombe

Sio contacts za mtu yeyote kwa sababu tunazo hata za wanaCCM wa huko. Tunataka za watu ambao ni committed kwa mabadiliko. Tutashukuru ukitusaidia za wanaharakati wa Ludewa kwa sababu za Makete zimeanza kuingia japo bado tunazihitaji zaidi. Asante sana Mkuu
 
Wakuu tunashukuru kwa kutuunga mkono. Tunaomba muendelee kutusaidia kuwapata watu wa Ludewa hata makete milango bado iko wazi
 
Gerrard,
Mko juu kaka. Natamani ningelikuwepo huko kuwasaidia bahati mbaya niko nje ya nchi hii.
Nitarudi karibuni nami niwashe moto huko kwetu ingawa Chadema kwetu huko wako juu sana, natamani bendera zote za kijani zing'olewe kila mahali. Na hili linawezekana. Mafisadi wanaelekea mwisho wao. Msisahau kuwapatia nakala za Katiba wasije kuogopeshwa. Wasome na waone jinsi viongozi wetu wanavyoisigina katiba. Ni udikiteta tupu.
 
Saaafi. Nice move hadi public ijue kuwa JF ni jukwaa la kujadili maendeleo ya Chadema.
 

Kuhusiana na uimarishaji wa chama cha CHADEMA, nilikwishafanya mawasiliano na viongozi wa kitaifa juu ya nia yangu kushirikiana na watu wote wenye mapenzi mema kwa wilaya ya Ludewa, ambao wanahitaji sana mabadiliko lakini wamekosa uongozi thabiti. Strategy ya mwanzo imekuwa kufungua ofisi za Chama katika kila kata, mengine tutaongea zaidi tutakapowasiliana kwa njia za simu na vikao. Mimi binafsi nitafurahi sana kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja ili kukamilisha lengo hili.

Sasa hivi nipo nje ya nchi lakini mara nikirejea katikati ya Februari, tutawasiliana. Nipo nanyi kwa hali zote. Tusiwe walalmishi bali watendaji, lazima tufanye kitu sasa kwaajili ya faida ya vizazi vijavyo. Taifa letu limekuwa la aibu kubwa kwa umaskini, siyo kwa sababu linahitaji kuwa hivyo bali kwa vile tumekosa uongozi, dhamira na mipango iliyo thabiti.

Nashauri kwa watu wote wanaouchukia umaskini, wanaochukia dhuluma, na wanaopenda wao wenyewe na watoto wasije kuishi kama tunavyoishi sisi leo, kila mmoja kuona atachangia namna gani kuleta mabadiliko, hasa katika majimbo yale ambayo CHADEMA imekosa wabunge na madiwani. Nia iwe ni kuwafikia wananchi wote wa Tanzania kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 

Laiti ningekuwa huko nyumbani ningewasha moto wilaya yote ya Kilosa ili wakwetu waamke maana bado wapo wanaodhani kuvaa mabiramu (mabango) ya Nambari wani ni ujiko!
 
Hongera sana tunataka iringa yote iwe kama kilimanjaro soon, mimi naanzisha harakati jimbo la kilolo prof msolla kwaheli,vijana wachukue nafasi.
 
Cdm iangalie uwezekano wa kuwa na mwakilishi kwa kuanzia kila kata ya tanzania hii. Vijana wanaoishi mijini wa kila kata hapa nchini waangalie uwezekano wa kuchangia chama katika kata husika ,tuwe na kijana mwenye elimu ya kati asiye mwoga atusaidie kueneza chama. Mimi niko tayari kuanza na kata ya bomalangombe kilolo iringa mwezi wa tatu, makao makuu iangalie uwezekano wa suala hili bila kujali sehemu gani kwenye washabiki ,ni kata zote nchi nzima tunataka kwanza tupape wawakilishi wa kata kwa nchi nzima baadae wawakilishi katika kila kijiji. Ukombozi wa taifa hili umewadia.
 
Kazi nzuri sana, hasa kama inaanza wakati huu.....4 years to come mtakuwa mbali sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…