Maendeleo na Uchaguzi Mtaani

Joined
Feb 13, 2009
Messages
68
Likes
0
Points
0

urassa

Member
Joined Feb 13, 2009
68 0 0
Nisaidieni wanajf, ninaambiwa namwonea wivu Diwani kwa kuwa anatembea na mwanamke fulani ambaye niliwahi kuhusishwa naye kimapenzi mwaka 1999 japo haikuwa kweli.

Diwani wetu hajawahi kutembelea mitaa ya kwetu hata siku moja tangu achaguliwe miaka 5 iliyopita, kwa hiyo shughuli za kijamii za kutengeneza barabara na daraja tumekuwa tunajitahidi sisi wenyewe.

Juzi mkazi mmoja kaleta makaravati 2 na kuyaweka kwa gharama zake, Wiki 3 baadaye Diwani kajitokeza na makaravati 3 lakini madogo kuliko yaliyokuwepo huku akisingizia hayo mawili yaliyowekwa yanatafutwa na polisi kwa hiyo akayachukuwa hayo makubwa na hatujui yalipelekwa wapi japo aliyeyaleta alikuwa tayari kukubali kwamba yeye ndiye mwenye nayo na yuko tayari kueleza alikoyapata.

Mimi nikajitokeza kumpinga Diwani kwamba alichokifanya siyo kitendo cha ungwana kwani anawavunja moyo wapigakura wake ambao wameamua kujitolea pasipo hamasisho lake.

Mimi nikasema kwa mamluki wake ni dhambi hata kwa mwenyenzi mungu kumpa tena kura huyo Diwani endapo atagombea.

Hapo ndiyo nikajibiwa nina chuki binafsi na Diwani, baadaye nikaambiwa namwonea wivu Diwani kwa sababu anatembea na mwanamke ambaye nilihusishwa kutembea naye miaka hiyo, kulikoni?
 

Forum statistics

Threads 1,190,287
Members 451,082
Posts 27,666,623