Maendeleo haya ni ya miaka mitano tu

jijiletublog

Member
Jul 23, 2020
31
74
KUHUSU ELIMU

SAT, imepanua wigo kwa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari ambapo mpaka sasa imetumika Sh trilioni 1.01. Kutoka shule za msingi 16,899 hapo awali hadi 17,804 na shule za sekondari 4,708 hadi 5,330. Kumefanyika ukarabati wa shule kongwe za sekondari 77 kati ya shule 89, na kujenga mabweni 253 na nyumba 227 za maabara, vifaa vya maabara 2,956 vimetolewa na kupunguza kiasi kikubwa cha uhaba wa madawati kutoka milioni 3.24 hapo awali hadi milioni 8.95 sasa.

Ukarabati wa vyuo vya walimu 18, kujenga vyuo vipya na kutoa kompyuta kwenye vyuo vyote 35 vya walimu lengo ikiwa ni kuimarisha ufundishaji wa Tehama katika shule mbalimbali zilizopo Tanzania. Ongezeko la vyuo vya Veta kutoka 672 hadi 712, ukarabati wa vifaa na miundombinu vya kufundishia 54 ndani ya vyuo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Bajeti ya elimu ya juu imeongezeka kutoka Sh bilioni 348.7 hadi Sh bilioni 450. Ongezeko hili limewapa nafasi wahitimu wengi wa kidato cha sita kuomba mkopo na kupata nafasi ya kujiendeleza na elmu ya chou kikuu. Idiadi ya wananfunzi wa vyuo vikuu wanaojiunga na mwaka wa kwanza imeongezeka kutoka 65,000 hadi 87,813, wenye kupata mikopo nao wameongezeka kutoka 98,300 hadi 130,000.

uandkishaji wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka milioni moja hadi milioni 1.6 hivi sasa. Idadi wanafunzi kidato cha kwanza hadi nne pia imeongezeka kutoka milioni 1.648 hadi milioni 2.185. hii yote ni shukrani kwa sera ya elimu bure kwani inampatia mtoto wa kitanzania haki yake ya msingi ya kupata elimu.

Idadi ya wanafunzi wa Veta nayo imeongezeka kutoka 117000 hadi 226767, vyuo vya maendeleo ya wananchi imeongezeka 69,300 hadi 9,736,. Kwa taarifa hii hatukosei kusema kazi kubwa imefanyika katika sekta ya elimu, kwani idadi ya watanzania walioelimika sasa ni kubwa.

KUHUSU AFYA
Serikali ya awamu ya tano imefanya mengi mazuri katika kuboresha sekta ya afya kuanzia upatikanaji wa huduma za kibingwa na vifaa tiba, upatikanaji wa rasilimali watu katika sekta ya afya na uboreshaji wa miundo mbinu ya Vituo vya kutoa huduma za Afya. Katika hili, tunayo mifano michache tu ya kumchagua tena raisi wetu;

Rais Magufuli alisema SAT imefanikiwa kujenga vituo vya afya 1,769 zikiwemo zahanati 1,198, vituo vya afya 487, hospitali za wilaya 71, hospitali za mikoa 10. Miongoni mwa hospitali hizo za mikoa ni pamoja na hospitali ya Mkoa wa Mara ambayo ni Mwalimu Julius Nyerere Memorial ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 1970.

Hospitali za rufaa za kanda tatu zimekwisha jengwa, waajiri watumishi wapya 14,479 tayari wamo makaziniikiwemo madaktari 1,000 walioajiriwa hivi karibuni, hii imeongeza idadi ya watumishi wa afya kutoka watumishi 8,6152 hadi 163,100. SAT, chini ya uongozi wa raisi JPM imeimarisha pia vifaa tiba na dawa ambapo bajeti ni kutoka shilingi bilioni 31 hadi shilingi bilioni 270 hivi sasa, SAT pia imenunua na kusambaza magari ya kubebea wagonjwa 117 ili kusaidia wagonjwa mahututi waweze kufikishwa haraka katika vituo vya afya kupata matibabu na huduma za kiafya.

“Vilevile tumefanikisha kusomesha madaktari bingwa 301 ambapo wamewezesha kuimarisha matibabu ya kibingwa ya moyo, masikio, kansa na ubongo. Vilevile idadi ya rufaa kwenda nje ya nchi nayo imepungua kwa asilimia 95,wagonjwa kutoka mataifa jirani wamekuja kutibiwa nchini, hii ni kwa sababu wataalamu tunao hapahapa kwetu.

“Kuboreshwa kwa huduma hizi za afya kumesaidia idadi ya kina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya kuongezeka kutoka asmili 64 haid 83 hivi sasa, vifo vya watoto wachanga vimepungua sana kutoka wastani wa vifo 25 hadi saba kwa kila vizazi hai 1,000,. Raisi magufuli pamoja na serikali yake anastahili pongezi katika hili.

Ameboresha huduma za kibingwa MOI na kutumia bilioni 6.91 kufanya upasuaji wa kibingwa kwa mafanikio makubwa na kuokoa zaidi ya Bilioni 12 (Kama zingefanyika nje ingetugharimu bilioni 18.34) hii inaokana na uwepo wa vifaa vya kisasa na wataalamu wakutosha.
Amekamilisha vyumba vya tiba mtandao (Telemedicine ) MOI na hospitali nyingine teule na kuziunganisha na hospitali za rufaa za Mikoa na Wilaya ili kurahisisha usomaji wa picha za X-Ray na CT Scan na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi.

Ametoa zaidi ya Bilioni 4.64 kusimika mitambo ya kisasa ya tiba ya mfumo wa umeme wa moyo pale #JKCI na kuhudumia zaidi ya wagonjwa 1,410 ukilinganisha na wagonjwa 246 (2015). Amefanikiwa kuanzisha huduma ya upandikizaji figo (Kidney Transplant) hospitali ya Benjamini mkapa Dodoma na kupandikiza figo wagonjwa 12 mpaka Sasa. Hapa tumeokoa bilioni 1.14 (Milioni 22-25 kwa mgonjwa ndani na milioni 100- 120 kwa mgonjwa Kama tungefanya nje).

Ameboresha taasisi ya saratani Ocean road kwa kuweka vifaa vya kisasa na kuongeza idadi wa wataalamu bingwa wa Onkolojia kufika 30 toka 13 (2015) na kupunguza idadi ya wagonjwa wa rufaa kwenda nje toka 164 (2015/2016) hadi 2 (2019/2020).

Ameongeza Vituo vya dawa za kupunguza makali ya HIV bila malipo toka 5,555 (2015) hadi 6,529 (2019).

Ameboresha huduma za uchunguzi wa TB kwa kuongeza mashine za kisasa za kupima TB (GeneXpert) toka 65 (2015) hadi 239 (2020) ambazo hutoa matokeo ndani ya masaa mawili tu. (Halmashauri 113 kati ya 184 zimefungwa vifaa hivi), hivyo tumepunguza vifo vinavyotokana na TB toka 30,000 (2015) hadi 2,200 (2020). Amefanikiwa kuongeza idadi ya vituo vya kutoa huduma ya afya toka 7,113 (2015) hadi 8,446 (2020) (Vituo binafsi na vya Umma).

Amepunguza maambukizi ya Malaria toka 14.8% (2015) hadi 7.3% (2020) na vifo vinavyotokana na Malaria toka 6,311(2015) hadi 2079 (2020).

Ameanzisha huduma ya upandikizaji wa uloto (Bone marrow) katika hospitali ya Mloganzila hapa tutaokoa mabilioni ya pesa kwa huduma hii kupatikana Tanzania. Muhimbili: Amefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 56 toka mwaka 2018 kwa kutumia bilioni 1.68. Kama wangepelekwa nje ya Tanzania tungetumia 6.72 bilioni.

Ameokoa 1.92 bilioni kwa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 9 toka 2017. Tumetumia bilioni 1.08 badala ya Bilioni 3 nje ya Nchi. (Mgonjwa mmoja milioni 36 ndani ya Nchi na milioni 100 nje ya Nchi). Kutokana na kuboresha huduma za matibabu ya TB na kuongeza Vituo vya huduma na tiba toka 662 (2016) hadi 1,201(2020) Amepunguza maambukizi ya TB toka 306/100,000 (2015) hadi 253/100,000(2020).

Kutokana na kuboresha huduma za Kibingwa na elimu kwa umma tumepunguza idadi ya watoto wanaaougua ukoma kwa 44% toka 98 (2015) hadi 53 (2019).

Amefanikiwa kufunga mashine za kisasa za X- Ray Za kidigitali katika hospitali za rufaa 12 nchi Nzima.

Amefanikiwa kuaminiwa kununua dawa za nchi 16 za SADC Jambo ambalo limeleta unafuu wa bei ya dawa toka kwa wazarishaji na kuokoa kiasi kikubwa. JPM alipewa fursa hii baada kufanikiwa kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini).

Ameboresha na kuongeza Vituo vya upatikanaji wa damu salama na kuongeza idadi ya chupa za damu salama toka 104,632 (2015/2016) hadi 227,677 (2020). Amepunguza idadi ya wagonjwa wa rufaa kwenda ya nchi toka 385 (2015) mpaka 53 (2020) na kuokoa kiasi kikubwa Cha pesa.

Ameongeza idadi ya Watanzania wanaopima na kupata ushauri wa VVU bila malipo mjini na vijijini toka 6,800,000 (2015) hadi 12,392,268 (2019) ongezeko la 82.2%. Ameongeza Vituo vya kupima VVU bure toka 5,600 (2015) hadi 6,397 (201 b9).

KUHUSU MAJI
Tanzania imebarikiwa kuwa moja ya nchi kati ya nchi nyingi zenye hazina kubwa ya maji, ambapo inakadiriwa kuwepo kwa hazina ya mita za ujazo wa maji wa zaidi ya Bilioni 150, hii ni sawa na wastani wa mita za ujazo wa 2250 kwa kila mtu kwa mwaka. Hiyo pekee haitoshi, ni kwamba Tanzania ni nchi ya maziwa Makuu matatu, ikiwa ni ziwa la Viktoria, ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa. Hii ina maana kuwa ukiachana na hazina ya maji iliyopo kwenye vyanzo vya ndani, pia tumebarikiwa kuwa vyanzo vya nje vya maji katika mziwa yetu Makuu. Kutokana na rekodi hiyo ni dhahiri kuwa Tanzania inahitaji chama makini na viongozi makini katika kuhakikisha kuwa watu wote wanayapata Maji hayo. SAT itabaki kuwa chaguo sahihi katika utekelezaji wa sera za maji.

Kwa kutambua hazina za maji tulizonazo nchni, serikali ya awamu ya tano, kwa maelekezo ya ilani ya CCM ya 2015/2020 chini ya uongozi wa Rais Dkt. John P. Magufuli, iliamua kuja na miradi mikubwa yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa maji lakini pia kuondoa kero zilizokuwa zikiwapata wanawake wakati wa kutafuta maji. Wote tunafahamu uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo mengi nchini, na kwamba ndio uliopelekea madhara ya unyanyasaji kwa wanawake na kwa wasichana ambapo ilichangia katika kusababisha mimba za utotoni kwa mabinti wanafunzi n.k.

SAT, ilionelea kheri kuongeza bajeti ya fedha katika serikali kupitia wizara ya maji na umwagiliaji katika kushughulika na matatizo yatokanayo na ukosefu wa maji, tangu Rais Dkt. John P. Magufuli aingie madarakani ameweza kupandisha bajeti ya wizara kufikia wastani wa zaidi ya shilingi Bilioni 500. Hii ina maana kwamba serikali imeazimia kwa dhati kabisa kuondoa kero ya maji kwa watanzania.

Maendeleo ya sekta ya maji yapo wazi na kwamba yamejidhihirisha yenyewe kwa watanzania. Na ukweli huu ni kwa sababu hakuna namna ambayo binadamu anaweza kutengana na maji. Binadamu ni Maji! Serikali ya CCM imeweza kupandisha bajeti ambayo imeweza kutekeleza jumla ya miradi ya maji 1423 mijini pamoja na vijiji ambapo miradi 1268 ni ya vijijini na miradi 155 ni ya mijini. Hata hivyo serikali pia imeendelea na kutekeleza miradi mikubwa ya kusambaza maji katika vijiji zaidi ya 200 na miji zaidi ya 70, kutika katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa, ambapo ili serikali iweze kutekeleza miradi hiyo imekuwa ikikarabati na kujenga miundombinu ya maji pamoja na kuchimba visima na kujenga mabwawa katika maeneo ambapo hazina ya maji ya chini inaweza ikavunwa kwa matumizi ya binadamu. Na kwa hakika miradi yote hiyo inatekelezwa kwa fedha za watanzania wenyewe.

SAT, kwa miaka Mitano imeazimia kuondoa kero ya maji kwa wananchi kwa kuwaletea maji Safi, salama na yenye kutosheleza lakini pia kuwezesha kukua kwa sekta ya viwanda nchi ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira. Katika kuhakikisha jambo hilo linatimia, Tanzania imeweza kupata mkopo nafuu kutoka serikali ya India wa shilingi trilioni 1.2 ili kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji katika miji zaidi ya 20 hapa nchini. Na mkopo huo utalipwa na sisi watanzania wenyewe. Lakini lengo ni kuharakisha idadi ya watanzania wanaopata huduma ya maji ya uhakika na yaliyosalama inaongezeka.

Ndani ya miaka Mitano ya kwanza ya Rais Dkt. John P. Magufuli , ameweza kupandisha idadi ya watanzania waliokuwa wakipata huduma ya maji Safi na salama kutoka 47% mwaka 2015 kwa upande wa vijijini mpaka 75% mwaka huu 2020: na kutoka 74% na kufikia 85% kwa upande wa mjini. Hakika haya ni mafanikio makubwa sana. Kwa makadirio hayo CCM imebakiwa na 25% ya idadi ya watu vijijini ili kuondoa kero ya maji kabisa kabisa na 15% idadi ya watu mijini... Na hiyo itawezekana ikiwa tuirudisha tena ilani ya CCM ya 2020-2025 na Rais Dkt. JOHN P. MAGUFULI kwa miaka Mitano mengine ili kuweza kuielekeza serikali kuiendeleza miradi hiyo kwa miaka Mitano mpaka mwaka 2025.

MAWASILIANO
SAT imeimarisha pia huduma za mawasiliano kutoka asilimia 79 hadi kufikia asilimia 94, idadi ya watumiaji wa huduma za simu na data imeongezeka maradufu. Na tunafahamu umuhimu wa mawasiliano kwa binadamu, kwani yanatusaidia kufikisha taarifa mbalimbali za binafsi, kimaendeleo, kiuchumi, kiafya, kielimu na hata kisiasa.

BARABARA
Barabara zenye urefu kwa kilomita 3,500 zimejengwa hivyo kuifanya nchi yetu kuwa na kilomita 13,000 za barabara za lami. Kwa mara ya kwanza pia tumejenga barabara za juu na hizi zimeanza kujengwa Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari, ambao ni kero kwa raia wengi kwani huwachelewesha wengi katika shughuli zao za kimaendeleo. Hakikisha tunaiunganisha mikoa kwa barabara za lami, na kwa usaidizi wa SAT, hili ni jambo linalowezekana kabisa.
 
Sasa kama wameboresha na kujenga vyuo vya ualimu lakini hao walimu waliopatikana hawaajiriwi inamaana gani? Kwangu haingii akilini boratu vyuo vingebadilishwa na kua shule za msingi ili watanzania wajue kusoma na kuandika kisha waingie kwenye siasa. Hapo ndio wasioelewa watakapoelewa
 
Maamuzi ni kuchagua Magufuli maana 28 October ni Magufuli day
Siyo kwa kukosa nyongeza kwa miaka mitano hadi nimeikimbia kazi ya serikali nimeenda kwa sector binafsi. Siyo kwa huo mpango wa kikokotooo hapa sitampa kura yangu kwa kweli
 
Kuna hajagani ya kuwasomesha walimu,kuboresha majengo na kujenga vyuo vipya kisha walimu hao wasiajiriwe? Naona kama wanapoteza muda wawatu na kodi zetu
 
Back
Top Bottom