Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,566
- 4,013
Maelfu ya waandamanaji wameingia katika mitaa ya Lebanon jana hii, ikiwa ni siku ya tatu ya maandamano ya kuipinga serikali.
Hasira ya waandamanji hao inawalenga wanasiasa wanaowalaumiwa kuuporomosha uchumi.
Kuanzia kusini hadi mashariki na kaskazini mwa nchi hiyo, waandamanaji walizuia barabara, kuchoma moto matairi na kukusanyika katika mitaa licha ya wapiganaji wa harakati za kundi la Amal, kutoka madhehebu ya Waislamu wa Shia wakijitokeza na silaha nzito kuwatisha.
Katika eneo la kati Beirut mwamko ulikuwa mkali na waandamanaji wa rika zote walikuwa wakipeperusha bendera na kuimba kutaka mapinduzi.
Awali hapo jana Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri alitoa masaa 72 kwa washirika wake katika serikali kukubaliana suluhusho la mgogoro wa kiuchumi.