Maelezo kuhusu gharama za huduma "service charge " za Tanesco

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MAELEZO KUHUSU GHARAMA ZA HUDUMA "SERVICE CHARGE"

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu gharama za huduma "service charge" kama ifuatavyo.
1. Gharama za huduma zipo kwa mujibu wa Sheria ya Bunge na si maamuzi ya Tanesco kupanga viwango bali mdhibiti ambaye ni EWURA.
MAELEZO: TANESCO anapoomba kupandisha bei ya umeme EWURA; bei ya unit moja inayotolewa na EWURA haijumlishi Gharama ya Huduma.

2. Nini maana ya Gharama za Huduma na Umuhimu wake. Gharama za Huduma ni gharama ambazo mteja analipa ili inapotokea Tanesco wanakuja mtaani kwenu kubadilisha nguzo iliyooza, kubadilisha waya uliokatika kwenye line ya mteja, kubadilisha mita yako ambayo ni mbovu, kukata matawi ya miti mtaani kwenu, kubadilisha transfoma iliyoibiwa mafuta au kuungua nk gharama hizo zifidiwe na michango hiyo ya "service charges" Ijulikane kwamba mfano waya, mita na nguzo ambazo mteja Ulilipia wakati unaingiziwa umeme kama zikiharibika, TANESCO wanakuja kukubadilishia bure. Je tufute "service charge" alafu nguzo ikianguka au mita kuharibika au ukitupigia emergency kuja nyumbani au mtaani kwako kutoa huduma tukucharge upya?

VIWANGO VYA "SERVICE CHARGE "
Wateja wote ambao hawazidishi unit 75 (D1) kwa mwezi hawalipi service charge. Na umeme wanauziwa TZS 100 kwa unit moja (Bila kodi). Ila ukizidisha unit. Kila unit utauziwa TZS 350.
Wateja wanaozidi unit 75 lakini hawavuki unit 7500 kwa mwezi (T1) wanalipa service charge ya TZS 5,520 na unit moja wanauziwa TZS 298 (Bila kodi). T2 na T3, ni kwa ajili ya wafanyabiashara, mahoteli, viwanda, migodi na wengine wanautumia umeme mwingi.

Hivyo si kweli kwamba wateja wanaotumia unit chini ya 75 wanalipa gharama za huduma. Kama una swali lolote tupigie 0800 780 800. Kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu
 
hilo shirika ni jipu kubwa sana yaani hizo sababu ulizoweka hapo ndio zinawafanya mkate hizo charge??aibu sana hii nchi.
 
Siyo kweli, situmii zaidi ya unit75 kwa mwezi lakini service charge nalipa, na ni zaidi ya 5520. Waongo hao.
 
Siyo kweli, situmii zaidi ya unit75 kwa mwezi lakini service charge nalipa, na ni zaidi ya 5520. Waongo hao.

Umenena vyema! hata wanao tumia umeme chini ya unit 75, service charge iko palepale.Kichekesho ni pale transfoma yao inapokorofisha mtaani kwenu; mtakosa umeme kwa miezi kadhaa huku mkiwapigia simu na kuwabembeleza mara kwa mara wakati wao ndio watoa huduma; na siku wakiwarudishia huo umeme un
utatakiwa kulipia hiyo service charge tangu hilo transfoma lao lilipoharibika wakati hukupata huduma ya umeme kwa muda wote huo! yaani wameiweka fixed! huu ni wizi wa asubuhi.

Bado hapo umeme haujakatakata hovyo, mara mgao! mara luku zimeisha, mara subiri nguzo!! kiujumla TANESCO ni janga kama majanga mengine. Bora serikali ikalifumua na kuliboresha hili shirika kwa kweli.
 
Hivi kuna tofauti gani na wenye daladala wakianza kutoza service changes kwa ajili ya magari yao. Baada ya abiria kulipa nauli ?
 
Tanesco ni washenzi na wezi kwani wasi query data za wateja wao wakaona Kama wapo chini ya unit 75 wakawaweka kwenye D1?
 
Hao wateja walisolipa service charge (wa chini ya 75) ikitokea itilafu ya waya, nguzo au lolote uliloeleza mnawatoza gharama za huduma hiyo? Kama siyo, mbona siyo fair sasa? kama service charge kufutwa ifutwe kwa wote, kama ni kulipa tulipe wote. Kwani nguzo ya mwenye unit 75 na mwenye unit 100 ni tofauti?
 
Wezi wakubwa watu wato wanalipia hyoo huduma isipokuwa mpaka wakutoe kwenye hyo system upelekwe kwenye tarif zeromkama sikosei ndio hukatwi hyo service charge
 
Fragmented thinking, nchi hii tuna akili chache sana. Kwa hiyo service charge ni kama insurance??? Kwanini msiyafanye malipo yote yawe consolidated? It will take years before we can get people who think in public offices.
 
Back
Top Bottom