Maegesho ya magari ya serikali zimehamia baa?

Mlangaja

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
579
218
Ni jambo la kusikitisha na kutia aibu pale unapotembea kila baa katika kila mji wa nchi hii na kukutana na misururu ya magari ya serikali yameegeshwa baa. Kwa mda mrefu nimetafakari suala hili, inaniuma sana kwani kwa moja kwa moja hela yangu inatumika kuwaweka watu baa. Wana jf naombeni mawazo yenu.
Je sheria inasemaje kuhusu matumizi ya magari ya serikali?
Je wizara inayohusika inafanya kazi gani? Na je kuna haja ya kuendelea kuwa na wizara hiyo pamoja na wafanyakazi wake? :angry:
Kwa mtindo huu taifa linakwenda wapi?
 
Mafisadi ambao unawaona leo walianza kwa kutumia vibaya baisikeli za serikali. Sasa tuna vifisadi, fisadi, mafisadi, na mafisadi papa. Tusipokuwa waaminifu kwa mambo madogo hatutakuwa waaminifu kwa mambo makubwa. Kumbuka mseomo usemao mazoea ni kilema.
Fitina tu hapa hakuna kitu.
 
bora umeliona hili,hapa dawa ni moja tu hamna kingine ..tukiyaona mitaa ya baa kuanzia saa2 usiku ni kutoa pumzi ama choma tairi kwa msumari,hii ndo dawa pekee ...humo ndani huwa wameiba wake za watu na vtoto vya shule
 
Na sasa wapo hapa Mjengoni watoto wa kike kwenye vyuo vyetu watapata shida...nawasihi wahadhiri muongeze assignment na test angalau tuwaokoe watoto wetu...Lo!
 
Tupe namba za magari na baa ipi uliyaona, siku gani na saa ngapi ndipo utakuwa umeisaidia serikali, walalamikaji mmekuwa wengi ...............unafikiri serikali itaota ndoto ya gari uliloliona baa bila kwanza wewe mwenyewe kuwa shaidi wa kwanza umeyaona wapi............kumbuka kwamba sina maana kwamba magari ya serikali hayaegeshwi baa.
 
naam sirikali ya bongo waacheni wale bata jamani kwa kuwa wengi wao wamepata madaraka kwa kuyagharamia
 
Back
Top Bottom